Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
Kwa uelewa wangu maana ya Fly-over Interchange ni makutano ya barabara nyingi za juu na zenye mizunguko mingi inayo ifanya magari kubadilisha barabara na kuendelea na safari bila kusababisha foleni na yenyewe kutokaa katika foleni katika makutano hayo.
Kwa definition hiyo ningependa kutoa rai kwa mara nyingine tena kwa wote wanao husika na ujenzi na usimamizi wa Ubungo Flyover Interchange ya kwamba mwonekano wa hiyo interchange kwenye hiyo clip sidhani kama utaleta result ambayo inategemea kupatikana. Kwa mtazamo wangu na uelewa wangu wa maana ya Interchage, haitakuwa busara kama hiyo interchange ita kuwa na level tatu tu. Level nne zinatakiwa.
Trafic lights kwenye flyover Interchange haitakuwa na maana yeyote katika mkutano hayo. Kwa kadri siku zinavyo kwenda, mji utazidi kupanuka na magari yata zidi kuongezeka kiasi kwamba baada ya mda sio mrefu itabidi kufanya marekebisho tena, kwani foleni zitaongezeka. Na hiyo ni gharama tena kwetu. Zaidi ya hapo ajali ambazo zitasababishwa na hizo trafic lights, zita kuwa kubwa mno na isitoshe umeme usio na uhakika utalazimisha trafic police ku-direct magari. Ushauri wangu kwa wahusika level nne zina takiwa badala ya tatu.
Barabara ya magari yanayo toka mjini kuelekea Mwenge na U-Turn yake kurudi mjini na yale ya kutoka Morogoro kuelekea Nelson Mandela Road na U-Turn yake kurudi Morogoro yawe katika level moja na barabara ya magari yanayo toka Mwenge kuelekea Morogoro na U-Turn yake kurudi Mwenge nayo yanatakiwa yawe kwenye level moja na barabara ya magari yanayotoka Neleson Mandela Road kuelekea mjini na U-Turn yake kurudi Nelson Madela Road. (Angalia picha)
Magari ya kutoka Station ya Mabasi ya Mikoani ya Ubungo kwenda mikoani au Nelson Mandela Road yanabidi kupita chini ya Morogoro Road, nyuma ya stand ya mabasi yaenda kasi kwenda Kimara, na kuibukia upande wa pili. Na yale ya kuingia Bus Station yanatakiwa yaingie chini ya Morogoro Road, mbele ya stand ya mabasi ya Mwendo Kasi, na kuibukia upande wa pili wa Station ya Mabasi ya mikoani ya Ubungo.(Angalia picha)
Barabara ya Morogoro Road kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja inatakiwa ijengwe upya. Inatakiwa iwe na barabara nane. Barabara au Lanes nne kila upande. Lanes mbili za katikati kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi kila upande. Katika hizo lanes tatu za kila upande, moja ni ya moja kwa moja kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja au vice versa. Hizo lanes mbili zilizo baki kila upande ni kwa ajili ya magari yanayo pinda kulia au kushoto na magari yanayo ingia kwenye main road.
Morogoro Road kutoka Ubungo Interchange mpaka Mnazimmoja isiwe na trafic Lights. Kwenye intersections ndogo ndogo kama za Magomeni na Fire Brigade, Morogoro Road inapita juu na hizo nyingine zinapita chini. Nazo zina kuwa na interchanges, lakini bila flyovers. (Angalia picha)
Njia za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu kila upande. Vivuko vyote vya waenda kwa miguu lazima viwe juu. (Angalia picha)
Kazi hizi za kutengeneza intersections au interchanges kama za Magomeni na Fire Brigade hazihitaji makampuni kutoka nje. Wahandisi wetu na makadarasi wetu wanaweza kufanya hizi kazi I am sure, wanatakiwa wawe na vifaa muhimu kama Tanroad na makampuni mengine.
Kinacho takiwa hapa ni usimazi mzuri. Wasimamizi wanatakiwa wajue nini kina endelea na sio wale walio somea miembeni.
Asanteni sana.