Ubunifu ni tabia muhimu sana katika utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii, lakini pia katika kuzalisha fursa mbalimbali za biashara.
Kama nilivyoeleza huko nyuma, fursa ya biashara ni tunda la wazo zuri la biashara.
Watu wengi wanachanganya matumizi ya maneno haya; yaani wanasema wazo la biashara ndio fursa ya biashara. Ukweli haya ni maneno yenye maana tofauti, ingawa yana uhusiano wa karibu.
Kupata wazo la biashara ni hatua ya kwanza kabisa katika mchakato wa uanzishaji wa biashara. Wazo ni dhana , ambayo inaweza kutumika katika kuanzisha uzalishaji wa bidhaa au utoaji huduma.
Katika kuhangaika ili apate kitu cha kufanya, tengeneza hamu au hamasa ndani ya ubongo wako ambayo mwisho wake huzaa mawazo mengi ya vitu vya kufanya.
Kutokana na mawazo haya, mtu huchagua wazo moja analovutiwa nalo zaidi ili aje kulitekeleza kivitendo baadaye.
Hata hivyo, wazo peke yake kichwani halina thamani yoyote. Na ukweli ni kwamba, mawazo mengi ya biashara huendelea kuogelewa tu, katika akili za watu, bila kuleta manufaa yoyote – hadi pale yanapotiwa katika vitendo.
Sasa, wazo la biashara lililoundwa akilini, halafu likafanyiwa utafiti au tathmini, na likaonekana linawezekana kufanyika – na linaweza kuleta manufaa kwa jamii; na faida au tija– ndio huzaa kitu kiitwacho fursa.
Watu wengi tunapata taabu sana kutengeneza wazo la biashara linaloweza kufinyangwa kuwa fursa. tunajitahidi kutazama huku na huko, au kusikiliza hiki na kile; lakini macho yao hayaoni, wala masikio yao hayasikii kitu.
Kwa ukweli, mawazo mengi yanayoweza kubadilishwa kuwa fursa yanakuja kwa msaada maalumu wa ‘macho na ubongo’.
yanaweza kubaini kitu kilichojificha ndani ya kitu kilicho mbele ya macho ya kawaida.
Mtu mwenye macho maalum ana uwezo mkubwa wa ubunifu pia.
Hatua ya kuchukua:
Ni lazima tubadili namna tunavyoyaona mambo au tunavyoitazama dunia.
Kila tunapotazama kitu, lazima tufanye hivyo kwa kuyashirikisha macho ya ubongo.
Haya ni macho maalum yanayotusaidia kwenda mbele zaidi ya macho ya kawaida, na kutengeneza mawazo ambayo huzaa fursa.