Ubunifu unaiua Sahara Media Group

Nakazia. UBORA ni tatizo sugu kwa radio na tv hasa tv hapa Tz. Miaka inavyozidi kwenda na ubora unapungua.
Wangekuwa makini katika kuandaa maudhui wasingekosa matangazo na sponsors walio tayari kutoa pesa nyingi sana.
 
Itakufa? Au ishakufa!
 
Sahara media ubunifu siku hizi ni zero, wamenasa na vipindi vilevile huku miaka imeenda. Kipindi hicho marehemu Fredwaa aliinogesha asubuhi vilivyo na sindano tano za moto, ukija usiku kipindi cha michezo na muziki wa DRC. Unakuja jumapili usiku vikota kutoka Mumbai huko. Ila sasa nyakati zimebadilika na mambo yamebadilika pia. Kwa startv content zao ni zilezile hadi leo na hazina ubunifu wowote ule ila wanafanya kimazoea tuu. Ukiangalia baadhi ya vipindi kama vile futuhi na wale akina mkombe wako vilevile hawachekeshi tena sababu ya kukosa ubunifu. Mimi nilishaacha kuitizama startv aisee
 
Anthony diallo bora angeiuza hii redio sema wasiwasi wangu sijui km ccm watamkubalia
 
Ukongwe hausaidii kama hutoendana na mabadiliko
 
Baba kwenye sindano za moto na Fred waa na kile kipindi cha hakuna kulala na beat ya juma nature πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Biashara ya utangazaji ilishapitwa na wakati sana. Tanzania bado biashara inasurvive kwa mbinde mbinde kwa sababu wenye media hizo wanatumia mbinu nyingine kijipatia kipato, siyo utangazaji tu. Halafu nchi yenyewe isiyokuwa na biashara nyingi ya utangazaji lakini ina wingi wa vituo vya redio na TV unadhani matangazo hayo ya kutosheleza vituo vyote yatatoka wapi.
 
Nakazia. UBORA ni tatizo sugu kwa radio na tv hasa tv hapa Tz. Miaka inavyozidi kwenda na ubora unapungua.
Wangekuwa makini katika kuandaa maudhui wasingekosa matangazo na sponsors walio tayari kutoa pesa nyingi sana.
Kweli kabisa na haipingiki! Kwanza Sahara media ndio ingekuwa inakimbiza Tanzania nzima lakini sasa ndio hivo unasikia hata hela haina.
 
Media inafaida kubwa sana ila wenye media hawana maono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…