Ismail Tano
Member
- Jul 23, 2022
- 7
- 1
Moja kati ya tabia kuu zinazokwenda sambamba na kazi yoyote ya kibunifu ni kueleweka kwa taratibu, kueleweka baada ya muda flani au kutokueleweka kabisa hata baada ya muda kupita hii ni kutokana na kazi za kibunifu kuhusisha utofauti kama nguzo yake kuu na kupinga ufanano.
Hii huwa inajitokeza kutokana na nature ya mwanadamu kupenda hali aliyoizoea, wataalamu wa lugha ya kigeni wanaiita confort zone. Hii ni ile hali ya kuishi kwenye maisha au kuwa kwenye hali ambayo umeizoea tu na kuepuka kitu chochote ambacho ni kipya.
Na hii ndio hali ambayo klabu ya Young Africans pamoja na designer wa jezi zake bwana Sheria Ngoi wanakutana nayo kwa siku za hivi karibuni baada ya kutambulisha jezi mpya kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2022/23.
Mapokeo yamekuwa tofauti matarajio ya wengi si kwa mashabiki wa timu pinzani ila hata kwa mashabiki wa timu wenyewe, wapo walioponda na kubeza ubunifu na akili iliyotumika kwenye mchakato wa upatikanaji wa jezi hizo.
Jezi za team ni kama gwanda za jeshi tu, ni utambulisho wa team na husimama kama alama ya team ni kama vile nembo ya team ambapo kila kitu kilichopo ndani yake huwa kimesimama kwa niaba ya kitu fulani kinachohusu team husika.
Itachukua muda kuelewa au huenda isieleweke kabisa kwa baadhi ya watu ila hongera za dhati ziende kwa mbunifu wa jezi mpya za Young Africans pamoja na uongozi mzima wa Young Africans katika kuamini kwenye ubunifu.
Jezi zimebeba maana kubwa na historia kubwa ya klabu ya Young Africans kiujumla hivyo katika kuibeza jezi unaibeza pia historia ya klabu.