Ubunifu wa Profesa Kapuya alipokuwa Waziri wa Elimu na fomu za kujiunga Msalato sekondari

Ubunifu wa Profesa Kapuya alipokuwa Waziri wa Elimu na fomu za kujiunga Msalato sekondari

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Kazi ya waziri wa Elimu ni kuwa Mbunifu Tanzania ilipata waziri wa elimu Profesa Juma Kapuya .

Aliposhika uwaziri ubunifu aliobuni ni wa kutaka shule zote za msingi na sekondari za Serikali watoto wa kike wawe wanavaa kiislamu kwa kuvaa vile vifunika uso na akaagiza walimu wakuu wasimamie hilo kuhakikisha kuwa kila msichana mwislamu avae hivyo.

Akajigeuza Ayatollah mtawala wa kiislamu wizara ya elimu mwenye kazi ya kusimamia mavazi ya wasichana wa kiislamu mashuleni

Huo ndio ukawa mwanzo wa uvaaji wa sare kwa wasichana wa kiislamu tunaouona leo shule za Serikali

Mtoto wa dada yangu mwanae alifaulu kidato cha tano kwenda shule ya sekondari ya wasichana Msalato Dodoma .Fomu ya kujiunga iliyokuja ilikuwa na sehemu ikieleza msichana kama ni muislamu aje na mavazi gani. Dada yangu akasema hivi hiyo ni shule au madrasa ya kiislamu hakumpeleka mtoto

Nauliza hivi hiyo shule ya Msalato bado hizo joining instruction ziko hivyo? Kuwa kazi ya mwalimu mkuu ni kusimamia uvaaji wa wasichana wa kiislamu?
 
Sasaivi hata Trafiki na polisi waruhusiwe kuvaa hijab na nikabu mbona waroma wanavaa rozali shuleni wakati kisheria haziruhusiwi.Hata mambo ya udini yanaathiri sana kwenye vichwa vya watu ukichukulia neg-

Mtoto wa Dada ako anaendeleaje saizi ?Weka namba yake hapa mabaharia tuchangamkie fursa ya uncle wako aliefaulu msalato akahamishiwa kusikojulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasaivi hata Trafiki na polisi waruhusiwe kuvaa hijab na nikabu.mbona waroma wanavaa rozali shuleni wakati kisheria haziruhusiwi.Hata mambo ya udini yanaathiri sana kwenye vichwa vya watu ukichukulia neg-
Shule gani ya serikali ambayo inalazimisha waroma kuvaa rozali? Na Ni agizo lililomo kwenye joining instruction?
 
Shule gani ya serikali ambayo inalazimisha waroma kuvaa rozali? Na Ni agizo lililomo kwenye joining instruction?
Upuuzi tu, kama joining instruction inatoa option kwa muislam kuvaa hivyo tatizo liko wapi?
Unataka kusema walikuwa wanakazimishwa?
Acha ujinga.
 
Upuuzi tu, kama joining instruction inatoa option kwa muislam kuvaa hivyo tatizo liko wapi?
Unataka kusema walikuwa wanakazimishwa?
Acha ujinga.
Jamaa kaeleza vizuri tu kwamba joining instruction (shule ya umma) ilielekeza wasichana wa kiislamu wavaeje.
 
Subiri waje wanaoweza elewa Kama kazi ya waziri na mwalimu.mkui kazi yake Ni kusimamia watu wa dini ya kiislamu wavaaje uniform Shuleni

Mwambie Ndalichako afute Uvaaji wa Hijab basi kama ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Prof Kapuya!
 
Mwambie Ndalichako afute Uvaaji wa Hijab basi kama ulikuwa ni uamuzi binafsi wa Prof Kapuya!
Issue tunayoongelea hapa Ni kuweka kwenye joining instruction na kumpa jukumu mwalimu mkuu alisimamie na ahakikishe limo kwenye joining instruction

Hii Ni kumgeuza mwalimu mkuu kuwa Ayatollah mtawala na msimamizi Sheria za kiislamu shuleni
 
Leo watu mmeamkaje kwani? Yaani mambo yaliyofanywa enzi za Mzee Kapuya yanaletwa leo, kisa nini hasa?

Mwacheni mzee wa watu apumzike na mke wake mpya!!
 
Si kweli hakuna joining instruction kwenye shule za serikali zinazolazimisha wanafunzi wa kike wavae mavazi ya kiislam..hiyo ni option ya mwanafunzi akipenda atavaa asipopenda ataacha.......vijana wa ccm siku hizi mbona hoja zenu mfu jamani
 
Nimetoa na mfano specific kabisa.Joining instruction za shule ya sekondari msalato.
Wizara ya elimu kazi.kwenu. Pitieni hiyo.ya msalato ninayoongea kwa uhakika
 
Ukimuuliza mfano Profesa Juma Kapuya kuwa Nini unachojivunia kikubwa ulichofanya ulipokuwa waziri wa Elimu? Atakujibu nilifanikisha kwa kusimamia
watoto wa kike wa kiislamu kuvaa hijabu mashule yote ya serikali!!!

hayo ndio.mafanikio makubwa ninayojivunia
Mkuu wakivaa hivo wanapunguzia nini wengine ambao hawavai?, Inawaathiri kitaaluma?.

Je mwalimu mkuu asiposimamia hayo nini kinamkuta, kuna hatua zozote anachukuliwa?.

Nini kazi ya walimu walezi katika dini husika, kama hio nikazi ya mwalimu mkuu?.

Je mwanafunzi wa kiislam asipovaa hivo kuna hatua gani anachukuliwa?, Anafukuzwa shule?.

Je wewe binafsi unapendekeza utaratibu upi ufanywe?.Maana naona hilo lahijabu kwa sasa kila shule inalitolea maelezo hasa shule za Serikali kuwa wavaaje, ingawa nafaham hawalazimishwi.

Je vipi mkuu vipindi vya dini navyo mashulen, sibora vifutwe ili wanafunzi wasijihusishe na dini kabisa wawapo shuleni,ili kazi yao ibaki kusoma tuu?.

Kwa nini kama inaonekana nikinyume Serikali ya ccm isifute huo utaratibu?.

Uvumilivu wakidini mahala popote unatakiwa, kama kuvaa hivo wanavyovaa haiathiri chochote haina haja yakushadadia mambo madogo kama hayo.Badala yakuzungumzia uboreshwaji wa elimu kuanzia shule za kata, mpaka vyuo vikuu ili kutoa wahitimu bora.
 
Issue tunayoongelea hapa Ni kuweka kwenye joining instruction na kumpa jukumu mwalimu mkuu alisimamie na ahakikishe limo kwenye joining instruction

Hii Ni kumgeuza mwalimu mkuu kuwa Ayatollah mtawala na msimamizi Sheria za kiislamu shuleni

Joining Instructions za Shule haziandaliwi na Waziri.
 
Back
Top Bottom