warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Nimependa sana huu ubunifu mpya wa mwanamuziki Benpol, audio yake ilinichosha kidogo, sio kwa kuwa wimbo mbaya la hasha!, ila haya mambo ya kuimbia mapenzi tu mara wanjera, sijui masogange na nyimbo kama hizo zilinifanya nisione jipya kwenye nyimbo zao.
Nilibahatika kuiona video mpya ya Benpol, kwa kweli ilinisisimua sana baada ya kumuona sophia aliyekuwa akimuimbia maneno matamu alikuwa ana ulemavu wa ngozi (albino ), licha ya ulemavu alionao bado alionekana kuwa binti mzuri na anayevutia, kwa kweli nilipenda sana kuona ubunifu mpya.
Ameonyesha usawa na haki katika mapenzi, kuwa kila binadamu ana haki ya kupendwa na kupenda awe na ulemavu au lah. Haya mambo ya kuwaimbia wanawake wenye makalio makubwa tu na uzuri wa kununua madukani tumeyachoka, sijui msambwinunga tumeyachoka, tunahitaji radha mpya kama izi, hongera bro, big up.