Ubunifu wa video mpya ya Benpol (Sophia)

Ubunifu wa video mpya ya Benpol (Sophia)

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Nimependa sana huu ubunifu mpya wa mwanamuziki Benpol, audio yake ilinichosha kidogo, sio kwa kuwa wimbo mbaya la hasha!, ila haya mambo ya kuimbia mapenzi tu mara wanjera, sijui masogange na nyimbo kama hizo zilinifanya nisione jipya kwenye nyimbo zao.

Nilibahatika kuiona video mpya ya Benpol, kwa kweli ilinisisimua sana baada ya kumuona sophia aliyekuwa akimuimbia maneno matamu alikuwa ana ulemavu wa ngozi (albino ), licha ya ulemavu alionao bado alionekana kuwa binti mzuri na anayevutia, kwa kweli nilipenda sana kuona ubunifu mpya.

Ameonyesha usawa na haki katika mapenzi, kuwa kila binadamu ana haki ya kupendwa na kupenda awe na ulemavu au lah. Haya mambo ya kuwaimbia wanawake wenye makalio makubwa tu na uzuri wa kununua madukani tumeyachoka, sijui msambwinunga tumeyachoka, tunahitaji radha mpya kama izi, hongera bro, big up.
 
Sasa ivi tunataka wasanii wengine muimbe umefall in love na mwanamke mbea Dinazarde, licha ya watu kumponda una mwanamke mbea na mchonganishi ila moyo wako ndo ushatua ,inapendeza, kuna watu wana fall in love na walemavu wa aina nyingi na maisha yanaendelea, inasisimua na kupendeza mapenzi kwa wote, sio kila siku akina masogange, kwan peke yao ndo wana K
 
Last edited by a moderator:
Halafu yule Albino mzuri sana na ameutendea haki ule wimbo
 
Hili niliwahi kuliona kutoka kwa Maurice Kyria na niliipenda sana ile video hadi nilitoa machozi the way jamaa alivyoonesha kumpenda na kumjali mpenzi wake ambaye ni Albino.
Nilitamani kuona mbongo nae akifanya hivyo,japo sijaiona ila kama Ben kafanya hivyo basi hongera zake.
 
Boda Boda hurry hurry I need my
Baby!
 
Mi kuna kitu sijakiona kwenye video ya sophia. Kwa nini hajatengeneza ki script akiwa anamdinya huyo mrembo??!!! Alitakiwa aonyeshe anampa mambo kwa bed. 😛😛😛
 
Mi kuna kitu sijakiona kwenye video ya sophia. Kwa nini hajatengeneza ki script akiwa anamdinya huyo mrembo??!!! Alitakiwa aonyeshe anampa mambo kwa bed. 😛😛😛

Ili ufungiwe au unataka nn? ,kweli kuna mtu humu alisema "common sense is not common to all common people".
 
Mi kuna kitu sijakiona kwenye video ya sophia. Kwa nini hajatengeneza ki script akiwa anamdinya huyo mrembo??!!! Alitakiwa aonyeshe anampa mambo kwa bed. 😛😛😛

pumbavu kabisa wewe
 
Hili niliwahi kuliona kutoka kwa Maurice Kyria na niliipenda sana ile video hadi nilitoa machozi the way jamaa alivyoonesha kumpenda na kumjali mpenzi wake ambaye ni Albino.
Nilitamani kuona mbongo nae akifanya hivyo,japo sijaiona ila kama Ben kafanya hivyo basi hongera zake.

Inasisimua sana, ni kitu ambacho hakikutegemea, yani kalenga sana ukizingatia kipindi hiki cha mauaji ya ma albino, kachangia sana kuwafariji na kujioa wana haki, Mungu ambariki sana, binadamu wote ni sawa, na wote wanahitaji kupendwa na kupenda, jamaa kaweza.
 
Mi kuna kitu sijakiona kwenye video ya sophia. Kwa nini hajatengeneza ki script akiwa anamdinya huyo mrembo??!!! Alitakiwa aonyeshe anampa mambo kwa bed. 😛😛😛

Unashangaza duh
 
Kijana yuko poa kimuziki istoshe ndio mgogo maarufu kuliko le mbebezzz hatumii nguvu kujulikana

Kwani ba mdogo ni mgogo? Mbona hajitangazi au anaona aibu kuwa mgogo? Anatamani walau awe msouth
 
Kwani ba mdogo ni mgogo? Mbona hajitangazi au anaona aibu kuwa mgogo? Anatamani walau awe msouth

Sio baba mdogo ni baba yake mkubwa yule huwa anasema yeye ndio mgogo maarafu tz.wakti ben ndio maarufu mpka wazee,vijana n watoto wanamjua
 
kwa hiyo umemsahau yule model wa kwenye wimbo wa Dudubaya-nakupenda tu.
 
Dah hiyo ngoma naikubali mno. Na hiyo video ametisha sana kwa ubunifu huo japo sijaiona.
 
kwa hiyo umemsahau yule model wa kwenye wimbo wa Dudubaya-nakupenda tu.

Ahahahah umenikumbusha mbali, yap alifanya poa, we need those swagg sasa, sio kila siku kuwasifia akina masogange
 
Back
Top Bottom