Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa taarifa yako Dar ipo karakana kule Oysterbay inayotengeneza vitu hivi, na baadhi vimewekwa mjini kwenye mizunguruko(keep left), na ukitaka kununua nenda kwenye hiyo karakana.Nimevutiwa na huu ubunifu na kipaji.. Pengine mitaala yetu ijayo itaangazia zaidi kwenye kutoa elimu isiyo tegemezi kwenye kuajiriwa tuu bali kwenye ubunifu, kuvumbua vipaji, kukuza vipaji, kujiajiri na kupunguza wimbi la vijana wasio na kazi mitaani
Ubunifu wa kutumia vitu visivyofaa tena kwa matumizi yake ya awali unaweza kuwatoa vijana wetu kwenye wimbi la
Vibaka
Kamari
Madawa ya kulevya na vilevi vingine nknk
Wanasema! An idle brain is a carpentry of a devil (akili isiyojishughulisha ni karakana ya shetani)
Majalala na mitaa yetu imejaa vitu vilivyoisha matumizi yake ya awali.. Kwa kutumia vipaji na ubunifu vitu hivyo badala ya kuachwa vichafue mazingira na kuhatarisha afya za watu vinaweza kuwa malighafi bora kwenye ununifu wa mapambo nknk
Nitaweka hapa kila nitakachokiona kinafaa kuwekwa kwa nia ya kuhamasisha wale wote wenye vipaji vya ubunifu na elimu pia lakini wapo mitaani vijiweni wakisubiri ajira za kuajiriwa na si kujiajiri na kuajiri
Natambua changamoto kubwa ya mitaji na support finyu ya serikali lakini lazima tuhamasishane kuna siku kitaeleweka
View attachment 2617339View attachment 2617340