Ubunifu wenye kipato na ajira

Ubunifu wenye kipato na ajira

34fca1d404e96da3f68d59a5fc320d70.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimevutiwa na huu ubunifu na kipaji.. Pengine mitaala yetu ijayo itaangazia zaidi kwenye kutoa elimu isiyo tegemezi kwenye kuajiriwa tuu bali kwenye ubunifu, kuvumbua vipaji, kukuza vipaji, kujiajiri na kupunguza wimbi la vijana wasio na kazi mitaani

Ubunifu wa kutumia vitu visivyofaa tena kwa matumizi yake ya awali unaweza kuwatoa vijana wetu kwenye wimbi la
Vibaka
Kamari
Madawa ya kulevya na vilevi vingine nknk
Wanasema! An idle brain is a carpentry of a devil (akili isiyojishughulisha ni karakana ya shetani)

Majalala na mitaa yetu imejaa vitu vilivyoisha matumizi yake ya awali.. Kwa kutumia vipaji na ubunifu vitu hivyo badala ya kuachwa vichafue mazingira na kuhatarisha afya za watu vinaweza kuwa malighafi bora kwenye ununifu wa mapambo nknk

Nitaweka hapa kila nitakachokiona kinafaa kuwekwa kwa nia ya kuhamasisha wale wote wenye vipaji vya ubunifu na elimu pia lakini wapo mitaani vijiweni wakisubiri ajira za kuajiriwa na si kujiajiri na kuajiri

Natambua changamoto kubwa ya mitaji na support finyu ya serikali lakini lazima tuhamasishane kuna siku kitaeleweka
View attachment 2617339View attachment 2617340
Ahsante sana kwa uhamasishaji na uelimishaji vijana wetu na sisi wazazi wao ili tuwakumbushe na kuchochea tunu na vipawa walivyozaliwa navyo. Wakivitambua na kuvitumia watafanikiwa kwa hakika kila vigeukapo. Mithali 17:8
 
Back
Top Bottom