Ubuyu na ukwaju

tama

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
602
Reaction score
71
Je kuna mapishi ya wali waweza tia juisi ya ukwaji au ubuyu ikanogo maana napenda sana hizo juisi natamani kupika hata kwenye chakula?
 
Mhh wali? Navyojua Ukwaju unawekwa kwenye mchuzi na kwenye urojo...hiyo ya wali sijawahi kusikia...
 
naemagine ukwaju ndani ya wali duu!! ila mapishi utundu, mayb jaribu unaweza fanikiwa
 
Je kuna mapishi ya wali waweza tia juisi ya ukwaji au ubuyu ikanogo maana napenda sana hizo juisi natamani kupika hata kwenye chakula?

Lol, we jaribu tu halafu uje utupe mshindo nyuma hapa
 
juice ya ubuyu na ukwaju na hiliki dah....tamu mno
 
yaani ni sawa na wali utie ndimu.hahahaaaaa uuuwiiiiiiiii.
 
yaani ni sawa na wali utie ndimu.hahahaaaaa uuuwiiiiiiiii.

Wali ukitiwa ndimu unachambuka haswaa..
ILa ukwaju kwa wali mhh hiki ni kitimtim jikoni
 
Jamani hv ukwaju na ubuyu vina nafasi gani kwenye mwili wa binadamu.
 
Ubuyu na ukwaju kwenye wali mi naona haitakuwa nzuri... Hivyo vibaki kuwa vya juisi tu au ukwaju pia hutumiwa wakt wa kula chakula km tunavyoona ukinunua chips baadhi ya sehemu huwa wanakuwa na ukwaju unamix km vile unavyomix tomato sauce na chakula chochote.
 
mi ukwaju kama ndimu, kwa wali haiendi naona. ila kwa juice na kwenye chachandu mashaallah
 
Jamani hv ukwaju na ubuyu vina nafasi gani kwenye mwili wa binadamu.

1) Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini
‘antioxidants’ ambavyo huzuia Saratani
(cancer)
2) Chanzo cha Vitamini B na C vile vile
“carotentes”
Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, h
asa homa ya malaria na homa ya matumbo
3) Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za
mafua kooni
Husaidia myeyusho na mmengenyo wa
chakula na kuondosha kuvimbiwa
4) Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile
disorders)
5) Husaidia kurahisisha choo (laxative)
6) Husaidia kupunguza wingi wa lehemu
(cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
7) Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile
husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua
au yenye vidonda
8) Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa
watoto wadogo)
9) Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile
husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua
au yenye vidonda
10) Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa
watoto wadogo)

www.hassan.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…