Ubuyu wa Zanzibar

Ina maana nyie Wazanzibar wenzangu hampo au dharau? Kwa hisani yenu tuelekezeni jamani, mana wengine sie tuna mimba changa so plzzzzzzz jamani,

Mi niko mbali kidoogo na jiji la bandar salama nikijaaliwa kurudi salama ntakutumia kashata za ubuyu hizo ni tamu kuliko.
 
Kama kuna mtu yoyote anayejua jinsi ya kutengeneza ubuyu ule wa rangi wenye pilipili wanauita ubuyu wa zanzibar anielekeze pls
Hii ndio Jamii Forum kisima cha yote ingawa utanyimwa Elimu lkn wako watakaokupa hapa Mrs Kharusy nampa maksi ... kwani anaelewa ila amekupa Hint ukahangaike
jc--
  • chambua Ubuyu km 2kg wako kuondoa nyuzinyuzi na mwishowe
  • uutenge unga wake na
  • ubuyu wenye tete (mbegu)
  • chukua Sukari nusu kilo,Ice sugar (sukari atificially) rangi ya Ice cream, Vanila au hiliki,
  • Sufuria kavu kabisa
  • Moto, mwiko, na maji kidogo

Hatua za kufanya
  • anza kuikaanga sukari hiyo nusu kilo ikiwa kavu mapaka iyeyuke
  • ongeza maji km kikombe cha chai tu
  • changa viungo vyako km vanila, rangi ya Ice-crfam, pilipili
  • hakikisha mpaka linatokea povu kubwa ndani ya viungo hivyo.
  • sasa weka unga wa ubuyu na ukorogr mpaka litokee liUji zito
    • Epua mara moja na uuingize ubuyu wako wote ule wenye mbegu na koroga chini / nje ya moto kwa mwiko.
    • Ni vizuri ukawa unapepeta hiyo sufuria ili ubuyu usivunjikevunjike au knatana km ugali
acha upoe kwa muda
Na sasa ubuyu wako ni tayari wa matumizi ya kumumusa
 
Last edited by a moderator:

Hahaha..sikumuacha akahangaike hivo ndo nijuavyo mm. Anyway vizur na ww umetupa ilu kidogo sikuwahi jua km hio sukar inaunguzwa km ya puding kwahio one day ntaajaribu kuinguza nione utofauti.
 
Last edited by a moderator:
Asanteni jamani. Pia baada ya kusumbuka sana kutafuta huu ujuzi,juzi nimepata hii video from youtube. Inaonyesha step by step. Fungua hii link
http://m.youtube.com/watch?v=2tgSTVRlZOs , kama nimekosea kuweka link nenda youtube search how to make.mabuyu. thanx kwa wote mliotoa mawazo yenu hapa.
 
Reactions: Kbd
Dah JF kuna raha zake. Asanteni woote tumepata elimu. Halafu ubuyu ni dawa jamani si kwamba ni kitu cha kumumunya kwa starehe ni kwa afyaa
 
Reactions: SDG
Sasa mwenye kufahamu kutengeneza kashata za ubuyu atujuze
 

Mrs Kharusy unaweza toa ratios za hivyo vitu?
 
Ukishakuuchambua Ubuyu wako, weka taratibu kwenye shira ili uweze kukisia...usiumimine wote kwa pamoja.
Kipimo exactly sikijui cha mabuyu mm hukisia tu
Thanks for reply, je ubuyu au hilo shira lina chemshwa? Na je inawezekana kuweka maziwa?. Please usinchoke nataka kufanya practically na ntakupa mrejesho.
 
Thanks for reply, je ubuyu au hilo shira lina chemshwa? Na je inawezekana kuweka maziwa?. Please usinchoke nataka kufanya practically na ntakupa mrejesho.

Mkuu hio shira ukiitia maziwa badala ya maji nahisi itakua fagi. Ww chemshia na maji tu.
Na ubuyu hua mkavu ila yapo mapishi ya ubuyu wa rojo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…