Uchache wa abiria na mizigo wafanya SGR nchini Kenya kuendeshwa kwa hasara. Je, Tanzania tutakwepa hali hii?

Uchache wa abiria na mizigo wafanya SGR nchini Kenya kuendeshwa kwa hasara. Je, Tanzania tutakwepa hali hii?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hi ni habari katika mtandao wa The Africareport.com ambapo imeripoti kuwa, uchache wa abiria na volume mdogo ya mizigo plus madhara ya COVID19, kumesababisha reli hiyo kuendesheshwa kwa hasara na sasa wanashindwa kulipa mkopo uliotumika kujenga reli hiyo.

Habari hii inaeleza kuwa, tatizo lilianza kabla hata Covid haijaingia na ujio wa Covid umechangia tu tatizo kuwa kubwa.

Swali:Kama Kenya yenye viwanda vingi kutuzidi, wanakuwa na uchache wa mizigo na kupelekea shirika lao kujiendesha kwa hasara,sisi wenye viwanda vichache ndio tutamudu kuendesha SGR yetu kwa faida?

Hata kama mkopo uliotumika kujenga reli hii utakuwa haulipwi kutokana na mapato ya kuendesha reli hii, tunaweza kukwepa hasara iwapo volume ya mizigo ni moja ya chanzo kikuu cha mapato na huku viwanda hatuna vya kutosha?

Naiona hatari ya serikali kubeba mzigo wa SGR hiii sambambamba na ATCL.

Muda utasema.

Kenya: China faces a critical test in train debt
 
Hii Ni miradi ya kutakasishia Kodi zetu bado si msaada kwa watz
 
Kwa hiyo SGR Kenya wakipata hasara na SGR Tanzania itapata? unajua gharama za kuendesha electric locomotives ukilinganisha na diesel locomotives? Kenya wanatumia diesel locomotives ambazo gharama zake za uendeshaji kubwa sana wakati Tanzania treni zake zitatumia umeme ambazo gharama zake za uendeshaji ni ndogo sana.
 
Kama wakenya na uchumi wao mkubwa kuliko wetu wanapata hasara, sisi hatuwezi kunusurika kupata hasara pia, japo inaweza kuwa kidogo, sababu wanasema SGR ya Kenya imejengwa kwa mkopo kutoka China, hivyo kuna mapato ya SGR ya Kenya serikali ya China inayachukua moja kwa moja kwa kipindi fulani (sikumbuki ni miaka mingapi).

Hii SGR ya kwetu wanasema inajengwa kwa fedha zetu za ndani, hivyo inawezekana serikali itakuwa inakusanya mapato moja kwa moja baada ya mradi kukamilika, jambo la msingi ni gharama za uendeshaji, je, wataweza kuzifanya ziendane na hali ya kipato cha mtanzania wa kawaida ili wengi waweze kumudu gharama za huo usafiri? ukizingatia hali mbaya ya uchumi wa mtanzania wa kawaida ilivyo hivi sasa, wakiweza ni vizuri; vinginevyo, SGR inaweza kugeuka Bombardier wataoweza kumudu gharama ni wachache.
 
Huu mradi Tanzania tumebebeshwa mzigo tusioujua, huu ni mradi wa Kagame ila tunamjengea kwa pesa zetu za ndani.
 
Duuu! Aisee kumbe kuna watu wajinga kiasi hiki? Umeishia darasa la ngapi wewe?
Wewe ndiyo ziro brain kabisa sijui shule mnaenda kusomea ujinga yaani hujui cost-benefits za railway electrification ukilinganisha na Diesel locomotives. SGR ya Kenya inatumia diesel locomotives ambazo gharama zake za uendeshaji ni kubwa sana lakini SGR ya Tanzania itatumia train za umeme ambazo gharama zake za uendeshaji ni ndogo sana hivyo hakuna hasara yoyote itakayopatikana kwa Tanzania. Kwa kutumia umeme watakuwa wamepunguza gharama za uendeshaji kwa kiasi kikubwa sana.
 
Hii sgr ya tz itakua yaumeme tofauti nakenya ambayo niyamafuta, hii ndoo tofauti kwenye uendeshaji ya umeme nirahisi zaidi.
Kwa kutumia umeme watakuwa wamepunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana kwenye mafuta, kununua spare na service hasa ukizingatia injini za umeme hazina parts nyingi sana ukilinganisha na injini za diesel.
 
P

Hii SGR itakuwa na faida ya kijamii zaidi kuliko kiuchumi.Kiuchumi tutarajie loss tu.
Wewe elimu itakuwa haijakusaidia kitu chochote yaani treni inayotumia umeme utegemee kupata loss? Hivi shuleni ulienda kusomea ujinga? yaani huwezi hata kujua cost benefits za electric locomotives ukiliganisha na diesel locomotives.
 
Kama tuna watu wenye mawazo kama haya basi Tanzania tuna safari ndefu sana kufikia maendeleo.
Bado ndefu Sana Kama ya Ethiopia wao wanayo kila kitu lkn ndo wanaoongoza afrika kwa kuikimbia njia yao.
 
Pole sana elimu yako haijakusaidia kitu chochote katika kupambanua mambo.
Miradi yote ni kichaka Cha upigaji na Wala sio kipaumbele Cha wananchi Bali Cha watawala kutakasishia Kodi zetu
 
Hii SGR ya kwetu wanasema inajengwa kwa fedha zetu za ndani, hivyo inawezekana serikali itakuwa inakusanya mapato moja kwa moja baada ya mradi kukamilika.

Heeee! Na wewe unamwini Magufuli? Jisomee hapo chini.
https://mof.go.tz/docs/news/STORY BENKI YA STANDARD CHARTED.pdf
IMG_20201001_221001_997.JPG
 
Hi ni habari katika mtandao wa The Africareport.com ambapo imeripoti kuwa, uchache wa abiria na volume mdogo ya mizigo plus madhara ya COVID19, kumesababisha reli hiyo kuendesheshwa kwa hasara na sasa wanashindwa kulipa mkopo uliotumika kujenga reli hiyo.

Habari hii inaeleza kuwa, tatizo lilianza kabla hata Covid haijaingia na ujio wa Covid umechangia tu tatizo kuwa kubwa.

Swali:Kama Kenya yenye viwanda vingi kutuzidi, wanakuwa na uchache wa mizigo na kupelekea shirika lao kujiendesha kwa hasara,sisi wenye viwanda vichache ndio tutamudu kuendesha SGR yetu kwa faida?

Hata kama mkopo uliotumika kujenga reli hii utakuwa haulipwi kutokana na mapato ya kuendesha reli hii, tunaweza kukwepa hasara iwapo volume ya mizigo ni moja ya chanzo kikuu cha mapato na huku viwanda hatuna vya kutosha?

Naiona hatari ya serikali kubeba mzigo wa SGR hiii sambambamba na ATCL.

Muda utasema.

Kenya: China faces a critical test in train debt
Maswali kama hili yalipaswa kujibiwa kwenye hatua za mwanzo za feasibility study kabla ya ujenzi kuanza.
Sasa ni too late!

Zaidi ya hivyo reli zitakuwa mbili, meter gauge na sgr zikiwa sambamba. Maana yake itafika wakati zatanyan'ganyana mizigo na abiria!
Ndiyo maana ya "kupanga ni kuchagua". Hatukupanga, kwahiyo tulipofika hatuna uwezo wa "kuchagua".
 
Kwa hiyo unasema SGR isijengwe au vipi? Mzee Mengi aliwahi kusema kitu kama kuwa ukiogopa hasara basi baki na hela yako, na maendeleo uatendelea kuyasikia redioni tu.

Mojawapo ya sababu zilizofanya wazungu waendelee sana licha ya kutokuwa na raslimali ni jinsi walivyokuwa wakipambana na chellenges. Sisi chellenge zikija, tunaanza kulalamika kwa nini hatuzikwepa challenges hizo badala ya kupambana nazo.
 
Back
Top Bottom