Sio lazima Tanzania SGR ipate hasara kama Kenya, sababu ziko nyingi.
1. Imeshasemwa SGR ya Tanzania itatumia umeme ya Kenya Diesel. Hii kwa Tanzania itaokoa gharama nyingi za matengenezo, vipuri, uendeshaji, muda wa safari, nk.
2. Mkopo-SGR ya Kenya imejengwa kwa mkopo mkubwa wakati ya Tanzania imejengwa kwa asilimia kubwa kwa fedha za ndani. Hii inafanya Kenya waweke bei kubwa na nauli kubwa ya usafiri na usafirishaji ili waweze kufikia lengo la kulipa deni. Nauli na bei juu inawafanya wasafiri na wasafirishaji wasitumie SGR watumie barabara.SGR inakosa mzigo. Tanzania haitalazimika kuweka bei juu kwa sababu haitakuwa na deni kubwa la kulipa. Gharama zikiwa nafuu wasafiri na wasafirishaji watapunguza matumizi ya barabara watahamia SGR.
3. Idadi ya nchi zinazotegemea bandari ya tanzania ni kubwa kuliko Kenya. Tanzania inazungukwa na nchi nane ambazo zinategemea bandari ya Tanzania. Kenya nchi za karibu ziko kama tatu ambazo zina mbadala wa bandari. Hizi nchi zinaangalia unafuu na ubora wa huduma. Sasa vile bandari za Tanzania zinaboreshwa na SGR ya umeme asilimia kubwa ya mizigo ya nchi hizi itapita Tanzania. Hata Uganda mshirika wa karibu na jirani na Kenya, mizigo yake itagawanywa Tanzania na kenya.
4. Uongozi-Tanzania kwa sasa kuna uongozi imara ambao hauna maswala ya nenda uje kesho. Rushwa inapigwa vita sana. Hii itasaidia kuondoa urasimu na ukiritimba kwenye utoaji huduma. Hapa Mizigo ikitoka bandari ni kwenye SGR mpaka nchi husika. SGR itakapokamilika hata Congo itapata mizigo yake bila kupitia nchi nyingine.
5. Ukuaji wa sekta ya viwanda vya ndani-viwanda vya ndani vinakua kwa kasi na kuongezeka Tanzaniana. Hii itaongeza mzigo wa kulisha SGR , Kenya ambayo uchumi wake unasimamia uwekezaji. Inachoangamoto ya wawekezaji kufunga uzalishaji na kuhamia maeneo mengine. Hapa mzigo unaweza kupungua.
6. Malighafi- Tanzania ina mashamba makubwa ya kuzalisha malighafi za kuja kutumika viwandani. Na reli ya mkoloni ilijengwa hasa si kutoa mizigo bandalini kwenda mikoani bali ilikuwa inalenga kutoa malighafi mashambani kwenda bandarini. Mazao karibunyote makuu Tanzania uzalishaji umeongezeka. Hivyo tutashuhudia SGR Ikienda na kurudi na mzigo hii italeta faida. Wakati Kenya uzalishaji wa malighafi na mazao uko chini hivyo SGR inaweza beba mzigo one way kutoka mombasa na mabehewa yakarudi mombasa tupu.
7. Mifugo- Kuna wakati niliishi shinyanga pale, mbali na mafuta na pamba kuchukua mabehewa mengi lakini pia niliona wasukuma walivyokuwa wakigombania mabehewa kusafirisha ng'ombe kuja Dar ea salaam. Sasa Tanzania ina machinjio mbili za kimataifa. Mifugo itachukua sehemu kubwa ya mzigo kuja pwani.
8. Idadi ya watu-Tanzania ina idadi kubwa ya watu , na wanapapenda kwao. Maendeleo hayako Dar na dodoma tu. SGR itarahisisha usafiri na tiketi zitakuwa zinakuwa full booked. Wakati wakenya wanapambana kubaki nairobi. Volume kubwa ya safari iko december tu wakienda kuona maji mombasa. Tanzania december watu wako station wanatafuta usafiri wa kwenda mikoani kwao na wilayani kwao wakale sikukuu . Kwa hiyo mgawanyo wa safari utarahisisha SGR ya Tanzania kutemgeneza mapato.
Wakenya niendeleee.....
Wewe ukizama shimoni, sisi tunaokuja nyuma shimo tunaliona lazima tulikwepe. Na hapo ndipo anayeanza huwa anaachwa njiani!