Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hapa ni malimbe,sehemu inaitwa nyamalango,kwa mbele kuna migahawa ambayo wanafunzi wa SAUT na wakazi wa eneo hili hujipatia chakula chao pamoja na mahitaji mengine
Uchafu huu huachwa hovyo hovyo pasipo kuchukuliwa kwa hatua husika na hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi na wakazi wa eneo hili
Na serikali ya mtaa wa silivini inafahamu uwepo wa jambo hili hivyo wanapaswa kuchukua hatua stahiki mapema kwani eneo hili pia inapatikana shule ya msingi nyamalango ambapo watoto wenye mahitaji maalumu pia wana darasa lao katika shule hii na hutumia njia hii kwenda na kutoka shuleni.