DOKEZO Uchafu umezagaa Mitaa mingi ya Manispaa ya Mpanda, wahusika hamuoni? Mvua zikianza itakuwaje?

DOKEZO Uchafu umezagaa Mitaa mingi ya Manispaa ya Mpanda, wahusika hamuoni? Mvua zikianza itakuwaje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245

Nimeona kampeni ya usafi ikifanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi lakini najiuliza kampeni hiyo ina maana gani ikiwa uchafu kwa wingi unazagaa katika mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo.

Oktoba 19 2026 nikiwa Mtaa wa Madukani, Buzogwe na Makanyagio nimekutana na uchafu mwingi umetelekezwa barabarani na hakuna gari la kubeba uchafu linalopita mara kwa mara kubeba uchafu huo na kusababisha kero kubwa ya mazingira kuwa machafu.

Katika Mtaa wa Nsemlwa kwa Muunga Mitupa kule ni kwa miaka zaidi ya minne hakuna gari la kuzoa uchafu iliyowahi kupita kubeba uchafu.

Naiomba mamlaka husika akiwemo mkurugenzi kushughurikia kero hiyo kwa haraka kabla ya mvua ya el mino haijaanza kunyesha Mpanda na kusababisha mlipuko wa magonjwa.
 
Nimeona mjusi tu ,sijaona uchafu wowote. Hongera Sana Manispaa ya Mpanda.Endeleza juhudi zenu maana wakubwa zenu sio mfano mzuri wa kujifunzia mambo ya usafi.
 
Back
Top Bottom