google helper
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 9,623
- 13,759
Uchafu ni maudhui, matendo au mata inayopatikana mahali pasipotakiwa kwa wakati usiotakiwa.
Hatuwezi kutenganisha maendeleo na usafi au mpangilio wa kila kitu, kila siku katika mambo yote yanayotuzunguka.
Uchafu katika nchi yetu sio jambo geni kabisa maana uchafu upo kila mahala. Uchafu huo ni uchafu wa Mazingira, uchafu wa kimwili na uchafu wa kiroho.
Uchafu wa mazingira.
Hili ni eneo muhimu sana katika uzalishaji maana shughuli zote za mwanadamu zinategemea mazingira rafiki kwa kilimo, makazi, viwanda nk. Lakini ajabu sana tumejisahau kabisa maana mazingira yetu yanatisha kabisa. Mazingira yetu tunayaharibu sisi wenyewe alafu tunaanza kutupiana mpira wa lawama sisi kwa sisi pamoja na serikali.
Wote ni mashahidi sio mara moja unakuta mtu, amebeba fuko la uchafu katoa kwake anakuja kutupa kwenye mifereji ya maji barabarani. Taulo za kike, chupi za mkojo za watoto ( pampasi) fuko zima limetawanyika pembezoni mwa barabara bila aibu tunaruka haoo na safari zetu. Kila mtu ni mbabe kwa mwenzake, mara kadhaa nimewahi tembea na marafiki huku tunatafuna miwa, kwa kiasi mimi ni muoga kutupa tupa taka hovyo ila utasikia wee acha uoga mara fuuuu kifuko cha uchafu mtaroni au kando kando ya barabara.
Eneo lingine ni katika ujenzi na mipangilio ya miji na majiji yetu, yote imekaa kama bomu tayari kulipuka. Kwa mwendo huu hakuna maendeleo wala hatua tutakayopiga. Katika eneo hili kila mtu anajua vituko, visa na mikasa yake, kesi ni nyingi huko wizara ya Ardhi, nyumba na makazi.
Mara huyu kajenga kwenye eneo la barabara, huyu kajenga kwenye chanzo cha maji, mara kiwanda hiki kinamwaga uchafu wake kwenye makazi ya watu, kwenye vyanzo vya maji nk.
Yote hayo ni sababu ya mipango mibovu, rushwa na kutokuwajibika kila mtu katika nafasi yake. Watanzania hatuna kabisa hamasa ya usafi hata chembe, ila ni wepesi sana kulalama pindi mvua ikinyesha alafu mafuriko na uchafu mpaka manyumbani mwetu, hapo serikali italaumiwa sana. Wakati huo huo sisi wenyewe tunazibua vyoo vyetu na kutuma tuma uchafu na taka kwenye mifereji, barabarani nk.
Wapo wengine wanajiona wajanja sana ni kama wanakomoa serikali na wenzao. Mtu mzima kabisa ni baba anayeongoza familia yake, mama kabisa mwenye watoto na dada wa kazi ndani ila asubuhi anabeba furushi la uchafu zigo zigo kweli anapanda nalo daladala alafu analitelekeza huko huko anashuka yeye anawaachia dereva na konda zigo la chupi za mkojo za mtoto wake nk.
Sasa kwa mwendo huu hayo maendeleo yanatokea wapi, kwa mwendo huu huo uvumbuzi wa tehama unatoka wapi kama mazingira yetu tu yanatushinda? Kilimo katika mazingira machafu hivi nini kitafanyika ? Viwanda na uzalishaji utapigaje hatua ?
Uchafu wa mwili na roho
Kama ni sherehe basi hapa ndio pazito kabisa, hapa panabeba yote maudhui mitandaoni, usafi wa mtu mmoja mmoja wa mwili wake, maneno machafu na huduma mbovu kabisa. Kama tumelogwa basi hirizi imepotea na mganga kafa maana haijulikani kabisa mstakabali wa kizazi kijacho vile kitakuwa maana uchafu umeshamiri kabisa, nchi imekosa maadili watu wanajianika uchi mitandaoni, hakuna ukosoaji wenye mwelekeo wa kujenga ila matusi matusi huku watu wakiunga mkono, vijana wadogoo wanafanya uchafu kuzidi wa sodoma na gomora. Watu tuko kasi sana na majibu ni mepesi sana tumejizima data.
Wale vijana wanaotegemewa kutumia mitandao kuleta ubunifu na mabadiliko chanya katika kilimo, biashara na kujiajiri ndio hao wanauza uchi kwa wingi wao telegram, instagram, tiktok nk. Hakuna hata chembe ya hofu kabisaa. Ajabu hata maeneo ya kazi ni uchafu uliopindukia, visa vingi tu mara huyu daktari kalala na mgonjwa hospitali, huyu mfanyakazi ofisini wanashikana shikana sasa uwajibikaji utatoka wapi watu wanalalana ? Nani atamwajibisha mwenzake kama wanachezeana ofisini. ?
Mwalimu analawiti wanafunzi, mwalimu anabaka wanafunzi sasa nani atakuwa mlinzi wa mwenzake? Kila mahala ni uchafu uliopindukia. Wanaojiita wachungaji, mashehe na viongozi wa kidini tena bila kuogopa vile wanavyopewa heshima katika jamii bado wanazini na wanafunzi, wanalawiti, wanaleta migogoro sana wakati wanategemewa kuwa faraja na makimbilio kwa wale wanaofanyiwa unyama na ukatili pamoja na uchafu usiomithilika.
Mambo ni mengi na ushahidi uko wazi kabisa katika jamii yetu.
Sasa nini kifanyike ?
Kwanza lazima tukubaliane hapa woote hapa tuna makosa kuanzia Serikali toka juu mpaka mwananchi mmoja mmoja . kona zote zinawajibika ili tusimame sawa sawa kwa pamoja na kweka shabaha kulenga maendeleo tu.
Uwajibikaji kwa serikali
Hapa serikali inayo wajibu moja kwa moja kuweka mambo sawa katika kupanga mambo kisasa, hapa wataalamu wahusishwe kikamilifu, mipango miji, miradi iwe ya muda mrefu zile mambo za jenga alafu baada ya miaka miwili mradi unabomolewa kupisha mradi mwingine ni kuongeza uchafu tu mjini wa vitu visivyokuwa na tija. Wazembe pia wawajibishwe kisawa sawa sio mpaka wananchi waanze minong'ono mitandaoni.
Serikali ina vyombo vingi katika kujikagua na kuwajibishana, siasa isitumike vibaya ili kuwawajibisha wale tu au yale tu ambayo wananchi wameona ila kila uchafu na uozo uwajibishwe. Wako watendaji wachafu kiutendaji na kimaadili huko kwenye ofisi za umma, wapo wakufunzi wachafu katika vyuo, wapo katika kila idara waliooza kabisa lakini wanaogopana na kulindana.
Sera, sheria na kanuni nyingi nzuri zipo kuwawajibisha wote wazembe na wachafu hivyo zifuatwe, serikali ikubali pia kukosolewa na kupokea ushauri wenye tija toka kwa taasisi nyingine, wanasiasa, wana mitandao na hata kwa mtu mmoja mmoja toka ngazi zote.
Uwajibikaji kwa viongozi wa dini
Viongozi wa dini nao wanaowajibu wa kuwafundisha waumini wao maadili sahihi, wanao wajibu pia wa kuwawajibisha viongozi wao wanapofanya uchafu na uozo wa namna yeyote ile. Watoe ushirikiano wa kwa polisi, kipelelezi na mahakamani pale kiongozi wao, au mtendaji wao anapofanya uchafu wowote kwa yeyote yule.
Kuacha mafundisho ya utajiri wa kuombewa, kupaka maji na mafuta lakini wawahimize vijana kuchapa kazi kwa maslahi mapana ya nchi kwa ujumla.
Kutoa semina elekezi kwa vijana na watoto kuhusu Afya ya akili, miili yao, kujipenda, kujitunza, kujisitiri, na kutunza mazingira yanayowazunguka. Kwa vile dini zote zinasisitiza usafi katika ibada basi watoe elimu elekezi wa usafi katika mazingira yote kwa ujumla, watu waone aibu kutupa taka taka kila mahala kama vichaa, watu waone aibu kujianika uchi mitandaoni.
Viongozi hawa wa dini zile zenye miradi basi watoe misaada kwa waumini kama ni mikopo, elimu ya biashara, elimu ya uongozi na kutoa usimamizi na mwelekeo kwa vijana sio muda wooote wao wanahimiza watu wanunue maji, keki, mafuta nk.
Uwajibikaji wa taasisi na mashirika mengine.
Taasisi zisizo za kiserikali zinawajibu pia wa kushirikiana, kukosoa, kushauri na kupendekeza njia nzuri zitakazoisaidia jamii kupiga hatua katika maendeleo ya ujumla, ziko taasisi nyingi zinazohusu mazingira, hizi zitoe ushauri namna nzuri ya kukabiliana na uchafu wa mazingira. Taasisi za haki za binadamu nazo zitoe ushauri na kuunganisha nguvu pamoja kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaoididimiza jamii. Kila sekta, kila kona kuanzia kwenye ngazi ya familia mpaka wafungwa magerezani ili kukomboa nguvu kazi inayopotea kwa kasi sana.
uwajibikaji kwa wazazi na walezi
Pamoja na ugumu wa maisha, lakini wazazi na walezi wana wajibu wa kuitunza familia katika maadili sahihi, kazi hii ya matunzo isiachwe kwa wadada wakazi, walinzi na madereva wa familia au boda boda wa mama au baba. Wengi wamenajisiwa watoto wao toka utotoni kwa kuacha wajibu wao kwa kisingizio cha utafutaji.
Tutengeneze urafiki, hali na motisha kwa watoto wetu ndugu au wale tunaoishi nao ili wakue na mawazo chanya. Wafundishe usafi lakini pia ishi kwa usafi ili waige kutoka kwako. Usiwaachie wengine walee watoto wako wakati wewe upo , kagua hatua za makuzi yao, changamoto na kujua shida au vipaji walivyonavyo ili uwasaidie. Wazazi au walezi wenye uwezo, watoto wanakuwa na simu, runinga au kuifikia mitandao ya kijamii basi wawafundishe kwa uwazi kwamba yapo mema na mabaya ndani yake. Hii itamjengea mtoto uwezo wa kuyakataa mwenyewe hata kukiwa na ushawishi kwa wenzie.
N.B
Pale serikali inapotumia wahamasishaji katika jambo, basi watumie watu sahihi, wasitumie watu wenye upeo mdogo waliojipatia umaarufu kwa sababu ya umaarufu wa hovyo walijijengea katika mitandao ya kijamii kuleta hamasa maana inaonekana kama maigizo na dhihaka na kebehi mbele ya jamii.
Asanteni sana, karibuni kwa michango, kura yako na kukosoa pia ili tuijenge jamii iliyostaarabika.

Upvote
0