The Legacy
JF-Expert Member
- Jun 1, 2022
- 5,879
- 11,318
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuhusu hali ya usafi na utunzwaji wa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Nimejaribu kupitia nadharia mbalimbali na uzoefu niliokuwa nao kwenda viwanjani mara kwa mara nikagundua kuwa uchafu ule ni zao la mfumo au taratibu tulizojiwekea kama Taifa.
1. Uchafu ni Nini?
Uchafu kwa lugha nyepesi ni kitu chochote kilichokaaa mahali ambapo sio pale. Mfano kuweka kopo la chooni chumbani. Mahali popote binadam anapokuwepo kunatokea uzalishwaji wa taka ngumu au taka laini zinaweza kuwa taka mwili nk.
2. Mfumo
Ni taratibu zilizowekwa na mamlaka au kikundi cha watu flani, mfano mfumo au utaratibu wa kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa (Lupaso). Mfumo huu unaruhusu watu kuingia uwanjani kwa muda mrefu na kukaa pale kiwanjani bila sababu. Hivyo matumizi ya binadam kwa kinywaji na chakula hupelekea uzalishwaji mkubwa wa taka mwili. Taka ambazo zinatakiwa kutolewa au kitupwa pale uwanjani.
Sababu ya kukaa muda mrefu kiwanjani hutokana na uwepo wa mfumo mbovu wa uingiaji kiwanjani kupitia mageti machache. Hivyo watu wengine hulazimika kuingia mapema ili kuepuka msongamano. Watu hawa wanapokaa ndani hukaa kwa muda wa masaa zaidi ya matano ndani ya uwanja.
Mathalani mechi ni sa 11 geti linafunguliwa saa 7 mchana. Uwepo wa ninadam huyu ndani wa uwanja lazima utazalisha taka na uharibufu mwingine kwa uwanja. Hivyo hupelekea uwezo wa uwanja kuzidiwa. Hata pale usafi unapofanyika unashindwa kurudishwa kwenye hali ile ya mwanzoni.
3. Mfumo Binafsi wa Maisha
Inawezekana kabisa usitumie choo cha uwanja kama ukiamua. Binafsi nilifundishwa na mama yangu mzazi (Mungu ampuzishe salama) kutotumia choo tofauti na cha nyumbani kwa haja kubwa kwa mfumo wa kuhakikisha ninaratiba kamili ya kula na haja kubwa asubuhi na usiku. Hivyo nilimaliza shule ya msingi pasipokutumia choo kwa haja kubwa.
Hii inanipa faida hata choo cha kazini, huwa natumia kwa haja ndogo tuu.
Nashauri mfumo wa uingiaji uwanjani uwe wa haraka ili kupunguza uwepo wa watu wengi kwa muda mrefu pale Lupaso. Hii itafanya mageti yafunguliwe masaa machache kabla ya mechi na watazamaji kutumia muda mchake kuingia na kukaa kiwanjani.
Kambona Jr.