Uchaguzi 2020 ni Uchaguzi wa mtaa kwa mtaa na kitanda kwa kitanda

Uchaguzi 2020 ni Uchaguzi wa mtaa kwa mtaa na kitanda kwa kitanda

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kila mtu Kuna vile anavyotaka awe navyo chumbani kwake, nyumbani kwake, na mtaani kwake anakoishi ambavyo vinategemea na Ni chama na kiongozi gani anayeongoza Mtaa, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Watu safari hii hawatapiga kura za jumla jumla Kama zamani Bali watajipigia kura wao wenyewe kutokana na Hali ilivyo kwenye chumba chake anamolala na kwenye mtaa, kata, tarafa, wilaya, nk.

Je, ni nani hakufanya Nini au atafanya Nini kwenye mtaa, Kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na Tanzania Kama nikimchagua?

Kama wewe uliboresha au utaboresha mtaa ule kule utapata kura za mtaa ule kulee sio huu huku.

Hii ndio maana pamoja na mengi yaliyofanywa na CCM kwa miaka 60 lakini bado vyama vya upinzani vipo na wafuasi wengi tu. maana yake yako mambo ya watu binafsi, familia, mtaa, kata, tarafa, wilaya,.... Wanakoishi hayakupewa kipaumbele na wabunge wao au chama.
 
Juzi nimekaa na mwana CCM mmoja anasema huu ndio wakati wa kuneemeka manake ukimaliza uchaguzi hela itatoweka. Nikajiuliza huyu hana cheti cha mirembe lakini? Sasa kwanini usichague wapinzani pengine wataleta hela miaka 5 yote. Kwanini ubaki na ccm wenye kuleta hela kwa msimu wa uchaguzi tu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
mtaa gani ulioboreshwa na upinzani kwa mfano?
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa,.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Kama mkoloni angefanya hivyo hata Nyerere angeuawa, tusingemkuta.
 
Back
Top Bottom