Uchaguzi 2025 itakuwa ni CCM na kivuli cha Hayati Magufuli

Uchaguzi 2025 itakuwa ni CCM na kivuli cha Hayati Magufuli

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Kama lipo eneo Magufuli aliwa-win wabongo ni kuwaaminisha kwanza Tanzania ni Nchi tajiri huko akitolea mifano akiba ya rasilimali tulizonazo na zaidi akiwaachia uhuru usiyo na mipaka walalahoi kufanya lolote lile wanalotaka huku akitoa amri ya wasifanywe lolote. Rejea machinga.

Sasa,kwa yanayoendelea Tanzania kwa sasa iwe kwa nia nzuri ama vinginevyo hakika madhara yake kisiasa yatarajiwayo 2025 ni ya kutisha!

Mfanyasiasa yeyote atakayekuja na slogan ya KWANINI KIPINDI CHA UTAWALA WA MAGUFULI HATUKUFANYIWA HIVI kwa hakika atali-win pakubwa kundi la walio wengi hasa wafurukutwa wa Hayati Magufuli.

Kina Polepole na shule zao za uongozi msifikiri wajinga na msidhani yupo peke yake-analo kundi tena la vigogo hasa na kwa hatua waliyofikia hawa timu JPM kupitia Polepole ni ngumu mno kuwadhibiti tena.

Tuombe uzima lakini 2025 ni pagumu mno kwa CCM kwa maana washindani wake watakuwa wawili kwa maana ya vyama hivi vya upinzani tulivyonavyo na waamini watakatifu wa Magufuli.

2025 ni hatari!
 
Miaka 4 from now ni mbali sana, endelea kuyaishi hayo maumivu huku ukisubiria kama fisi! Siku huyo Polepole akiturn 180 degrees baada ya kurushiwa fupa usije kumtukana hapa
 
Miaka 4 from now ni mbali sana, endelea kuyaishi hayo maumivu huku ukisubiria kama fisi! Siku huyo Polepole akiturn 180 degrees baada ya kurushiwa fupa usije kumtukana hapa
Polepole na timu yake hawana cha kupoteza
 
Kama lipo eneo Magufuli aliwa-win wabongo ni kuwaaminisha kwanza Tanzania ni Nchi tajiri huko akitolea mifano akiba ya rasilimali tulizonazo na zaidi akiwaachia uhuru usiyo na mipaka walalahoi kufanya lolote lile wanalotaka huku akitoa amri ya wasifanywe lolote...
Haujui CCM vizuri kijana.. waulize nccr ya Mrema, CUF Lipumba na chadema ya Mbowe. Mwaka 95 wakati hayati Mkapa anapitishwa kugombea uraisi kupitia mgongo wa mw Nyerere kuna kundi la machekibob ambalo lilikuwa na nguvu kubwa ndan ya chama hicho.

Kundi hili lilipoona Mkapa amepitishwa dhidi ya Kikwete lilitishia kujitoa ndani ya chama, hali iliyopelekea ndugu Mrema na genge lake wawe na uhakika wa kushinda uchaguzi ule maana waliamini CCM bila vijana hao machekibob au boyz 2 men ni sawa na debe tupu. Cha kushangaza zilipofika kampeni wote waliungana na mgombea wa CCM (Mkapa) dhidi ya Mrema na chama chake, na matokeo yake CCM ikashinda uchaguzi.

Mwaka 2015, chadema na genge lao waliamini kwamba CCM ingemfia mikononi aliekuwa raisi na mwenyekiti wa chama hicho, bingwa wa siasa na mbinu za kimkakati wa aina zote mh J. Kikwete. Chadema Wakakaa mkao wa kula na kuanza kupanga kabisa baraza lao la mawaziri. Wakati wao wakipanga hivyo, mwenzao mzee Msoga akapanga mbinu yake ya kusimamisha wagombea wawili wa CCM katika vyama tofauti.

Kweli baada ya mpango kusukwa na mambo kwenda kama yalivyotakiwa kwenda, likaanzishwa zengwe kusudi dhidi ya mwenye mkakati mmoja. Na yeye bila kuchelewa akatumia mbinu alizopewa na mwenyekiti wake kukimbilia upande wa pili Chadema ili akakamilishe ile kazi ya mwenyekiti kusimamisha wagombea wawili wa CCM katika vyama viwili tofauti.

Baada ya hapo kila mtu anajua kilichoendelea na jinsi gani CCM ilifanikiwa kuusambaratisha upinzani na baadae waliopewa mikakati wakarudi CCM walipotoka na kuendelea kuwa kitu moja. So mleta mada unatakiwa ujifunze kwanza historia ya chama husika kabla haujakurupuka kuandika vitu ambavyo kiuhalisia haviwezekani.
 
Back
Top Bottom