Uchaguzi 2020 Uchaguzi Bukoba Vijijini Wagubikwa na rushwa, Wanne Wadakwa na TAKUKURU, Kura za Lweikiza shakani

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Jana tarehe 21/07/2020, katika harakati za wajumbe kupiga kura Bukoba Vijijini kwa wajumbe waliotia nia Ubunge kupitia CCM, kulitokea utofauti asubuhi ambapo mbunge Rweikiza alituma vijana wake kutoa rushwa na kukamatwa jana ile ile Asubuhi.

Naamini TAKUKURU watalitolea taarifa sakata hili.

====

Katibu wa mbunge wa Bukoba Vijijini aliye kamatwa na PCCB, anadaiwa alikuwa akigawa pesa ndani ya ukumbi wa kura Tsh 50,000 kila Mjumbe na 100,000 kwa makatibu na 200,000 kwa viongozi wao

Viongozi hao wamekamatwa jana na TAKUKURU Bukoba muda mchache kabla ya uchaguzi ndani

Katibu wa Mbunge Mh Jasson Rwankomezi ambaye ni Diwani Kata Kaibanja , Diwani Paschal Bashongere na Mwenyekiti Wa UWT wa Wilaya ambao bado wameshikiliwa na TAKUKURU Bukoba Mjini.

Pamoja na hayo uchaguzi mzima umegubikwa na mizengwe Mingi ikiwemo upigwaji wa kura za wazi badala ya siri kama kanuni inavyosema


Mtuhumiwa akiwa ameficha hela ndani ya kofia. Ziliweza kuonekana kwa Nyuma


Mwingine alikutwa huku akigawa mshiko
 
Mbona picha ya Kwanza sio mazingira na udongo wa bukoba?
 
Na wewe kwa nini usingegawa, au ulidhani ubunge unapatikana bure bure, kisa ile laki ya fomu unayo ukajua umeula sio? Mbaya zaidi malalamiko unaleta huku JF badala ya kuyafikisha sehemu husika!!!
 
Hawa TAKUKURU nao ukamataji wao wa rushwa unaohusiana na rushwa za CCM ni wakisanii mtupu, hakuna hata kesi moja ya watoa rushwa na wapokea rushwa wa CCM iliowahi kufanikiwa.
 
Mbona matokeo ya uchaguzi biharamulo kimya Kuna Nini Kama tayali nijuzeni
 
Kesi ya nyani hakimu ni nyani shamba la bwana nyani hapo hakuna hukumu maana wote ni ndugu hao
 
Huwezi kuitenganisha ccm na rushwa ni sawa na uji na mgonjwa,ccm woyee
 


Hata kama sisi wengine hatuungi mkono chama chenu lakini kwenye hili tunapaswa kuwapongeza .

Hongera ccm mpya , hongera awamu ya 5
 
Huu uvhaguzi wa maoni wa ccm kiukweli ulijawa na Rushwa kumbe takukuru ni kwa baadhi ya watu na vikundi vya watu..
 
Kana kwamba mifuko haikutosha kuweka hayo mabulungutu?

Inasaundi gudi walah!
 
Hii picha ni ya mazingira ya nyanda za kati au maeneo mengine lakini siyo Bukoba. Yote kwa yote CCM na rushwa ni ndugu wa baba mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…