figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Jana tarehe 21/07/2020, katika harakati za wajumbe kupiga kura Bukoba Vijijini kwa wajumbe waliotia nia Ubunge kupitia CCM, kulitokea utofauti asubuhi ambapo mbunge Rweikiza alituma vijana wake kutoa rushwa na kukamatwa jana ile ile Asubuhi.
Naamini TAKUKURU watalitolea taarifa sakata hili.
====
Katibu wa mbunge wa Bukoba Vijijini aliye kamatwa na PCCB, anadaiwa alikuwa akigawa pesa ndani ya ukumbi wa kura Tsh 50,000 kila Mjumbe na 100,000 kwa makatibu na 200,000 kwa viongozi wao
Viongozi hao wamekamatwa jana na TAKUKURU Bukoba muda mchache kabla ya uchaguzi ndani
Katibu wa Mbunge Mh Jasson Rwankomezi ambaye ni Diwani Kata Kaibanja , Diwani Paschal Bashongere na Mwenyekiti Wa UWT wa Wilaya ambao bado wameshikiliwa na TAKUKURU Bukoba Mjini.
Pamoja na hayo uchaguzi mzima umegubikwa na mizengwe Mingi ikiwemo upigwaji wa kura za wazi badala ya siri kama kanuni inavyosema
Mtuhumiwa akiwa ameficha hela ndani ya kofia. Ziliweza kuonekana kwa Nyuma
Mwingine alikutwa huku akigawa mshiko