Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Hizo ndio sera za tinga tinga.....akapumzike miaka 19 mjengoni hakuna alichofanya......hivi hawa wazee ni mpaka wafie mjengoni?

kILA MTU ANAJUA KUWA AMECHOKA IMEBAKI YEYE TU KUACHIA NGAZI. du asije akasikia jamaa akasema nimetumwa na nchimbi!
 
Naona so called wapinzani wamegundua sera mpya ya kuzomea baada ya zile za awali za kufyatua mabomu mwembe yanga, kurusha mawe mbeya kushindwa kufanya kazi.

Keep it up...
 
Hzo picha jamani hazipo kama umeziona si zipachike zionekane acheni utani kwenye vitu vya msingi
 
Hzo picha jamani hazipo kama umeziona si zipachike zionekane acheni utani kwenye vitu vya msingi

Hebu kuweni serious kidogo inamaana ni kweli hamzioni hizo picture? Du naona na tukio la kuchoma bendera kalikava vizuri, thaks for nice pics
 
CCM wamefanya zengwe lao ndiyo sababu hamzioni. Invisible fanya mavitu yako, watu wan hamu ya kuona kinachoendelea Busanga.
 
Naona so called wapinzani wamegundua sera mpya ya kuzomea baada ya zile za awali za kufyatua mabomu mwembe yanga, kurusha mawe mbeya kushindwa kufanya kazi.

Keep it up...

Lengo la wapinzani ni kupata fursa ya kuongoza serikali na wakifanya jambo lolote la kufanikisha hili lengo shaka hakuna. tatizo linakuja kama wakifanya mambo ambayo ni kinyume na sheria kama mlivyoiba nyie kuiba fedha za umma ili mchaguliwe.....Laana tupu
 
mshahara wa dhambi ni mauti yote hayo ni sababu ya kukumbatia ufisadi. Watanzania wameamka sio wale wa enzi za mwaka 47.CCM someni alama za nyakati.
 
Jamani mkiambiwa Serikali ipo mbioni ,inatakiwa mufahamu kuwa inakimbia majukumu yake na haitaweza kuyatekeleza ndio maana yake kila unapowasikia utasikia wapo mbioni sijui wanakimbia nini ?
 
Kumbe Ngeleja alikuwa na mipango ya muda mrefu na Dowans, mbona hakuliambia bunge?

Makubwa haya kumbe jenereta uamuzi ulishapita kuzinunua.

Hivi haya majenereta ya Downs si yalinunuliwa kwa ajili ya emergency cases. Sasa leo inakuwaje leo wanasema wameshindwa kuwepelekea wananchi umeme kwa sababu ya Downs?? Hivi huu umeme wa Downs wa 200 MW ni asilimia ngapi ya umeme tunaozalisha. Kweli wadanganyka kwa porojo nimekoma..........!!!!

Sasa kwa nini alishindwa kuwambia mpango unaofuta baada ya Downs kupigwa chini???????????
 
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. CCM wanandhani watanzania ni wale wale kudanganywa peremende siku zote, haya........
 
je wananchi wa DAR wamechoka na wanaweza kuzomea kama busanda?
katika miji mikuu DAR ni masikitiko
miji mikuu ndio vuguvugu za kisiasa zinakuwa kubwaaa
yani watu wa busanda wana muako kuliko dar????????
kweli dar tambarare...
 
Wakuu samahanini sana niliziweka kumbe kutokana na matatizo ya kimtandao huku zikawa hazijatokea nimemtumia invisible na Mwanakijiji ili waziweke na nyingine nitaweka usiku pamoja na maelezo ya kina .

Mkiziona picha ya kwanza ni ya gari la polisi ambalo lilienda kumchukua diwani aliyekamatwa na kikosi cha CHADEMA jana saa saba usiku akiwa ananunua shahada kwenye kata ya busanda, ya pili ni diwani aliyekakamatwa na ya tatu ni balozi mmoja wapo aliyekamatwa akiwa ananunua shahada na alikutwa na shahada 17 za wananchi na alipohojiwa alisema kuwa wameagizwa na ngazi za juu.

Wameshikiliwa na sasa wametolewa kwa dhamana ila watafikishwa mahakamani.

Nyingine ni za mkutano wa Zitto kata ya Katoro juzi .

Mengine baadae kwanni huku umeme shida na jenereta wanawasha usiku tuu hivyo ni hadi usiku tena.
 
Picha zinaonekana , mbili tu, lakini mimi nisichoelewa, zina uhusiano gani na Zitto?
Kwanza
 
picha ya mwisho ni kama fid q huyo aliyezibwa na zitto, au macho yangu?
 
hizi kampeni hizi, wananchi watalishwa kila aina na maneno. Sasa ngeleja anataka tuamini kuwa Dowans ilikuwa inataka kununuliwa kwa ajili ya busanda!!!
 
Jamani kama kweli hao watapiga kura basi nahesabu CCM chaliiiiiiiiiiiii dah CHADEMA wamekula vichwa balaaa kitu nyomi kha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…