Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Sasa arsenal wanahusiana nini na huu mjadala?

Acheni upuuzi huu mnaotaka kuuleta

issue hapa ni zitto kumtukana mzee malecela na si arsenal

Game tutajie hilo tusi kwanza, tukilijua tuendelee kulijadili
 
"Huyu Zitto sasa keshaanza kuboa. Sijapendezwa na matusi yake ya reja reja kwa mzee malecela na kama anazo attacks ilitakiwa azielekeze kwenye policies za CCM na siyo Mzee huyu ambaye hakuna alichomkosea

Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu

Mbona yeye mama yake aliiba pesa za walemavu na kukimbia mji na hakuna aliyepanda jukwaani kumwambia kuwa ni mwizi?

Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi"

GT: Matusi yako wapi? Ni lugha ambayo yeye mwenyewe Malecela huitumia sana dhidi ya wapinzani!
 
“Watakuja, kina Dk. Mwakyembe kuwaambia wao wanapambana na mafisadi, lakini hao ni wanafiki, na wao ni mafisadi tu, kwani huwezi kusema unapambana na ufisadi halafu ukiwa ndani ya CCM,” alisema Zitto.

Source: Tanzania Daima 10/05/2009

Hivi Zito ni kwanini vita dhidi ya ufisadi anaiendekezea itikadi?. Nani aliyemuambia kuwa chama cha upinzani kunampa tiketi na hatimiliki ya pekee ya kulaani ufisadi? Hivi alivyotaka TANESCO iinunue DOWANS ndio ulikuwa msimamo wa wapinzani? kama sio, yeye alikuwa anazungumza kwa niaba ya nani?

Haoni kuwa msimamo wake huo ungeifisadi nchi yetu pasi na kikomo? na kwa kiasi kikubwa ufisadi huo aliokuwa akiushabikia ulifanikiwa kusimamishwa na hao hao anawashutumu kukaa kwao CCM hakuna faida dhidi ya vita juu ya ufisadi?

Sijawahi kumsikia Zito akilaani ufisadi wa mtu mmoja mmoja kwa majina; kama alivyofanya mwanzoni Slaa, akifuatiwa na Mwakyembe na hatimaye juzi Mengi. Mara nyingi akiongelea mtu mmoja mmoja atasema huyu ni rafiki yangu...kama anavyonukuliwa akimuongelea JK mara kwa mara, hii sio tu inanionyesha Zito ni mwanasiasa asiyejiamini hasa linapofikia suala la kupambana na wanasiasa (wezi) wenye ushawishi kwenye mpambano wa mmoja mmoja (off course ukimuondoa Mwakyembe) ambaye anahatarisha umaarufu binafsi wa Zito; bali pia linaonyesha, ukuta pekee anaoweza kujifichia kurushia shutuma zake ni kwa kukiweka CCM katika kundi, bila ya kuonyesha uovu wa mtu mmoja mmoja.

Sina hakika na wanachama wengine wa JF wanafikiria nini juu ya mwanasiasa huyu. Lakini binafsi, kwa mtiririko wa kauli na vitendo vyake, nashawishika kuamini kuwa ni mtu wa kujali sana umaarufu wake binafsi bila ya kuangalia maslahi ya umma mpana anaodai kuuwakilisha.

Ushauri wangu kwake ni muhimu kwake na wengine kuunga mkono wale wote wanaoonyesha umma kuwa wanauchukia ufisadi, na hili bila kuangalia wanapiga kelele hizo kutokea ama CCM au nje ya CCM, Kwani kelele zao zinatusaidia sana wazalendo wengine hata kama zinafunika umaarufu wa mtu mmoja mmoja kwenye upinzani kama wa kina Zito.

Ni muhimu kwa Zito kuwaunga mkono majemadari na Watanzania wote bila ubaguzi kwenye vita dhidi ya ufisadi bila kujali kwa kufanya hivyo watakuwa wengi wanaopiga vita dhidi ya suala moja, na yeye hana hatimiliki ya kupinga maovu na hakuna mwenye hatimiliki.
 
NAIBU Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto amesema tingatinga? la Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Bw. John Malecela limeshindwa kupanda jukwaani kwa kuwa limegeuka bajaj? kwa kuanza mikutano ya mafichoni.

"CCM hawana ubavu wa kupambana na CHADEMA, hata wabunge wao wanaojidai wanapambana na ufisadi ni waongo wakubwa?. Kama wanataka kupambana na ufisadi waondoke CCM kwa sababu hawawezi kupambana na ufisadi wakiwa ndani ya CCM," alidai Bw. Zitto.
Alisema CCM imekuwa na mazoea ya kumtuma Bw. Malecela kwenye uchaguzi unaokuwa na upinzani mkubwa na ndio maana akaletwa hapa kama tingatinga lakini amejikuta akikwama kupanda jukwaani.
 
Hivi hapa kuna tusi jamani au mcho yangu? Then kama kuna tusi basi hili neno tusi limeanza kupoteza maana. This is politics kama mtu anajiita tingatinga wewe ukamwita kibajaji hilo si tusi asilani. Unless hilo tusi unalirefer kwenye neno jingine mkulu. Hayo mengine mama yake kuiba sidhani kama yanaingia hapa kuna namna nyingine ya kuyafuatilia lakini kuyaweka kwenye hili ni kumwonea tu mheshimiwa. Anyway this is just my opinion as far my interpretation of golden rule is concerned.
 
Hakuna tusi hapo mkuu. Unawaka bure tu, katika medani za siasa vijembe,kejeli na misemo vina nafasi yake kubwa sana. jaribu kupanua wigo wako wa kusoma makala na matukio ya kisiasa.
Kwa mtazamo wangu japo sijui umri wako wewe ndio umekosa adabu kwa mama yake Mh Zitto,
In politics always expect anything from the rivl camps
 
Hakuna tusi hapo mkuu. Unawaka bure tu, katika medani za siasa vijembe,kejeli na misemo vina nafasi yake kubwa sana. jaribu kupanua wigo wako wa kusoma makala na matukio ya kisiasa.
Kwa mtazamo wangu japo sijui umri wako wewe ndio umekosa adabu kwa mama yake Mh Zitto,
In politics always expect anything from the rival camps
 
- Zitto a.k.a Dowans ameibukia wapi tena? Vipi uwaziri wa nje kwenye serikali ya Masha? Chadema mmekula chuya na hawa viongozi mufilisi, nani wa kuliokoa taifa hili?

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES!
 
Msome vizuri mweshimiwa pasipokuwa na itikadi kichwani kwako utamwelewa ukitaka. Wakati sisemi kwamba kwenye upinzani hakuna upinzani lakini ni kweli ulio wazi kwamba sisiem ni vitara wa ufisadi. Mtanzania yeyote mwenye akili ya kawaida tena mwanasisiem damu atakubaliana na hilo pasi kupinga. Pont ya zito ni kwamba ngumu kupandana na ufisadi ukiwa ndani ya sisiem kwani the whole system is corrupt. Wote tunakumbuka namna ambavyo wazee wa chama kama kingunge walivyo kinyume sana na wabunge wa sisiem wanaopambana na ufisadi. So hii ni ngumu sana hasa kwa wabunge wa sisiem kwani ni sawa na kusema swala anao uwezo wa kumkoromea simba. Nikumbushe hotuba moja ya mwenyekiti wa sisiem ambayo alikemea vikali ufusadi kwa dhati kabisa.
 
Adaiwa kukwama kupanda jukwaani
.CCM yafanya mikutano mafichoni

Reuben Kagaruki na Faida Muyomba, Busanda

NAIBU Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto amesema tingatinga la Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Bw. John Malecela limeshindwa kupanda jukwaani kwa kuwa limegeuka bajaj kwa kuanza mikutano ya mafichoni.


"CCM hawana ubavu wa kupambana na CHADEMA, hata wabunge wao wanaojidai wanapambana na ufisadi ni waongo wakubwa. Kama wanataka kupambana na ufisadi waondoke CCM kwa sababu hawawezi kupambana na ufisadi wakiwa ndani ya CCM," alidai Bw. Zitto.

Alisema CCM imekuwa na mazoea ya kumtuma Bw. Malecela kwenye uchaguzi unaokuwa na upinzani mkubwa na ndio maana akaletwa hapa kama tingatinga lakini amejikuta akikwama kupanda jukwaani.

Bw. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alidai moto wa CHADEMA jimboni hapa Bw. Malecela hauwezi kwa kuwa ni bajaj iliyochoka na ndio maana imeamua kufanya mikutano ya mafichoni na wanachama yenye lengo la kuiba kura.

Katibu huyo ambaye alikuwa akishangiliwa muda wote alisema hata kama CCM watapeleka viongozi wao maarufu wakiwemo wabunge kama akina Dkt. Harrison Mwakyembe na Bi. Anne Kilango jimboni hapa lakini akatamba kuwa ngoma
hawaiwezi kwa kuwa ni nzito.



Source: Majira, Sunday, 10 May 2009

- Zitto ni bingwa kupigana na ufisadi? mpaka ana ubavu wa ku-question wabunge wengne? Haya makubwa sana madogo yana nafuu!

- Sasa analalamikia mbinu za uchaguzi za CCM badala ya kujali za chama chake? Tayari ameshaanza kilio cha kuibiwa kura?

- Sio yeye aliyesema anam-support Mwakyembe katika vile vita vyake na Rostam? Sasa leo hakuna vita vya ufisadi ndani ya CCM, lakini anakubali kwamba hawa wabunge ni maarufu?

- Zitto, sasa ukiwa mshiriki wa Dowans ya Rostam utasaidia vipi wananchi wa Busanda? Utawaletea hela kidogo ulizochotewa na Dowans aka Rostam/Lowassa/Mkamba/Manji?

Respect.

FMES!
 
si hivyo tuuu mbona mama yake ZITTO ambaye ni mlemavu aliiiba pesa za walemavu na kukimbilia Mwanza hakuna anayemtukana au basi tuu anataka umaarufu kupitia mgongo wa mzee malecela?

au pesa za MENGI zinamlewesha?
 
Nilitaka niachane nawe lakini ngoja nikujibu tu!

1. Kama RA ashikilii ccm kwa nini mnashindwa kumface na kumtimua kwenye chama chenu. Mtu mabaye image yake imeharibika hivyo hata kama anaonewa ni better ajkae pembeni lakini mmeshindwa kumtoa na anaendelea kukizamisha chama chenu. Sasa hhvi ili mptate ushindi ni lazima muibe tu na ndipo hapo umuhimu wake unapoonekana. Chama chenu tunajua kisipomtaka mtu huwa kinamwambia live, kumbuka John malecela alivyokemewa na mkapa kuwa aache kulilia kama ajakubaliana na matokea ahame chama. Unaona msipo mtaka mtu mnavyofanya kwa hiyo wewe bwabwaja tu lakini bado RA ni muhimu sana kwa chama chako.

2. Kutolewa uweka hazina hii nayo nimoja ya vioja unavyovirudia rudia humu mara kwa mara. Kwanza unataka kuonesha kuwa unamjua Jk mpaka rohoni kwa kusema kuwa amemtema uweka hazina RA kwa sababu unajuaje kama hawakukubaliana mapema kuwa atoke? hebu ona hili, hawa jamaa mwaka 2005 waliiba fedha za umma, na walijua kuwa wameiba fedha za umma inawezekana siku moja waka gundulika na wakigundulika wasipoteze image yao. nini wafanye ni kumtoa ni kumtoa mshiriki kwenye nafasi amabayo soo likigundulika haliwezi kukiweka chama chenu kwenye nafasi mbaya. Kwa hiyo RA alichagua yeye mwenyewe kutoka na ndiyo maana aliyebadili anachukua order kutoka kwake. Au unataka kusema kuwa mmeleta mtun mpya kwenye hiyo post?

3. Hii ya takukuru wewe subiri tu kwa nini unataka kuwahi hivyo? njisi alivyopokelewa tu inaonesha njisi mlivyo mpa nguvu kwenye chama chenu na serikali yenu. Kwa sasa kikwazo chake ni sisi wanachi tu kwani nyie (ccm na Serikali) tayari amewakamata pabaya sana, pale!

4. Kuhusu kutumia Jina la Yesu wewe niombee tu kwani nampenda sana na nitaendelea kumweka mbele. Naomba unieleze ila nijirekebishe kuhusu kulitumia vibaya jina lake kwani hiyo ni moja ya mambo ambayo ninakuwa mpole kabisa

5 Mimi sijifanyi chadema ila kwa sasa kura yangu inaelekea huko. Naona unatamani niwe ccm na nimtumikie nchimbi na chama chako. kwani kwa wewe bora ni ushindi kwa chama chako na sio maslai ya taifa. unachotaka hakiwez kutokea ni ndoto tu. ccm haiwezi hata siku moja kujisafisha kwani imeoza.

6. tafuta njia nyingine ya kumbana mwanachama mwenzio nchimbi na sio kupitia kwangu mimi. Mimi sian tatizo na wewe binasfi wala sikujui na siitaji kukujua ila ukileta mawazo yako hapa nakujibu.

7 Namalizia kwa kusema kuwa kama unataka ushindi wa chama chako no=i lazima umpende RA kwani ndiye ushindi wenu

- Irrelevant na haina faida yoyote kwa masilahi ya taifa, Nchimbi sio Chadema!

Respect.

FMES!
 
Huyu Zitto sasa keshaanza kuboa. Sijapendezwa na matusi yake ya reja reja kwa mzee Malecela na kama anazo attacks ilitakiwa azielekeze kwenye policies za CCM na siyo Mzee huyu ambaye hakuna alichomkosea

Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu

Mbona yeye mama yake aliiba pesa za walemavu na kukimbia mji na hakuna aliyepanda jukwaani kumwambia kuwa ni mwizi?

Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi
angekuwepo sophia simba hapa angekwambia, UTAJIJU!!
 
si hivyo tuuu mbona mama yake ZITTO ambaye ni mlemavu aliiiba pesa za walemavu na kukimbilia Mwanza hakuna anayemtukana au basi tuu anataka umaarufu kupitia mgongo wa mzee malecela?

au pesa za MENGI zinamlewesha?
kwa nini umuingize mama yake zitto kumtetea malecela ? na mimi nikimuhusisha mama yako kumtetea zitto utapenda ?
usiende huko GT !
 
unajua sasa vijana washaanza kuwatolea uvivu wazee na hii ndio njia moja inayohitajika katika kulikomboa taifa hili.

suala ni sera mbovu za ccm zikitetewa na watu kama malecela, msekwa, mzee makamba ndizo zinazoturudisha watanzania nyuma. Mbaya zaidi wazee hawa hawa wanadai ni utamaduni, huku nikiita tabia hii kama mazoea mabaya !
 
- Acha vitisho mkuu kwenye siasa matusi kama ya Zitto yanakubalika, GT weka vitu mwanangu!

FMES!
kumjadili kada haitokusaidia chochote, i still stand with my position HAKUNA TUSI LOLOTE LILILOONGELEWA NA ZITTO.

Hakuna yeyote yule anayepaswa kukingiwa kifua ! i mean no ONE!
 
Huyu Zitto sasa keshaanza kuboa. Sijapendezwa na matusi yake ya reja reja kwa mzee Malecela na kama anazo attacks ilitakiwa azielekeze kwenye policies za CCM na siyo Mzee huyu ambaye hakuna alichomkosea

Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu

Mbona yeye mama yake aliiba pesa za walemavu na kukimbia mji na hakuna aliyepanda jukwaani kumwambia kuwa ni mwizi?

Chonde Zitto kama unaanza matusi basi ujue wengine nao wanaweza kukutusi kama unavyowatusi hawa wazee...regardless of their flaws huwezi kupanda jukwaani kumtukana mzee kama yule bila sababu ya msingi
inavyooelekea hali ni ngumu kwa CCM busanda...sioni matusi kwa mzee malecela zaidi ya lugha za katika kampeni...matusi huwa anatoa mzee makamba bwana ngoja muda si mrefu utamsikia especial wakati huu maji yakionekana kuwa shingoni...

tuwaombe wapiga kura wa busanda wawe makini katika uchaguzi huu..wasikubali kununuliwa na wawe na hoja za msingi kwa wanasiasa kwani ni wakati mzuri kwao kupima maendeleo ya uwakilishi wao kisiasa....
 
kumjadili kada haitokusaidia chochote, i still stand with my position HAKUNA TUSI LOLOTE LILILOONGELEWA NA ZITTO.

Hakuna yeyote yule anayepaswa kukingiwa kifua ! i mean no ONE!

- Ninasema hivi acha vitisho kama una hoja weka hapa, Zitto aka Dowans hana jipya ni CCM-Mtandao.

FMES!
 
- Ninasema hivi acha vitisho kama una hoja weka hapa, Zitto aka Dowans hana jipya ni CCM-Mtandao.

FMES!
sawa sipingi hata moja!
vitisho gani ? ( kama nimetoa basi nawaachia mods wanifungie maana kutoa vitisho ni kuvunja sheria za forums, so ningependa sheria ifuate mkondo wake IWAPO UNACHOSEMA NI UKWELI, which i know is NOT)

sipo hapa kubishana na wewe wala na malecela wala kilango, lakini point yangu ni kwamba malecela hana lolote/jipya na ni aibu tu kwake yeye kama mzee mwenye busara, badala ya kutetea mema yeye anatetea uozo, na kama alivyosema zitto kuhusu malecela kama una lolote unadhani limekosewa na zitto mkosoe zitto na sio kulumbana na watu bila mpango!
 
Back
Top Bottom