Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Huyu Tinga Tinga sijui amelogwa, yeye sio Makamu Mwenyekiti wa CCM wala sio Mbunge wa kanda ya Ziwa. Nani kamwambia ajipendekeze kwenye uwanja wa vita huko? Akivuliwa nguo wakina FMES wanakuja kulia lia hapa. yeye anajua kuwa Magesa ni bora kuliko huyo mgombea wa CCM halafu akwenda kumuuza kwa sababu tu ya kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya taifa. Sasa unamlaumu vipi Zitto kuanika unafiki unaoendelea?

Asha

- Kwenye kampeni za uchaguzi unatakiwa kujali mbinu za chama chako, ila huwezi kuingilia mbinu za wengine, Malecela ni mjumbe wa kudumu wa CC na NEC ya CCM kwa hiyo ni haki yake kisheria kuwepo huko, kutukana ni haki yako kama ilivyo ya wengine pia hapa JF, it does not matter nani anayetukanwa ndio maana ninamtetea Mengi mpaka mwisho badala ya kumuuliza kwa nini anajipendekeza kwa sisi wananchi, mkuu mkishaanza kuuliza haki ya Malecela kuwepo huko Busanda sasa kisiasa mnasema wazi kwamba mnamuogopa na mmeshindwa tayari,

- Zitto analia eti kwa nini Malecela anafanya vikao vya siri, ebo yeye vile vikao vyake vya Dowans havikuwa vya siri? Yaaani sasa Asha mnataka kutupangia CCM wapi pa kufanyia vikao na saa? Sasa kufanya mikutano ya siri ni unafiki? au lazima Malecela awe na mawazo kama yako na Zitto aka Dowans, ndio hawi mnafiki? Zitto kama anajua hoja na matusi mbona alikimbia hapa JF? Asha Zitto ndiye atawawezesha kushinda Busanda? Kwa sababu anauliza kwa nini vikao vya CCM vinafanyika kwa siri? Wewe huoni mmeshashindwa tayari maana hata ameshaanza kulalamikia kuibiwa kura na hazijapigwa? Anaweka tayari njia ya kutokea, akishindwa aseme aliibiwa kura?

Mkuu again ni haki ya Malecela kuwepo huko Busanda, na ni haki yako na yangu kuwepo hapa JF, ku-support anything na anybody, ukimtukana mtu yoyote hata mwana JF bila sababu nitamsimamia, na hata kiongozi wa chama chochote kile, kuna viongozi na wananchi kama Mengi huwa sina tatizo kuwasimamia hapa au popote bila uoga wala kujali uwingi wa upande wa pili, na Malecela ni mmojawapo, hoja hujibiwa kwa hoja na matusi hujibiwa kwa matusi! Ya kutishana hamna hapa hata siku moja! Asha demokrasia hii sio lazima wote tuwe na mawazo kama yako ya kumuona Mengi ni tatizo, huwa tunakwua na mawazo tofauti katika demokrasia sio ajabu!

Otherwise tupo pamoja sana mkuu, tuendelee kukata ishus, najua uko karibu sana na huko Busanda lete habari na dataz! Leo Malecela amefanya nini mkuu? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!

 
Wakuu JF.

Hivi huyu GAME THEORY yuko vipi? Au maana ya jina lake (GT) linaakisi na hoja zake? Maana komenti zake nyingi huwa naziona zinamaanisha tafsiri ya Game Theory. Mwenye ufahamu zaidi naomba anifahamishe au GT mwenyewe akikakaa na kuanza kuzitathmini hoja zake anaweza akawa kwenye nafasi nzuri ya kutuambia kuwa hoja zake zinazingatia maana halisi ya game theory.

- Mkuu changia taifa, achana na personal GT ni GT na wewe ni wewe na mimi ni mimi, ya binafsi hayatusaidii hapa, taifa kwanza!

FMEs

 
- Mkuu Asha, wewe ninakuheshimu na nitakujibu kistaarabu ni kwamba huko Busanda kampeni ni kali sana, na toka jana nimekubali kwamba CCM ina wakati mgumu sana kwa sababu moja kubwa wamechelewa sana kwenda huko, Chadema waliwahi, ninarudia tena kwamba baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa CCM walioko Busanda ninakubali kwamba chama changu CCM kina wakati mgumu sana kushinda huko,

- However, Malecela kusema hoja kwamba wapinzani hawawezi kuleta maendeleo huko Busanda, kwangu ni hoja je wamewahi kuleta maendeleo wapi? Ninajua for a fact kwamba jimbo moja tu la Ndesamburo ndilo lenye maendeleo ambayo hayakuepelekwa na CCM, ni kwa sababu mzee Ndesamburo mwenyewe hutumia hata hela zake kuwasadia wananchi, kwa mfano one time nilimuona kwa macho yangu majuu akinunua malori ya Fire akiyapeleka jimboni kwake, sasa kuacha hili jimbo mengine yote kama yana maendeleo yamepelekwa na CCM, kama hakuna basi wamenyimwa kwa sababu ya siasa za CCM Vs Upinzani, hizi siasa hata majuu kwenye demokrasia za kweli zipo.

- Wabunge wa upinzani hawana mchango mzito bungeni kwa sababu kwanza ni wachache na besides wengi wao ni CCM anyways, kwa hiyo hoja inasimama Republicans wamekataa Stimulus Bill lakini kwa sababu ni wachache wameshindwa na Democrats ambao ni wengi zaidi yao, sasa ukisema Republicans hawana effect yoyote Congress unakua unakosea? Au ukisema Upinzani hawana effect kwenye bunge letu kwa nini unakwua unakosea? Kushinda kwa Chadema au upinzani Busanda ni kuongeza ruzuku kwa chama, lakini not in anyway or shape kubadili upepo wa upitishwaji wa miswaada bungeni kwa ajili ya wananchi, no way! hii kwangi ni reality sio siasa au blah! balh!

- Umri mkubwa wa Malecela au umri mdogo wa Zitto, Rostam, na Manji bado hakuna scientific studies hapa bongo kuthibitisha kwamba kuna effect katika kuleta maendeleo ya taifa, ya jimbo, au kuwa sound politically, Kikwete amechaguliwa kwa platform ya ujana, sasa kama umri ni ishu then kwa nini tunamlilia sana hapa kwamba ameturudisha nyuma? Mimi sijawahi kusikia mtu mmoja akitajwa katika uchaguzi ambaye wala sio mgombea kama huu, maana yake ni moja tu kwamba ni threat na ataishia kushinda huko, na pia media inauza kutokana na jina lake, meaning kwamba majina mengine yalioko huko Busanda sio effective kama la Malecela, kuaniza kisiasa mpaka biashara ya media! Sasa kama all the attention huko Busanda iko kwa Malecela, then ni clear kwamba atashinda tu tena sina wasi na hilo!

Othwerwise, tupo pamoja mkuu!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMEs!

Asante kwa kujibu kistaarabu

Wapinzani wanaweza kuleta maendeleo kumbuka karatu na hai.

Wapinzani wachache bungeni wanaweza kuzidi nguvu ya wabunge wengi wa CCM, si unakumbuka madhara ya Zitto kusimamishwa kwa hoja yake au unasahau pia Dr Slaa anavyokuwa wa maana bungeni kuliko halaiki ya wapiga makofi na wazomeaji?

Huyo mbunge wa Busanda kura zake haziwezi kuongeza ruzuku kwa kuwa ruzuku inahesabiwa kwa kura za mwaka 2005, lakini anaweza kuongeza sauti ya upinzani bungeni lakini pia ataleta hamasa ya kuongeza wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.

Malecela kwa umri wake wala sikatai awe mbunge wa Mtera, tatizo langu ni la yeye kujitembeza na kujipa kazi zisizozake za utinga tinga. haya alishayamaliza akiwa makamu mwenyekiti.

Sasa akiendelea kujipeleka peleka wajukuu watamuuliza yeye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti fedha za EPA zilipoibwa na wakina Mkapa na Mangula kupitia kwa Rostam na jeetu Patel; atajibu nini?

Hebu mwambie mzee arudi akapumzike, aacheni na uwizi wa kura- huo nao ni ufisadi na ni dhambi kwa Mungu

Asha
 
- Mkuu changia taifa, achana na personal GT ni GT na wewe ni wewe na mimi ni mimi, ya binafsi hayatusaidii hapa, taifa kwanza!

FMEs


You are right in this one. Watu wameondoka kwenye hoja kabisa na kuconcentrate on GT. Swala ni kuchangia hoja. Tukubali kuwa not all will think alike. Tukazanie mada siyo mtu binafis. GT hata tumfanyeje it won't do anything for the nation. Lets concentrate on what will actually save the nation. I think GT is the least of the nations worry.
 
1.
Asha Abdala;Asante kwa kujibu kistaarabu

Wapinzani wanaweza kuleta maendeleo kumbuka karatu na hai.

- Siyajui maendeleo ya Karatu, lakini ninamuamini sana DK. Slaa kwamba ninaamini yapo, Hai hapana yangekuwepo basi mgombea wa Chadema baada ya Mbowe angeshinda, the fact kwamba mgombea urais wa Chadema, aliyetoka ubunge Hai na kugombea urais alishindwa kumuweka anothe chadema inajisema yenyewe kwamba hakuna kitu huko!

2.
Wapinzani wachache bungeni wanaweza kuzidi nguvu ya wabunge wengi wa CCM, si unakumbuka madhara ya Zitto kusimamishwa kwa hoja yake au unasahau pia Dr Slaa anavyokuwa wa maana bungeni kuliko halaiki ya wapiga makofi na wazomeaji?

- Zitto na kufukuzwa bungeni it was wrong na aliyemfukuza ni Lowassa, co-owner wa Dowans, ambayo sasa Zitto anaitetea, does it make a sense kwako na the whole ishu ya ubunge wa Zitto na upinzani?

- Dk. Slaa ni kweli alikuwa effective lakini tatizo likawa wabunge wengi wa upinzani ni CCM anyways, halafu he was one man only Chadema inahitaji viongozi imara na wasafi kama Slaa wawe wengi, otherwise ni kufukuza upepo tu angani!

3.
Huyo mbunge wa Busanda kura zake haziwezi kuongeza ruzuku kwa kuwa ruzuku inahesabiwa kwa kura za mwaka 2005, lakini anaweza kuongeza sauti ya upinzani bungeni lakini pia ataleta hamasa ya kuongeza wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.

- Lakini haina maana TLP wataendelea kupata the same ruzuku sasa kukosekana wka mbunge wao mmoja, au? Hapa naomba darasa zaidi.

4.
Malecela kwa umri wake wala sikatai awe mbunge wa Mtera, tatizo langu ni la yeye kujitembeza na kujipa kazi zisizozake za utinga tinga. haya alishayamaliza akiwa makamu mwenyekiti.Sasa akiendelea kujipeleka peleka wajukuu watamuuliza yeye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti fedha za EPA zilipoibwa na wakina Mkapa na Mangula kupitia kwa Rostam na jeetu Patel; atajibu nini?Hebu mwambie mzee arudi akapumzike, aacheni na uwizi wa kura- huo nao ni ufisadi na ni dhambi kwa Mungu

Asha

- Malecela hakujipa kazi ndani ya CCM, kamati kuu imemuomba, ilimuomba Tarime, akakataa kwa hiyo huwa anakubali na kukataa depending, otherwise hapa huna hoja kwa sababu ni haki ya kila mwananchi kushiriki huko Busanda, wewe sio kiongozi wa anything, sasa authority ya kuuliza haki ya mzee kuwepo huko unaitoa wapi mkuu? Sasa mkipata huo utawala mna maana wazee wote watauliwa maana mnaoneakan mna taabu sana na wazee katika jamii,

- I mean kushabikia tununue Dowans ni dhambi zaidi mkuu, ya kuiba kura ni cover tu mkishindwa tumewazoea on that, hela za EPA walioziiba wanajulikana, lakini haiwezi kuwa sababu ya kumzuia mzee, kiongozi au mwananchi yoyote kuwepo huko Busanda, kama hamumuwezi mzee acheni siasa, lakini hoja hujibiwa kwa hoja, hamuwezi kushinda kwa ubabe wala matusi, na hamuwezi kutuamulia CCM wapi pa kufanyia vikao na saa, huyu Zitto aendelee kuchoma bendera kama wahuni wa US, kazaneni acheni kulia lia na Malecela, kelele mlizopiga tayari ni dalili za kumuogopa mzee, hiyo peke yake inasikitisha sana kwa chama cha demokrasia makini,

Serious political strategy ya kuzima umaarufu wa mzee huko Busanda ingekua ni kumu-ignore na kusema in the public kwamba wala hamna habari kama yupo, huku mkimtwanga kwa wananchi wa Busanda door to door, lakini all this attention hakuna mwananchi wa Busanda atakayekosa kutaka kumjua vizuri na hata kumpa kura, sasa mmeng'ang'ania kumtukana na kumtukuza huku kwenye mitandao as if wapiga kura wapo huku? I mean huku tutabishana tu yataisha je haya mabishano yatawasaidia nini wananchi wa Busanda?

- Again ni haki kikatiba Malecela kuwepo huko kama ilivyo haki yako pia!

Respect.

FMES!
 
- Sawa mimi nilifikiri unatishia kumtukana Mkulu wangu GT, otherwise Zitto ndiye hana jipya mkuu, maana sio siri na yeye ni CCM, sasa kama CCM imeoza basi na yeye ameoza au? Halafu hakuna mahali nimetukana Zito wala mama yake kwa hiyo hapo huna point mkuu!

- Halafu naomba nikuulize huko Busanda yupo Malecela tu? Mbona wengine hatuwasikii? Mema yako yaani ya Zitto kutetea Dowans huku DK. Slaa akikataa Dowans ile ile, maana yake ni moja kwamba mema yako sio lazima yawe na yangu, mimi ninaitetea CCM kama viongozi wengine wa CCM wanavyotetea huko Busanda, CCM tuna viongozi wachache wabovu so is Chadema, ya Zitto kuteeta Dowans kwangu ni uozo kwako ni sawa kwa sababu anayetetea ni Zitto, kwa hiyo hata kwenye hili la uozo huna point mkuu ni haki ya Malecela kama kiongozi mstaafu wa CCM kukitetea chama chake kama ilivyo haki yako kumtetea Zitto na Dowans ya Rostam.

- Otherwise hakuna anayetaka matusi ila wote tunaweza kuyarusha hakuna sababu ya kutishiana nyau! Na ninasema hivi Zitto zile dakika 15 za political fame zilishaisha, yeye sasa ni CCM the fact kwamba Chadema inaweza kumpeleka kwenye kampeni dhidi ya CCM ni dalili za Chadema kuishiwa mufilisi!, Chadema ninamuaminia DK. Slaa peke yake, wengine ni muflisi!

Respect

FMEs!
unajua nilikuwa namuaminia sana malecela, lakini hivi karibuni nae ameanza kula "ubwabwa" na mafisadi. Kauli yake ya kusema kwamba kumuachia JK agombee kwa awamu mbili mfululizo na asiwe na mpinzani ndani ya ccm kwa maana ni utamaduni wa ccm ILIKUWA SABABU TOSHA ya kunifanya nione huyu mzee amepitwa na wakati ( out of touch ) na hahitaji somo kueleweshwa maana it will cost time hadi yeye aelewe, if this is the case kwa nini tusiwaamini wengine wenye misimamo thabiti na wenye kuweza kukosoa pale panapostahili kukosolewa ?

Kauli hiyo ya malecela ya kuita mazoea mabaya "utamaduni wa ccm" ndio sababu iliyonipeleka kuamini kwamba MALECELA HANA LOLOTE, NA HAKUNA JIPYA ATAKALOLIONGELEA HUKO BUSANDA. Kama malecela kweli ana "thubutu" na kama kweli ana busara ya kuweza kuonya, kwa nini asifanye kitu kimoja tu, cha kuwaambia akina JK wasifanye mikutano yao ya ccm ndani ya ikulu ? au hilo pia anashindwa ? ndipo hapo nilipofikia kusema kwamba malecela nae anakula ubwabwa na mafisadi!

Kauli hiyo ya malecela kusema kwamba ni utamaduni kumuachia rais agombee bila kupingwa, ni tosha kumuharibia legacy yake kama kiongozi ( KAMA LEGACY YAKE NI NZURI, WHICH I DOUBT )!!

Haina haja ya kujua kuna wana-ccm wangapi huko Busanda, lakini iwapo kauli tata zitatolewa ( zimeshatolewa na malecela ) basi mimi kama kada sitosita kuzisema. Hapa kinachoongelewa ni maamuzi na kauli za viongozi na sio viongozi wao kama viongozi !!! Kwa nini unadhani malecela anaonewa ?

Aliyesema wewe umemtukana zitto nani ? na sawa sina point, wewe ndio unazo mkuu wangu, tena unazo nyingi lakini nitawaachia wenzangu hapa barazani nao waseme kama una point au la ! i dont mind kuambiwa ninachoongea ni pumba, as long as i get my point across !

Unashangaa zitto kuunga mkono suala la dowans ? kwani malecela hamuungi mkono jk ? je jk hana connection na RA ? Anayo ! Je malecela anajua uwepo wa connection ya JK na RA ? Anajua ! Je malecela anafahamu RA ni fisadi kama ulivyosema ? NDIO, sasa iwapo malecela anamuunga mkono JK ambaye ana connection na fisadi RA, judgement/reasoning ya malecela ipo vipi unadhani ?? NIKISEMA MALECELA ANAKULA UBWABWA NA MAFISADI UTAKATAA ? There are things you simply cant dispute, na hapo hata hatujaingia kwenye rekodi yake mzazi !

Kazi na Dawa !
 
Last edited:
unajua nilikuwa namuaminia sana malecela, lakini hivi karibuni nae ameanza kula "ubwabwa" na mafisadi. Kauli yake ya kusema kwamba kumuachia JK agombee kwa awamu mbili mfululizo na asiwe na mpinzani ndani ya ccm kwa maana ni utamaduni wa ccm ILIKUWA SABABU TOSHA ya kunifanya nione huyu mzee amepitwa na wakati ( out of touch ) na hahitaji somo kueleweshwa maana it will cost time hadi yeye aelewe, if this is the case kwa nini tusiwaamini wengine wenye misimamo thabiti na wenye kuweza kukosoa pale panapostahili kukosolewa ?

- Kukosoa kwa kutuambia Dowans ni safi? Chama gani cha siasa chenye mapya kinachoweza kwenda kwenye kampeni na kulilia kujua upande wa pili wanafanya nini! Kwa nini wanafanya mikutano ya siri unasema haya ndio mapya ya kutusaidia taifa? Katika maneno yote ya Zitto ni wapi ametoa hoja ya kulisaidia taifa? Kwangu chadema na Zitto wamepitwa na wakati, kwa sababu how can you let Zitto speak leo mwaka 2009 kwenye kampeni ya uchaguzi dhidi ya CCM?

- Hoja yako hapo ni umri wa Malecela ambaye wala sio mgombea, au rais wa jamhuri sasa hata akija mgeni hapa si atauliza hivi Malecela ndio nani huko Busanda? Eti utasema ni mzee aliyepitwa na wakati, sasa Why all this attention? Mkuu jifunzeni siasa, Chadema mnahitaji sana kupigwa msasa wa siasa, hizi kelele zote maana yake ni moja mnamuogopa, I mean unasema Chadema wana mapya kumuita Malecela bajaji inaweza kukupatia kura na wananchi, yes inakupatia umaarufu huku Jf, na kuuza magazeti, lakini kisiasa ni waste of time, ndio maana siiku zote mnaishia kutupa moya hapa kwamba mtashinda kumbe ni uongo, halafu mnaishia kuibiwa kura!

- Halafu kumuamini au kutomuamini kwako Malecela, hakumpunguzii wala kuongeza anything, ila ni mawazo yako tu kama mimi nilivyo na yangu, ila naomba nikuambie one thing kiongozi aliyepitwa na wakati ni waste of time hata kumzungumzia!


Kauli hiyo ya malecela ya kuita mazoea mabaya "utamaduni wa ccm" ndio sababu iliyonipeleka kuamini kwamba MALECELA HANA LOLOTE, NA HAKUNA JIPYA ATAKALOLIONGELEA HUKO BUSANDA. Kama malecela kweli ana "thubutu" na kama kweli ana busara ya kuweza kuonya, kwa nini asifanye kitu kimoja tu, cha kuwaambia akina JK wasifanye mikutano yao ya ccm ndani ya ikulu ? au hilo pia anashindwa ? ndipo hapo nilipofikia kusema kwamba malecela nae anakula ubwabwa na mafisadi!

- Mkuu CCM inao utamaduni kwa mfano rais lazima awe wa dini moja kubwa kwa kupokezana, hatuna sheria on it that lakini huo ni utamaduni wa CCM, na ni utamaduni wa dunia nzima, naomba unitajie nchi moja duniani ambako a sitting president alitolewa na mgombea wa chama chake?

- CCM ni chama tawala, na serikali ni ya CCM, sasa mkuu rais wa jamhuri anakuwa kazini 24 hours, kama kuna ishus muhimu za taifa ambazo zinamfanya asitoke Ikulu then hawezi kutoka Ikulu, na anything of serious importance politically ni lazima kimfuate Ikulu, kama Usalama wanamuambia hawezi kutoka Ikulu hawezi mkuu kuna sababu nyingi za kiutawala za kufanyika kwa baadhi ya vikao vya CCM CC Ikulu,

- Ya kula ubwabwa na mafisadi we all do that, kwa sababu in one way or another wananchi karibu wote wa Tanzania we are connected somehow somewhere, kama CCm na serikali yake ni fisadis, basi hata kupokea ruzuku ya CCM na serikali yake ni kuwa fisadi, Vodacom ni ya fisadi sasa ukitumia simu zake unakwua nini mkuu fisadi! kwa hiyo be careful na maneno kabla ya kuyarusha mkuu maana mengine yanatuhusu wote waananchiw Tanzania.


Kauli hiyo ya malecela kusema kwamba ni utamaduni kumuachia rais agombee bila kupingwa, ni tosha kumuharibia legacy yake kama kiongozi ( KAMA LEGACY YAKE NI NZURI, WHICH I DOUBT )!!

Haina haja ya kujua kuna wana-ccm wangapi huko Busanda, lakini iwapo kauli tata zitatolewa ( zimeshatolewa na malecela ) basi mimi kama kada sitosita kuzisema. Hapa kinachoongelewa ni maamuzi na kauli za viongozi na sio viongozi wao kama viongozi !!! Kwa nini unadhani malecela anaonewa ?

- Legacy anayeiandika ni wewe mkuu then itakua mbaya maana kwa nini anakubali mikutano ya CCM ifanyike Ikulu, lakini kama huandiki wewe itakua fair maana Malecela kama wengine ni bina-adam, halafu hakuna aliyekukataza kusema anything kuhusu Busanda wala Malecela ni haki yako, ila itabidi uheshimu na haki za wengine kukujibu, Malecela sio kiongozi ni mstaafu kwa hiyo rekebisha hiyo kauli, nani amesema Malecela anaonewa hapa? Wewe unaweza kumuonea Malecela? Hapa tunajadili siasa ya taifa ambayo mmeamua kuigeuza Malecela, sasa tuendelee kujadili mkuu hakuna noma! Haya maneno maneno ni ya kufurahishana tu hapa JF lakini bajaji haiwezi kumsaidia anything mwananchi wa Busanda, Zitto bingwa hoja na kejeli alikimbia hapa bila kuaga leo eti ana nguvu ya kusiaidia Chadema kushidna ubunge, that is inredible! Inaonyesha tu Tanzania tulivyo na safari ndefu! Mimi ningekua Chadema ningeruhusu DK. Slaa tu kuzungumza kwa niaba ya chama, maana he is the only clean leader huko kwa maoni yangu!

Respect na sasa ni saa ya kulala kesho!, Otherwise I love it tutaendelea kesho mkuu!

FMES
 
Unashangaa zitto kuunga mkono suala la dowans ? kwani malecela hamuungi mkono jk ? je jk hana connection na RA ? Anayo ! Je malecela anajua uwepo wa connection ya JK na RA ? Anajua ! Je malecela anafahamu RA ni fisadi kama ulivyosema ? NDIO, sasa iwapo malecela anamuunga mkono JK ambaye ana connection na fisadi RA, judgement/reasoning ya malecela ipo vipi unadhani ?? NIKISEMA MALECELA ANAKULA UBWABWA NA MAFISADI UTAKATAA ? There are things you simply cant dispute, na hapo hata hatujaingia kwenye rekodi yake mzazi !

Kazi na Dawa !

- Sasa naomba nikuulize hivi Chadema kama chama wanamtambua JK kama rais wa jamhuri, sasa kwani hawajui connections zake na Rostam? Sasa nikisema chadema nao ni mafisadi kwa mantiki yako je vipi nitakua ninakosea?

- Unasema tuingilie uzazi wa viongozi wetu wa CCM na Upinzani you really want that? Halafu unasema ya kuwaachia watu hapa unafikiri mimi huwa ninajali hayo ya watu? Ninajali hoja na ukweli wa hoja, na dataz wewe subiri ushangiliwe na watu wote hapa mimi ninakta ishus tu mkuu!

FMES!
 
Hizi Siasa za Kulambana miguu sijui zitatufikisha wapi..........kuuza uhuru wa kuwa na free mind ni tatizo linalotukabili Taifa letu.......nyie endeleeni tu.....
 
Field Marshall Es,
Mkuu nimekusikia sana lakini mkuu wangu mbona unarudia yaleyale usiyoyataka?.. Naposoma hoja zako naona unamvua nguo Zitto kama wengine wanavyojaribu kwa Malecela. Binafsi naiona lugha moja tu hapa isipokuwa wahusika ndio tofauti..
Nilitegemea ungekuwa tofauti kwa sababu kipenzi cha Zitto anaweza kudai Zitto hakukimbia JF isipokuwa alitingwa na kazi nyingi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya chama kwa uchaguzi wa mwaka 2010.
Zitto sii msafi, wala Malecela na hata Dr. Slaa wote hawa ni binadamu wana mapungufu yao. na sidhani kama mapungufu yao wote hawa yanahusiana na uchaguzi wa Busanda kwani Zitto kukimbia JF pia haimsaidii kitu mwananchi wa Busanda..Na nakubaliana nawe sana tu kuwa Malecela ana kila haki ya kuwepo Busanda kama mpiga debe mkubwa wa chama. Nyerere alifanya hivyo kwa Mkapa wakati hakuwa na wadhifa wowote wa serikali wala chama.. na tulipiga kura kumweka Mkapa mara mbili Ikulu..

Wengi hapa tunakubali kwamba Zitto alichemsha na pengine hata yeye anafahamu kuwa alichemsha lakini that's not the issue here - Zitto sii mgombea..na sidhani kama wewe unakubali kuwa Mzee Malecela kisha wahi kuchemsha..
Binafsi nampenda sana mzee Malecela na ni mmoja kati ya wazee naowaheshimu na kuwapenda pengine hata nadiriki kusema angeweza kuwa rais bora kuliko Mwinyi na Mkapa..na CV yake ktk uongozi ni kubwa kuliko viongozi wengi CCM..Isipokuwa tuelewe tu kwamba pamoja na kwamba Chadema ina wachache wenye sifa au tuseme huyo mmoja Dr.Slaa mwenye sifa zinazokubalika, mkuu wangu baada ya kustaafu kina Malecela, Salim, Warioba, Tandau, Mwakawago na wazee wengine waliokuwa na moyo wa kitaifa sidhani kama CCM imebakia na mtu hata mmoja mwenye sifa hata zilizo kukaribiana na Dr. Slaa - HAKUNA..
Hivyo, hadi sasa hivi Chedema wana bao moja, CCM bila..
 
Binafsi ningependa sana CCM ishindwe na hasa kwenye hiki kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

Sababu za kutaka wapinzani washinde ni hizi zifuatazo:

1. Iwapo CCM itashindwa kwenye Jimbo ambalo walikuwa wanalishikilia, hiyo itakuwa ni changamoto kwa CCM ili iweze kujisafisha pamoja na kujipambanua na ufisadi, hoja ambayo imekuwa ikitumiwa na wapinzani. Hii itawafanya wakumbuke ile kauli ya Mwakyembe kwamba watanzania wa leo si mabwege tena kiasi kwamba unaweza kwenda kuwadanganya na kuwapa ahadi hewa na bado wakakupa kura zao. Kwa hiyo ili kushinda uchaguzi wa 2010 itabidi CCM wawe na Ilani nzuri inayotekelezeka pamoja na ahadi zinazotekelezeka.

2. CCM ya sasa ina makundi, na ni makundi hayo hayo ndiyo ambayo yanaendelea kukimaliza chama; makundi hayo ni waumini wa ufisadi a.k.a mtandao na la pili ni wale ambao wanapinga ufisadi, na kakundi ka tatu ni bendera fuata upepo ambao mara nyingi wamekuwa wakitumiwa na mafisadi ili kupitisha maamuzi pindi kura zikihitajika kutumika. Hali ndani ya CCM si shwari na kinachowaumiza ni ufisadi na makundi. Diallo ametakiwa kuondoka Busanda pamoja na kwamba ni mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mwanza, mjumbe wa NEC na pia kigogo mzito sana kwenye siasa za Kanda ya Ziwa. Kisa cha kuondolewa ni kwamba mtu wake (Bwana Max) alienguliwa kwenye kura za maoni na pia alipoombwa aende kwenye kampeni ili amsaidie mgombea wa CCM, Bwana Max alikataa akasema hayuko tayari kuwasaliti wananchi wa Busanda. Kama mgombea wa CCM atashindwa basi Chama kitalazimika/shinikizwa kuvunja makundi na hasa kundi la mtandao ambalo limekuwa likiiumiza nchi kwa kuwa wengi wao ni mafisadi.

3. Mzee Malecela ndani ya CCM ni mtu safi in terms of ufisadi na makundi na ndiyo maana amekuwa akitumika pale chama kinapoona kuna upinzani wa kutosha na hasa nyakati za chaguzi ndogo. Usafi wa Mzee Malecela unamfanya aonekane kuwa ni mpiga kampeni ambaye yuko neutral na pia hajawahi kuandikwa na magazeti katika miaka ya hivi karibuni kwamba ni mmoja wa mafisadi. Iwapo CCM itashindwa huko Busanda basi wazee kama akina Malecela hawatakubali kuenda kwenye kampeni kirahisi kwa kuwa hata wao wanaona aibu/noma kuzomewa na wapiga kura. Kwa hiyo in a way Chama kinaweza kulazimika kutafakari nini kifanyike ili kupunguza hiyo zomea zomea na pia kujipanga upya ili ikifika 2010 wasije wakapoteza viti vingi vya ubunge. Ikifika 2010 kila mgombea itabidi ajipigie kampeni kwenye jimbo lake bila support ya uongozi wa chama kitaifa.

Ikitokea kwamba CCM imeshinda basi tumeliwa kwa kuwa CCM will take Tanzanians for granted na hivyo ufisadi ndiyo utazidi kushamiri maana wanajua kwamba hata wakifanya ufisadi bado watanzania wataendelea kuwachagua tu.
 
Mzee kapelekwa huko kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi ya kuiba kura za wananchi. Siwaonei haya watu kama hawa.

Katika uchaguzi wa 1995, ilibidi Mwenyekiti wa CCM wa wakati ule aibe mwenyewe kura. Sote tunajua alibadilisha matokeo ya uchaguzi Zanzibar (ambako CUF walikuwa wameshinda) na kwenye baadhi ya sehemu bara (ili kumnyima Mrema ushindi).

Ilipofika uchaguzi wa 2000, Mzee aliombwa asimamiye yeye uchaguzi kwa upande wa CCM. Alianza kwa kuwaasa vijana wa CCM wapigane na wapinzani kama ikibidi. Wale wasio na kumbukumbu fupi watakumbuka hayo.

Kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wana CCM dhidi ya ushindi wa Dr. Slaa Karatu iliwafungua Watanzania macho kuhusu jinsi CCM inavyodharau kura zao. Ulitolewa ushahidi wa wazi mahakamani jinsi viongozi wa CCM walivyojaribu kubadili matokeo ya uchaguzi katika sehemu mbali mbali. Yote hayo yaliwekwa hapa JF na tumeyaona.

CCM watajaribu kuiba kura Busanda. Hiyo ni kawaida yao. Wamemtuma Malechela kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi hiyo.

It is also my thesis that CCM is delaying the issuance of national identity cards for the simple reason proper identification could interfere with their usual methods of rigging elections. Prove me wrong if you can.
Mambo ya aibu sana....mzee kama yule 75yrs anaiba! keshafikia kikomo aliyofanya kwa taifa tunamshukuru sasa kuanza kuwaibia haki wananchi na uzee huu haipendezi
 
jamani wekeni picha hizo tuone hiyo halaiki iliyokuwepo kwenye huo mkutano ili izidi kuwatia hofu chadema.
 
- Zitto analia eti kwa nini Malecela anafanya vikao vya siri, ebo yeye vile vikao vyake vya Dowans havikuwa vya siri? Yaaani sasa Asha mnataka kutupangia CCM wapi pa kufanyia vikao na saa? Sasa kufanya mikutano ya siri ni unafiki? au lazima Malecela awe na mawazo kama yako na Zitto aka Dowans, ndio hawi mnafiki? Zitto kama anajua hoja na matusi mbona alikimbia hapa JF? Asha Zitto ndiye atawawezesha kushinda Busanda? Kwa sababu anauliza kwa nini vikao vya CCM vinafanyika kwa siri? Wewe huoni mmeshashindwa tayari maana hata ameshaanza kulalamikia kuibiwa kura na hazijapigwa? Anaweka tayari njia ya kutokea, akishindwa aseme aliibiwa kura?

Usiku wa kuamkia jana chadema walivamia kikao kimoja wapo cha siri cha ccm. Wamemkamata Diwani wa Busanda (CCM) Alphonce Ngoko Matonange na balozi wa nyumba kumi kumi wakinunua shahada za wapiga kura kwenye hicho kikao cha siri cha ccm. Vikao vya usiku vya siri vya CCM ni vikao vya kununua kadi za wapiga kura. Hamna lingine lolote linaloendelea. Ni kipi wanachoshindwa kukiongelea mchana mpaka wakijadili giza likishaingia? Na hao waliobambwa wamesema wametumwa na viongozi wa juu wa ccm kuendesha hilo zoezi. Zitto aliliongelea hilo jukwaani Busanda na sasa upo ushahidi kwamba alichokuwa akilalamika kweli kipo. Malecela alikuwa tingatinga la kusomba kura enzi zake siku hizi amegeuka kibajaji cha kuiba kura.


Na ninasema hivi Zitto zile dakika 15 za political fame zilishaisha, yeye sasa ni CCM the fact kwamba Chadema inaweza kumpeleka kwenye kampeni dhidi ya CCM ni dalili za Chadema kuishiwa mufilisi!, Chadema ninamuaminia DK. Slaa peke yake, wengine ni muflisi!

Ina maana dakika 15 za political fame ya Mzee Malecela ndio bado zipo? Mie nafikiri alipodhalilishwa kwa kunyimwa kugombea urais na mkapa he siezed to exist politically. Unaposema Zitto ni ccm basi kwa mantiki hio Nape na Kilango ni Chadema-mtandao pia. Kama si hivyo basi utuambie Zitto alichukua kadi ya ccm lini na wapi? Na inakuwaje kwamba ni wewe peke yako unayejua hata viongozi wa chadema wasijue? Na ni vipi mwana ccm akapanda kwenye jukwaa la chadema "akawatukana" ccm? Naomba tugange hoja iliyopo mbele yetu, mambo ya hisia na matamanio tuachane nayo.

Mimi simwamini kiongozi yeyote wa ccm hivyo kuwapeleka wakina msekwa na malecela kwenye kampeni dhidi ya chadema ni dalili za ccm kuishiwa mufilisi! Yote hayo tisa, tusubiri tarehe 24 tuone kweli mufilisi ni nani kwa sababu wenye kutapatapa tumeshawaona.
 
Wanafunzi wachapwa kwa kuizomea CCM

.Diwani akamatwa akiorodhesha shahada

Na Faida Muyomba, Busanda
Monday, 11 May 2009 16:33
Source: Majira


WANAFUNZI sita wa Shule ya Sekondari Butundwe mjini hapa wamechapwa viboko sita kila mmoja na kupewa adhabu ya kufyeka huku wengine wakigomea adhabu hiyo baada ya kuuzomea msafara wa mgombea ubunge Jimbo la Busanda kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia kutokana na tukio hilo, wazazi wa wanafunzi hao wameandamana hadi
shuleni hapo kuuona uongozi kwa lengo la kubaini kwa nini watoto wao
walifanyiwa kitendo hicho walichokilaani kuwa ni kinyume cha sheria.

Shule hiyo iko katika kijiji alichozaliwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Finias Magesa ambaye pia aliwahi kujitolea kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa saa 10 jioni wakati msafara wa kampeni za mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Bi. Lolensia Bukwimba ulipopita jirani na shule hiyo na wanafunzi kuzomea huku wakishika vichwani na kuonesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA.

Hali hiyo ya kuzomea ilimuudhi mmoja wa makada wa CCM, Bw. Oscar Magoli
ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nyakagomba ambaye alimfuata Mkuu wa shule hiyo Bi. Monica Nzungu.

Mara baada ya kuambiwa tukio hilo, Mkuu huyo shule alimwamuru mwalimu mmoja kuwachapa viboko wanafunzi wote, lakini wengine waligoma hivyo kufanikiwa kuwachapa hao ambao wote ni wa kidato cha kwanza.

Baada ya hali hiyo, jana wazazi wa wanafunzi hao waliandamana hadi shuleni hapo na kulazimika kuitisha kikao cha dharura na Mkuu wa shule hiyo ambaye hata hivyo alikana kuagiza mwalimu kuwachapa viboko wanafunzi hao.

Alidai alichosema yeye ni kuwaonya wanafunzi kutoshabikia vyama vyovyote vya siasa, lakini si kuwapiga wanafunzi kama alivyofanya mwalimu huyo ambaye anadaiwa kutoroka tangu siku ya tukio na hajulikani mahali alipo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa shule alilazimika kuwaomba msamaha wazazi wa wanafunzi hao na kuwa kitendo hicho hakitorudiwa tena kufanywa na mwalimu yeyote shuleni hapo.

Katika hatua nyingine, CHADEMA imemkamata Diwani wa Kata ya Busanda (CCM), Bw. Alphonce Matonange na makada wawili wa chama hicho wakidaiwa kuorodhesha majina na shahada za wapiga kura kwa lengo la kuzinunua.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Busanda, SSP Kimea alisema tayari watu hao wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Geita.

Alisema mbali ya diwani huyo wengine wanaoshikiliwa ni Bw. Abdallah Ibrahim na Bw. Japhet Shilungule ambao walikutwa wakiwa na orodha ya majina zaidi ya 20 pamoja na namba za shahada za wapiga kura.

"Tunawashikilia watu hao watatu wakati tukiendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo," alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa walikamatwa juzi saa 2 usiku.
 
Freedom of Expression hiyo...Ingekuwa kitu kingine kuchoma bendera ya nchi, lakini kwa vile ni bendera ya chama, ni kitu cha kawaida kabisa!

Swali langu: Hivi, ina-make sense kufanya uchaguzi sasa ivi, ambapo utafanyika uchaguzi mwingine mkuu 2010? Kwa wananchi wa Busanda kukosa mwakilishi bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja kunawadhuru kiasi gani, ukilinganisha na hela itakayoliwa kufanya chaguzi mbili ndani ya mwaka mmoja? Wangefanyiwa nini ndani ya huo mwaka?
 
siku hizi jf ...tumezidi kwa newspaper clips ....habari za uchunguzi zetu wenyewe ndio tunataka......bora tuwe na thread chache tulizoanzisha wenyewe kuliko kujaza..clips cut za mwananchi na mtanzania daima hapa....

halafu pia watu wana post thread ambazo tayari zipo.....ukiangalia thread za uchaguzi wa busanda ..zipo kama kumi humu...kwanini mtu ukikita thread ipo usipost humohumo

mimi naomba moderator aunganishe thread zote zinazoongelea subject moja ...
 
1.


- Zitto na kufukuzwa bungeni it was wrong na aliyemfukuza ni Lowassa, co-owner wa Dowans, ambayo sasa Zitto anaitetea, does it make a sense kwako na the whole ishu ya ubunge wa Zitto na upinzani?

Huku Malecela Akishindilia Msumari wa Mwisho. Malecela naye ni Dowans.
 
hii inanikumbusha mwaka 1995 pale wanafunzi wengi walipokuwa wanakiunga mkono chama cha NCCR-Mageuzi na kupigwa sana na walimu makada wa Chama Chenye Mwenyewe pia Polisi waliwafuata wanafunzi wa baadhi ya shule na kuwatia lupango kwa madai wameleta vurugu wakati wanafunzi walikuwa wanashangilia na kusukuma magari ya mgobea wa NCCR-Mageuzi.
Dhahama hii imewakuta sana wale waliokuwa shule za boarding.

Hongera wazazi kwa kutokubali watoto wenu kuonewa kwa sababu mwalimu anamapenzi yaliyopitiliza ya chama chake.
 
Back
Top Bottom