William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Huyu Tinga Tinga sijui amelogwa, yeye sio Makamu Mwenyekiti wa CCM wala sio Mbunge wa kanda ya Ziwa. Nani kamwambia ajipendekeze kwenye uwanja wa vita huko? Akivuliwa nguo wakina FMES wanakuja kulia lia hapa. yeye anajua kuwa Magesa ni bora kuliko huyo mgombea wa CCM halafu akwenda kumuuza kwa sababu tu ya kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya taifa. Sasa unamlaumu vipi Zitto kuanika unafiki unaoendelea?
Asha
Wakuu JF.
Hivi huyu GAME THEORY yuko vipi? Au maana ya jina lake (GT) linaakisi na hoja zake? Maana komenti zake nyingi huwa naziona zinamaanisha tafsiri ya Game Theory. Mwenye ufahamu zaidi naomba anifahamishe au GT mwenyewe akikakaa na kuanza kuzitathmini hoja zake anaweza akawa kwenye nafasi nzuri ya kutuambia kuwa hoja zake zinazingatia maana halisi ya game theory.
- Mkuu Asha, wewe ninakuheshimu na nitakujibu kistaarabu ni kwamba huko Busanda kampeni ni kali sana, na toka jana nimekubali kwamba CCM ina wakati mgumu sana kwa sababu moja kubwa wamechelewa sana kwenda huko, Chadema waliwahi, ninarudia tena kwamba baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa CCM walioko Busanda ninakubali kwamba chama changu CCM kina wakati mgumu sana kushinda huko,
- However, Malecela kusema hoja kwamba wapinzani hawawezi kuleta maendeleo huko Busanda, kwangu ni hoja je wamewahi kuleta maendeleo wapi? Ninajua for a fact kwamba jimbo moja tu la Ndesamburo ndilo lenye maendeleo ambayo hayakuepelekwa na CCM, ni kwa sababu mzee Ndesamburo mwenyewe hutumia hata hela zake kuwasadia wananchi, kwa mfano one time nilimuona kwa macho yangu majuu akinunua malori ya Fire akiyapeleka jimboni kwake, sasa kuacha hili jimbo mengine yote kama yana maendeleo yamepelekwa na CCM, kama hakuna basi wamenyimwa kwa sababu ya siasa za CCM Vs Upinzani, hizi siasa hata majuu kwenye demokrasia za kweli zipo.
- Wabunge wa upinzani hawana mchango mzito bungeni kwa sababu kwanza ni wachache na besides wengi wao ni CCM anyways, kwa hiyo hoja inasimama Republicans wamekataa Stimulus Bill lakini kwa sababu ni wachache wameshindwa na Democrats ambao ni wengi zaidi yao, sasa ukisema Republicans hawana effect yoyote Congress unakua unakosea? Au ukisema Upinzani hawana effect kwenye bunge letu kwa nini unakwua unakosea? Kushinda kwa Chadema au upinzani Busanda ni kuongeza ruzuku kwa chama, lakini not in anyway or shape kubadili upepo wa upitishwaji wa miswaada bungeni kwa ajili ya wananchi, no way! hii kwangi ni reality sio siasa au blah! balh!
- Umri mkubwa wa Malecela au umri mdogo wa Zitto, Rostam, na Manji bado hakuna scientific studies hapa bongo kuthibitisha kwamba kuna effect katika kuleta maendeleo ya taifa, ya jimbo, au kuwa sound politically, Kikwete amechaguliwa kwa platform ya ujana, sasa kama umri ni ishu then kwa nini tunamlilia sana hapa kwamba ameturudisha nyuma? Mimi sijawahi kusikia mtu mmoja akitajwa katika uchaguzi ambaye wala sio mgombea kama huu, maana yake ni moja tu kwamba ni threat na ataishia kushinda huko, na pia media inauza kutokana na jina lake, meaning kwamba majina mengine yalioko huko Busanda sio effective kama la Malecela, kuaniza kisiasa mpaka biashara ya media! Sasa kama all the attention huko Busanda iko kwa Malecela, then ni clear kwamba atashinda tu tena sina wasi na hilo!
Othwerwise, tupo pamoja mkuu!
Respect.
Wazee wa sauti ya umeme FMEs!
- Mkuu changia taifa, achana na personal GT ni GT na wewe ni wewe na mimi ni mimi, ya binafsi hayatusaidii hapa, taifa kwanza!
FMEs
Asha Abdala;Asante kwa kujibu kistaarabu
Wapinzani wanaweza kuleta maendeleo kumbuka karatu na hai.
Wapinzani wachache bungeni wanaweza kuzidi nguvu ya wabunge wengi wa CCM, si unakumbuka madhara ya Zitto kusimamishwa kwa hoja yake au unasahau pia Dr Slaa anavyokuwa wa maana bungeni kuliko halaiki ya wapiga makofi na wazomeaji?
Huyo mbunge wa Busanda kura zake haziwezi kuongeza ruzuku kwa kuwa ruzuku inahesabiwa kwa kura za mwaka 2005, lakini anaweza kuongeza sauti ya upinzani bungeni lakini pia ataleta hamasa ya kuongeza wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.
Malecela kwa umri wake wala sikatai awe mbunge wa Mtera, tatizo langu ni la yeye kujitembeza na kujipa kazi zisizozake za utinga tinga. haya alishayamaliza akiwa makamu mwenyekiti.Sasa akiendelea kujipeleka peleka wajukuu watamuuliza yeye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti fedha za EPA zilipoibwa na wakina Mkapa na Mangula kupitia kwa Rostam na jeetu Patel; atajibu nini?Hebu mwambie mzee arudi akapumzike, aacheni na uwizi wa kura- huo nao ni ufisadi na ni dhambi kwa Mungu
Asha
unajua nilikuwa namuaminia sana malecela, lakini hivi karibuni nae ameanza kula "ubwabwa" na mafisadi. Kauli yake ya kusema kwamba kumuachia JK agombee kwa awamu mbili mfululizo na asiwe na mpinzani ndani ya ccm kwa maana ni utamaduni wa ccm ILIKUWA SABABU TOSHA ya kunifanya nione huyu mzee amepitwa na wakati ( out of touch ) na hahitaji somo kueleweshwa maana it will cost time hadi yeye aelewe, if this is the case kwa nini tusiwaamini wengine wenye misimamo thabiti na wenye kuweza kukosoa pale panapostahili kukosolewa ?- Sawa mimi nilifikiri unatishia kumtukana Mkulu wangu GT, otherwise Zitto ndiye hana jipya mkuu, maana sio siri na yeye ni CCM, sasa kama CCM imeoza basi na yeye ameoza au? Halafu hakuna mahali nimetukana Zito wala mama yake kwa hiyo hapo huna point mkuu!
- Halafu naomba nikuulize huko Busanda yupo Malecela tu? Mbona wengine hatuwasikii? Mema yako yaani ya Zitto kutetea Dowans huku DK. Slaa akikataa Dowans ile ile, maana yake ni moja kwamba mema yako sio lazima yawe na yangu, mimi ninaitetea CCM kama viongozi wengine wa CCM wanavyotetea huko Busanda, CCM tuna viongozi wachache wabovu so is Chadema, ya Zitto kuteeta Dowans kwangu ni uozo kwako ni sawa kwa sababu anayetetea ni Zitto, kwa hiyo hata kwenye hili la uozo huna point mkuu ni haki ya Malecela kama kiongozi mstaafu wa CCM kukitetea chama chake kama ilivyo haki yako kumtetea Zitto na Dowans ya Rostam.
- Otherwise hakuna anayetaka matusi ila wote tunaweza kuyarusha hakuna sababu ya kutishiana nyau! Na ninasema hivi Zitto zile dakika 15 za political fame zilishaisha, yeye sasa ni CCM the fact kwamba Chadema inaweza kumpeleka kwenye kampeni dhidi ya CCM ni dalili za Chadema kuishiwa mufilisi!, Chadema ninamuaminia DK. Slaa peke yake, wengine ni muflisi!
Respect
FMEs!
unajua nilikuwa namuaminia sana malecela, lakini hivi karibuni nae ameanza kula "ubwabwa" na mafisadi. Kauli yake ya kusema kwamba kumuachia JK agombee kwa awamu mbili mfululizo na asiwe na mpinzani ndani ya ccm kwa maana ni utamaduni wa ccm ILIKUWA SABABU TOSHA ya kunifanya nione huyu mzee amepitwa na wakati ( out of touch ) na hahitaji somo kueleweshwa maana it will cost time hadi yeye aelewe, if this is the case kwa nini tusiwaamini wengine wenye misimamo thabiti na wenye kuweza kukosoa pale panapostahili kukosolewa ?
- Kukosoa kwa kutuambia Dowans ni safi? Chama gani cha siasa chenye mapya kinachoweza kwenda kwenye kampeni na kulilia kujua upande wa pili wanafanya nini! Kwa nini wanafanya mikutano ya siri unasema haya ndio mapya ya kutusaidia taifa? Katika maneno yote ya Zitto ni wapi ametoa hoja ya kulisaidia taifa? Kwangu chadema na Zitto wamepitwa na wakati, kwa sababu how can you let Zitto speak leo mwaka 2009 kwenye kampeni ya uchaguzi dhidi ya CCM?
- Hoja yako hapo ni umri wa Malecela ambaye wala sio mgombea, au rais wa jamhuri sasa hata akija mgeni hapa si atauliza hivi Malecela ndio nani huko Busanda? Eti utasema ni mzee aliyepitwa na wakati, sasa Why all this attention? Mkuu jifunzeni siasa, Chadema mnahitaji sana kupigwa msasa wa siasa, hizi kelele zote maana yake ni moja mnamuogopa, I mean unasema Chadema wana mapya kumuita Malecela bajaji inaweza kukupatia kura na wananchi, yes inakupatia umaarufu huku Jf, na kuuza magazeti, lakini kisiasa ni waste of time, ndio maana siiku zote mnaishia kutupa moya hapa kwamba mtashinda kumbe ni uongo, halafu mnaishia kuibiwa kura!
- Halafu kumuamini au kutomuamini kwako Malecela, hakumpunguzii wala kuongeza anything, ila ni mawazo yako tu kama mimi nilivyo na yangu, ila naomba nikuambie one thing kiongozi aliyepitwa na wakati ni waste of time hata kumzungumzia!
Kauli hiyo ya malecela ya kuita mazoea mabaya "utamaduni wa ccm" ndio sababu iliyonipeleka kuamini kwamba MALECELA HANA LOLOTE, NA HAKUNA JIPYA ATAKALOLIONGELEA HUKO BUSANDA. Kama malecela kweli ana "thubutu" na kama kweli ana busara ya kuweza kuonya, kwa nini asifanye kitu kimoja tu, cha kuwaambia akina JK wasifanye mikutano yao ya ccm ndani ya ikulu ? au hilo pia anashindwa ? ndipo hapo nilipofikia kusema kwamba malecela nae anakula ubwabwa na mafisadi!
- Mkuu CCM inao utamaduni kwa mfano rais lazima awe wa dini moja kubwa kwa kupokezana, hatuna sheria on it that lakini huo ni utamaduni wa CCM, na ni utamaduni wa dunia nzima, naomba unitajie nchi moja duniani ambako a sitting president alitolewa na mgombea wa chama chake?
- CCM ni chama tawala, na serikali ni ya CCM, sasa mkuu rais wa jamhuri anakuwa kazini 24 hours, kama kuna ishus muhimu za taifa ambazo zinamfanya asitoke Ikulu then hawezi kutoka Ikulu, na anything of serious importance politically ni lazima kimfuate Ikulu, kama Usalama wanamuambia hawezi kutoka Ikulu hawezi mkuu kuna sababu nyingi za kiutawala za kufanyika kwa baadhi ya vikao vya CCM CC Ikulu,
- Ya kula ubwabwa na mafisadi we all do that, kwa sababu in one way or another wananchi karibu wote wa Tanzania we are connected somehow somewhere, kama CCm na serikali yake ni fisadis, basi hata kupokea ruzuku ya CCM na serikali yake ni kuwa fisadi, Vodacom ni ya fisadi sasa ukitumia simu zake unakwua nini mkuu fisadi! kwa hiyo be careful na maneno kabla ya kuyarusha mkuu maana mengine yanatuhusu wote waananchiw Tanzania.
Kauli hiyo ya malecela kusema kwamba ni utamaduni kumuachia rais agombee bila kupingwa, ni tosha kumuharibia legacy yake kama kiongozi ( KAMA LEGACY YAKE NI NZURI, WHICH I DOUBT )!!
Haina haja ya kujua kuna wana-ccm wangapi huko Busanda, lakini iwapo kauli tata zitatolewa ( zimeshatolewa na malecela ) basi mimi kama kada sitosita kuzisema. Hapa kinachoongelewa ni maamuzi na kauli za viongozi na sio viongozi wao kama viongozi !!! Kwa nini unadhani malecela anaonewa ?
- Legacy anayeiandika ni wewe mkuu then itakua mbaya maana kwa nini anakubali mikutano ya CCM ifanyike Ikulu, lakini kama huandiki wewe itakua fair maana Malecela kama wengine ni bina-adam, halafu hakuna aliyekukataza kusema anything kuhusu Busanda wala Malecela ni haki yako, ila itabidi uheshimu na haki za wengine kukujibu, Malecela sio kiongozi ni mstaafu kwa hiyo rekebisha hiyo kauli, nani amesema Malecela anaonewa hapa? Wewe unaweza kumuonea Malecela? Hapa tunajadili siasa ya taifa ambayo mmeamua kuigeuza Malecela, sasa tuendelee kujadili mkuu hakuna noma! Haya maneno maneno ni ya kufurahishana tu hapa JF lakini bajaji haiwezi kumsaidia anything mwananchi wa Busanda, Zitto bingwa hoja na kejeli alikimbia hapa bila kuaga leo eti ana nguvu ya kusiaidia Chadema kushidna ubunge, that is inredible! Inaonyesha tu Tanzania tulivyo na safari ndefu! Mimi ningekua Chadema ningeruhusu DK. Slaa tu kuzungumza kwa niaba ya chama, maana he is the only clean leader huko kwa maoni yangu!
Respect na sasa ni saa ya kulala kesho!, Otherwise I love it tutaendelea kesho mkuu!
FMES
Unashangaa zitto kuunga mkono suala la dowans ? kwani malecela hamuungi mkono jk ? je jk hana connection na RA ? Anayo ! Je malecela anajua uwepo wa connection ya JK na RA ? Anajua ! Je malecela anafahamu RA ni fisadi kama ulivyosema ? NDIO, sasa iwapo malecela anamuunga mkono JK ambaye ana connection na fisadi RA, judgement/reasoning ya malecela ipo vipi unadhani ?? NIKISEMA MALECELA ANAKULA UBWABWA NA MAFISADI UTAKATAA ? There are things you simply cant dispute, na hapo hata hatujaingia kwenye rekodi yake mzazi !
Kazi na Dawa !
Mambo ya aibu sana....mzee kama yule 75yrs anaiba! keshafikia kikomo aliyofanya kwa taifa tunamshukuru sasa kuanza kuwaibia haki wananchi na uzee huu haipendeziMzee kapelekwa huko kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi ya kuiba kura za wananchi. Siwaonei haya watu kama hawa.
Katika uchaguzi wa 1995, ilibidi Mwenyekiti wa CCM wa wakati ule aibe mwenyewe kura. Sote tunajua alibadilisha matokeo ya uchaguzi Zanzibar (ambako CUF walikuwa wameshinda) na kwenye baadhi ya sehemu bara (ili kumnyima Mrema ushindi).
Ilipofika uchaguzi wa 2000, Mzee aliombwa asimamiye yeye uchaguzi kwa upande wa CCM. Alianza kwa kuwaasa vijana wa CCM wapigane na wapinzani kama ikibidi. Wale wasio na kumbukumbu fupi watakumbuka hayo.
Kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wana CCM dhidi ya ushindi wa Dr. Slaa Karatu iliwafungua Watanzania macho kuhusu jinsi CCM inavyodharau kura zao. Ulitolewa ushahidi wa wazi mahakamani jinsi viongozi wa CCM walivyojaribu kubadili matokeo ya uchaguzi katika sehemu mbali mbali. Yote hayo yaliwekwa hapa JF na tumeyaona.
CCM watajaribu kuiba kura Busanda. Hiyo ni kawaida yao. Wamemtuma Malechela kwa vile ana uzoefu mkubwa kwenye kazi hiyo.
It is also my thesis that CCM is delaying the issuance of national identity cards for the simple reason proper identification could interfere with their usual methods of rigging elections. Prove me wrong if you can.
- Zitto analia eti kwa nini Malecela anafanya vikao vya siri, ebo yeye vile vikao vyake vya Dowans havikuwa vya siri? Yaaani sasa Asha mnataka kutupangia CCM wapi pa kufanyia vikao na saa? Sasa kufanya mikutano ya siri ni unafiki? au lazima Malecela awe na mawazo kama yako na Zitto aka Dowans, ndio hawi mnafiki? Zitto kama anajua hoja na matusi mbona alikimbia hapa JF? Asha Zitto ndiye atawawezesha kushinda Busanda? Kwa sababu anauliza kwa nini vikao vya CCM vinafanyika kwa siri? Wewe huoni mmeshashindwa tayari maana hata ameshaanza kulalamikia kuibiwa kura na hazijapigwa? Anaweka tayari njia ya kutokea, akishindwa aseme aliibiwa kura?
Na ninasema hivi Zitto zile dakika 15 za political fame zilishaisha, yeye sasa ni CCM the fact kwamba Chadema inaweza kumpeleka kwenye kampeni dhidi ya CCM ni dalili za Chadema kuishiwa mufilisi!, Chadema ninamuaminia DK. Slaa peke yake, wengine ni muflisi!
Mag3,
Hapana. Kingunge ni mzee zaidi ya Malecela. Ngoja aje hapa FMES atupe dataz.
1.
- Zitto na kufukuzwa bungeni it was wrong na aliyemfukuza ni Lowassa, co-owner wa Dowans, ambayo sasa Zitto anaitetea, does it make a sense kwako na the whole ishu ya ubunge wa Zitto na upinzani?