Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Hii sheria ndio inaliza watu wengi. Labda kwenye thread hii badala ya kuhangaika na RA tungetumia muda huu kuwaelemisha Watanzania wengine kwa faida yao ya baadaye. Nina uhakika RA ni safi kwenye hili maana watu wangeshamvaa zamani.
Kama mtu alizaliwa na mzazi mmoja ambaye hakuwa mtanzania wakati anazaliwa na kule kwao wanatambua mtoto kama huyo kuwa raia basi wewe una uraia wa nchi mbili na unaruhusiwa mpaka miaka 18. Baada ya hapo lazima uukane uraia wa hiyo nchi nyingine. Kwa mfano baba mwingereza na mama Mtanzania, kwa miaka mpaka 18 unakuwa na uraia wa nchi mbili, baada ya hapo kwasababu Tanzania haitambui uraia wa nchi mbili, inabidi uukane uraia wa UK ili ubaki kuwa Mtanzania.
Kundi lingine la kuangalia ni lile la Watanzania wanaoishi nje ya nchi kihalali ambako mtoto akizaliwa anakuwa raia pia. Hata kama hamjaomba huo uraia, kwasababu huyo mtoto anakuwa atomatically ni raia basi baada ya miaka 18 lazima aukane uraia wa nchi nyingine, vinginevyo siku anaingia siasa, wajanja watakuwa wanamsubiri.
Hiyo sheria wala hata sio lazima uchukue gamba, inatosha tu kwamba kwa sheria za nchi husika mtu kama huyo anakuwa raia.
Huko mbele tusipobadilisha sheria kuna Watanzania wengi waliozaliwa na wazazi wote Watanzania watakumbwa na sheria hii na kuleta matatizo hasa pale watakapojihusisha na siasa.
Wanasheria tuelemisheni ili watu wajifunze na wasifanye makosa hayo hayo hata siku za mbele.
Kuna watanzania wengi sio wafuatiliaji wa sheria na wanajikuta hata hawajui nini kinaendelea. Kwa mfano kuna Watanzania wengi ambao walikuwa wanasoma UK na kupata watoto kabla ya mwaka 1983, baada ya muda kurudi nyumbani. watoto wao wamehangaika kutafuta visa za kuja Ulaya bila kujua wao automatically ni raia wa UK hata kama wazazi wao wahakuwa raia. Baadhi yao mpaka wanashutuliwa na ubalozi ndio wanajua kumbe ni raia. Kwa wale ambao wamepoteza hata vyeti ndio imetoka tena.
naomba wengine mnaojua ongezeeni.
Sheria hiyo inambana tuu kama amezaliwa on a third country ambayo siyo ya baba wala mama.sheria inambana huyo bwana, kama mama na baba ni watu wa kutoka nchi tofauti basi ukufika 18 lazima uchague uraia wa baba, mama au wa kuzaliwa, hapa namaanisha kama baba na mama wanatoka nchi tofauti na ulizaliwa kwenye nchi ambayo sio ya baba wala mama yako
Bahati mbaya sijaifuatilia kesi ya premji, tatizo linawezekana japo anahaki zote za Utanzania, hawa wenzetu wamekuwa na passport mbilimbli.Pasco,
Hapo juu ni kama hauko sahihi, refer case ya Premji kule Kigoma.
Pasco,Bahati mbaya sijaifuatilia kesi ya premji, tatizo linawezekana japo anahaki zote za Utanzania, hawa wenzetu wamekuwa na passport mbilimbli.
narudi tena kwa Mtikila na uraia wa RA, jamaa kasema anapasport mbili. ya tanzania huitumia mpaka Nairobi tuu, baada ya hapo, ni passport ya Persia. RA hakumshitaki wala ina maana kuna ka uwezekano wa kwa ukweli, unless RA aliamua kumpuuza Mtikila na sensitive issue ya urais lakini ametoa statement alipoitwa 'fisadi papa' labda kwa vile yule ni Mtikila na huyu ni Mengi.
huyo ni Mtikila, anaonekanaga kichekesho,punguani, kichaa, hamzazo bud sometimes there is some truths in between the lines. kwanini RA hakukanusha sensetive issue kama hii, leo katoa statement kukanusha 'fisadi papa'.Pasco,
Wewe ni RA, una mabilioni bank uliyopata kwasababu ya Utanzania, unapata visa kirahisi kokote unakotaka kwenda, ni mbunge, kweli uta risk kuwa na passport mbili?
Arguments zingine ni vichekesho, passport mbili zinatufaa sisi walalahoi ambao ukiomba visa ya kwenda nchi nyingine ni matatizo tupu.
Kama ni flawed reasoning ina maana kuna strong reasoning, unaonaje mwenzetu ungetuambia hiyo ni ipi?this is flawed reasoning.. kwa vile hawajamvaa ina maana ni safi?
Bahati mbaya sijaifuatilia kesi ya premji, tatizo linawezekana japo anahaki zote za Utanzania, hawa wenzetu wamekuwa na passport mbilimbli.
narudi tena kwa Mtikila na uraia wa RA, jamaa kasema anapasport mbili. ya tanzania huitumia mpaka Nairobi tuu, baada ya hapo, ni passport ya Persia. RA hakumshitaki wala ina maana kuna ka uwezekano wa kwa ukweli, unless RA aliamua kumpuuza Mtikila na sensitive issue ya urais lakini ametoa statement alipoitwa 'fisadi papa' labda kwa vile yule ni Mtikila na huyu ni Mengi.
Jasusi,Mtanzania,
Hii ya RA kuwa na passport mbili usibishe. Inawezekana kabisa. Najua kuna waziri katika serikali ya sasa ya JK ambaye ana pasipoti mbili. Usiniulize ni nani.
Mtanzania,
Hii ya RA kuwa na passport mbili usibishe. Inawezekana kabisa. Najua kuna waziri katika serikali ya sasa ya JK ambaye ana pasipoti mbili. Usiniulize ni nani.
Mkuu Kipunguni,Mzee Jasusi, si useme tu mwenye pasi mbili ni waziri kijana!
Mkuu Kipunguni,
Unafikiri Masha ni mjinga kiasi hicho? Atakuwa alishaitupa hiyo passport siku nyingi?
Kuwafunga kamba watu kama hawa lazima Watanzania tuanze kufikiri mbali zaidi ya maneno ya kijuweni ambayo hayawapi shida hawa mafisadi.
Unajua ukimwambia mtu ana hili wakati hana unakuwa umemwondolea matatizo kibao.
Ukiweza kuonyesha mtu ana passport mbili kwa TZ atapoteza ubunge na uwaziri hapo hapo. Kama tunapigana na ufisadi kwanini tunashindwa mambo hata rahisi kama haya kama tuna ushahidi?
Kwani hujui kwamba DIKTETA ni mmoja wa wale uv-ccm waliotoa lile tamko majuzi.alizaliwa mwaka gani? inaonekana unajua mengi..
Mkuu punguza jazba kidogo, kisha angalia historia ya hawa mafisadi na namna wanavyofanya ufisadi wao...kisha njoo hapa utuambie kama sio wajinga wa kupindukia.
Nakubaliana na wewe kuwa kuthibitisha kuwa fisadi ana pasipoti ya nchi nyingine ni kesi nyepesi na tena ya moja kwa moja...ila unasahau kuwa kwa sababu ni issue nyepesi kuthibitisha na kumtoa mtu madarakani basi haiondoi uwezekano wa kuwa kweli. Wewe umekaa chini ukafikiria hilo la uraia wenzio hawa mafisadi usiku na mchana wanafikiria namna ya kupeleka fedha zetu ulaya na america hawana muda wa kufikiria suala kama la pasipoti na uraia.
Angalia jinsi ufisadi wote unaojulikana jinsi ulivyokuwa rahisi kugundua kuwa hawa jamaa ni wezi, kuanzia Richmond, Kagoda, NSSF, EPA n.k ufisadi wote hakuna hata mmoja ambao umeenda shule...kote wameacha paper trail, namba za simu, address zinazofanana, majina yale yale, matumizi yale yale ya pesa...mpaka wengine wakafungua kampuni wakiwa ikulu na kuweka mke na watoto kama share holders...bado unaona hawa watu ma-genious mkuu...it's just a matter of time.
Kweli yanaweza kuwa rahisi na mtu ukiangalia kwa juu juu unaweza kuona ni kitu cha kuchukuliwa hatua mara moja.
Nikukumbushe kesi ya Mh. Chitalilo. Watu walilalamika kwamba amegushi elimu yake ya sekondari. Swala likaenda Polisi, Polisi wakafanya kazi na wakathibitisha kwamba tuhuma ni za kweli, na report ikaenda kwa DPP. DPP akasema Chitalilo hana kesi ya kujibu.
Kabla ya hapo JK alishaenda jimboni kwa Chitalilo akasema kelele za mlango hazimnyimi usingizi mwenye nyumba. Na Chitalilo mwenyewe alisema hata watu wapige kelele kiasi gani, hakuna chochote atakachofanywa.
Sasa jiulize DPP alitumia vigezo gani kusema kwamba Chitalilo hana kesi? DPP alisema kwamba kuwadanganya wananchi siyo kosa kwa kuwa kuna wagombea wengi huwa wanatoa ahadi hewa. Hivi kweli unaweza kulinganisha ahadi hewa na udanganyifu uliofanywa kwenye fomu iliyosainiwa mbele ya Hakimu kwa kiapo? Je, mtu akila kiapo cha uongo hana kesi ya kujibu? Nilitarajia kwamba condition ya kusaini fomu mbele ya Hakimu ni kuongeza uzito kwamba ameidanganya mahakama na hivyo anakuwa na kesi ya kujibu. (Mimi siyo mwana sheria, japo hayo ni mawazo yangu)
Tatizo ni kwamba sheria za Tanzania zinaangalia sura za watu. Kama huyo mtu hatakiwi na system (serikali na CCM) basi ni kesi rahisi sana. Lakini kama system inamhitaji, siyo kitu rahisi. Maana hao unaowapelekea ushahidi ndiyo watakuwa wa kwanza kwenda kuharibu ushahidi kwenye source. Angalia kwenye hii link uone vichekesho Parliament of Tanzania
Kama mtu hakumaliza sekondari kwanini hiyo taarifa iwekwe huko? Ina maana mtu aki-disco pale UD atasema nilisoma mpaka Mlimani na sikumaliza? Something is wrong somewhere na nina uhakika maelezo yanayosema NOT COMPLETED yaliwekwa baada ya kuona Polisi wametoa report ambayo ilikuwa inaonyesha wazi kijana aligushi elimu. Jamaa mpaka leo bado anadunda na yuko mstari wa mbele kutetea mafisadi.