Uchaguzi ccm tawi la mum demokrasia yatoweka:

mwobho

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
808
Reaction score
352
Wana jf, hivi sasa katika chuo kikuu cha waislamu morogoro (mum) kuna kampeni zinaendelea za uchaguzi wa ccm katika ngazi mbalimbali za uongozi. lakini cha kushangaza ni kutozingatiwa kwa kanuni na taratibu za ccm katika uchaguzi huo.

Hali hii imejitokeza pale ambapo baadhi ya nafasi za ungozi kutogombewa kwa sababu eti wenye nafasi zao wapo mwaka wa pili kwahiyo nafasi zinazo gombewa ni zile ambazo zimeshikiliwa na viongozi wa mwaka wa tatu (WANAONDOKA), na zinagombewa kwa sababu wanamaliza. Nafasi ambazo hazigombewi ni; katibu mkuu wa tawi na katibu mwenezi, nafasi hizi zinashikiliwa na SHADHIRI JIRANI-KATIBU na MAJALA-katibu mwenezi.

Lakini nilipofanya mahojiano na mwenyekiti anayemaliza muda wake ndugu MALELA aliniambia kuwa katika kanuni za CCM kiongozi anatakiwa adumu katika nafasi yake kwa takribani miaka 5, na wao kama matawi maalum wanatumia katiba ya ccm iliyopo sasa hivyo hawana budi kuendesha uchaguzi wa kuziba mapengo katika nafasi zinazoshikiliwa na wanachuo wa mwaka wa 3.

Lakini chaajabu katika nafasi ya MWENYEKITI wa UVCCM tawi inayoshikiliwa na Bw. ATHUMANI anayesoma mwaka wa 2, inagombewa kama kawaida. nilipo hoji nikaambiwa kuwa mwenye nafasi hiyo ameandika barua ya kujiuzulu na baada ya kutolewa majina ya wagombea nikaliona jina lake lipo katika orodha ya wanaogombea nafasi ya UENYEKITI wa tawi.

MAswali yangu kwa NAPE NAUYE

1) Ni kwanini chama kikongwe kama hiki hakina hata RASIMU inayoongoza matawi ya vyuo vikuu kama ilivyo kwa CDM?
2} Ni kwanini demokrasia ya CCM vyuo vikuu inaendeshwa bila ya kanuni?
3) Hamuoni mnaandaa viongozi watakaokua hawajali misingi ya katiba ya chama chenu na hata ya nchi katika siku za usoni?
4) Je hakuna haja ya kusimamisha uchaguzi huu hadi nafasi zote za uongozi ziwekwe katika kinyang`anyiro?
5) Hamuoni kwamba mnatumia UDIKTETA katika kuwapata viongozi wa matawi ya ccm vyuo vikuu?

ANGALIZO
TAFADHALI UNAPOCHANGIA MADA HII, NAKUOMBA USIIHUSISHE NA MASWALA YA KIDINI, USIKICHAMBUE CHUO CHA MUM ILA CHAMBUA MADA YA DEMOKRASIA YA CCM VYUONI.
NAKUOMBENI SANA NDUGU ZANGU WACHANGIAJI FUATENI MAELEKEZO
.
 
Nani ana haja na MUM na uchaguzi wa CCM? Who cares after all? Tafunaneni tu mkitaka uaneni mmalizane tu. Kwetu sisi maisha yataendelea hata mkifia mbali. Inaniuma sana kuona watu ambao tunadhani upstairs kukosawa wanakuwa busy na CCM!
 
MUM hii iko wapi?nielezeni tafadhali na ni chuo cha namna gani? Unalalamika ccm halafu bado uko huko huko.
 
MUM hii iko wapi?nielezeni tafadhali na ni chuo cha namna gani? Unalalamika ccm halafu bado uko huko huko-stupid mind
ni chuo chao ccm kiko morogoro kinamilikiwa na BAKWATA
 
MUM hii iko wapi?nielezeni tafadhali na ni chuo cha namna gani? Unalalamika ccm halafu bado uko huko huko-stupid mind

Follow the instruction, make your contribution about the topic
 
Wana jf, hivi sasa katika chuo kikuu cha waislamu morogoro (mum) kuna kampeni zinaendelea za uchaguzi wa ccm katika ngazi mbalimbali za uongozi. lakini cha kushangaza ni kutozingatiwa kwa kanuni na taratibu za ccm katika uchaguzi huo.

Hali hii imejitokeza pale ambapo baadhi ya nafasi za ungozi kutogombewa kwa sababu eti wenye nafasi zao wapo mwaka wa pili kwahiyo nafasi zinazo gombewa ni zile ambazo zimeshikiliwa na viongozi wa mwaka wa tatu (WANAONDOKA), na zinagombewa kwa sababu wanamaliza. Nafasi ambazo hazigombewi ni; katibu mkuu wa tawi na katibu mwenezi, nafasi hizi zinashikiliwa na SHADHIRI JIRANI-KATIBU na MAJALA-katibu mwenezi.

Lakini nilipofanya mahojiano na mwenyekiti anayemaliza muda wake ndugu MALELA aliniambia kuwa katika kanuni za CCM kiongozi anatakiwa adumu katika nafasi yake kwa takribani miaka 5, na wao kama matawi maalum wanatumia katiba ya ccm iliyopo sasa hivyo hawana budi kuendesha uchaguzi wa kuziba mapengo katika nafasi zinazoshikiliwa na wanachuo wa mwaka wa 3.

Lakini chaajabu katika nafasi ya MWENYEKITI wa UVCCM tawi inayoshikiliwa na Bw. ATHUMANI anayesoma mwaka wa 2, inagombewa kama kawaida. nilipo hoji nikaambiwa kuwa mwenye nafasi hiyo ameandika barua ya kujiuzulu na baada ya kutolewa majina ya wagombea nikaliona jina lake lipo katika orodha ya wanaogombea nafasi ya UENYEKITI wa tawi.

MAswali yangu kwa NAPE NAUYE

1) Ni kwanini chama kikongwe kama hiki hakina hata RASIMU inayoongoza matawi ya vyuo vikuu kama ilivyo kwa CDM?
2} Ni kwanini demokrasia ya CCM vyuo vikuu inaendeshwa bila ya kanuni?
3) Hamuoni mnaandaa viongozi watakaokua hawajali misingi ya katiba ya chama chenu na hata ya nchi katika siku za usoni?
4) Je hakuna haja ya kusimamisha uchaguzi huu hadi nafasi zote za uongozi ziwekwe katika kinyang`anyiro?
5) Hamuoni kwamba mnatumia UDIKTETA katika kuwapata viongozi wa matawi ya ccm vyuo vikuu?

ANGALIZO
TAFADHALI UNAPOCHANGIA MADA HII, NAKUOMBA USIIHUSISHE NA MASWALA YA KIDINI, USIKICHAMBUE CHUO CHA MUM ILA CHAMBUA MADA YA DEMOKRASIA YA CCM VYUONI.
NAKUOMBENI SANA NDUGU ZANGU WACHANGIAJI FUATENI MAELEKEZO
.
Hivi CHADEMA wana Tawi hapo?CUF je?
 
Back
Top Bottom