Uchaguzi CHADEMA na hatima ya kiti cha mwenyekiti

Uchaguzi CHADEMA na hatima ya kiti cha mwenyekiti

Mbelajr2023

Member
Joined
Nov 23, 2022
Posts
54
Reaction score
115
Habarini wana jukwaa wa JF.

Ni wiki chache sasa Zimebaki CHADEMA waingie katika UCHAGUZI wa viongozi wao wakuu wa chama.Hii ndio tafakuri yangu.

1)Lissu anaungwa mkono na idadi kubwa ya wanachama pamoja na wengine wasio wanachama,je hii inaweza kumfanya apate ushindi katika UCHAGUZI?

2)Mbowe ndio MWENYEKITI kwa Sasa na anatetea nafasi yake KWA zaidi ya miaka 20,je ataweza kukubali kushindwa UCHAGUZI na kumuachia Lissu?

3)Lissu na Mbowe wamegeuka mahasimu wa kisiasa ghafla,hii inatokana na nini hasa? Maneno yao na matendo yao yanadhihirisha jambo hili.

4)Mbowe anaungwa mkono na tabaka la juu(inner circle) la ndani na nje ya chama chake(rejea sakata la wenje na Abdul),je hii haiwezi kuwa ni kura ya turufu ya ushindi kwake?

5)Lissu hakubaliki na Mbowe pamoja na watawala,je Lissu amejipanga vipi kuzikabili ngome hizi? Au ndio anategemea nguvu ya umma tu?

6)Baada ya UCHAGUZI kuisha KWA vyovyote vile nini kinakwenda kutokea? Au ndio panya atamfunga paka kengele?

Hitimisho!

Katika mantiki ya siasa zetu Africa ni muujiza pekee wa nguvu ya umma unaweza kumpa Lissu ushindi,nje ya hapo Mbowe anakwenda kutangazwa mshindi mchana kweupe.

Kama ndiye aliyechaguliwa na yeye basi ni yeye.Wakati utatuambia.
 
Ukweli mchungu ni kwamba chadema ni mali ya familia ya Mbowe.

Ndiyo maana Mbowe hana ajenda wala sera zaidi ya kujigamba na kumdhihaki Lisu kuwa ni mbangaizaji.
 
Tuendelee tu kubaki CCM, hivi Vyama vingine hivi hakuna tofauti na MACHINGA WA MBAGALA. 🤒🤒
 
Back
Top Bottom