Uchaguzi CHADEMA ni litote lizame, liwalo na liwe.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwavyovyote vile chadema kuna upande hauna nia njema na chama. Wana uhakika kwa asilimia 100 kuwa chadema itapungua nguvu kuelekea October 2025 wakati wa uchaguzi mkuu. Pamoja na kulijua hilo bado kuna mtu anasema liwalo na liwe nitagombea.

Ili kuepusha mpasuko Chadema inahitaji hekima na busara za Nabii Suleiman alizotumia kuamulia ugomvi wa akinamama wawili waliokuwa akigombania mtoto kila mama akidai kuwa mtoto wake. Mgombea ambae ana nia mbaya na chama lazima atalazimisha kugombea no matter what na hatayakubali matokeo hata kidogo, lakini mgombea ambae ana nia njema na chama atakuwa radhi kujitoa au kukubali matokeo kwa namna yatakavyojitokeza na kuvunja makundi na kumuunga mkono aliyeshinda.

Utamjuaje mgombea mwenye nia mbaya na chadema?
1. Anazidisha mpasuko kwa kutukana au kubesa au kutoa siri za chama na vikao hadharani.
2. Anaungwa mkono wa watu wa chama tawala. Yaani fisi anamsaidia swala kupambana na mbwambitu.
3. Hataki suluhu
 
Wanapambana kugawana mbao za jahazi lao ambalo limewabeba.
 
CHADEMA imepita mapito na mitihani migumu sana, ni matumaini yetu CHADEMA itavuka salama katika hili.
 
mapito haya ndiyo waliyopitia NCCR na CUP, je wako salama? Kama ningekuwa wanaomba ushauri wangu, ningewashauri waahirishe uchaguzi wao hadi uchaguzi mkuu wa taifa. Yaani mwaka wa uchaguzi wa chadema upishane na mwaka wa uchaguzi mkuu. Hawatavuka salama kwakuwa kuna watu hawapendi uvuke salama.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa. CHADEMA katika hili itavuka salama salimini ninajua na kutambua hilo
Mark my words.
 
Lissu anasahau kuwa wananchi hawako tayari kukifia chama kwa sababu:
1. Manufaa ya yanayopatikana yanageuka mali binafsi za viongozi, wabunge, madiwani. Wabunge wananunua V8, wanajenga majumba na mahoteli kwa kutumia jasho za wafuasi.
2. Viongozi wa upinzani wananunuliwa na kwenda CCM kuunga juhudi kwa maslahi yao bila kuchukuliwa hatua na chama.
3. Wapinzani hawana sera mbadala
4. Viongozi wa vyama wanatoroka nchi mambo yanapokwenda mrama wakati wafuasi wao wakisiginwa.
5. Baadhi ya viongozi hawana familia zao hapa nchini, wako salama huko ng'ambo.
6. Hela ya ruzuku haijawahi kusaidia kununua hata kaptula moja ya yatima wala kuchimba kisima hata kimoja kwenye jamii.

Mbowe alifungwa na Lissu alipigwa risasi lakini sikuona aliyeandamana kupinga hayo. Wanajua ni kwanini? Je, chama kinamsaidiaje mwanachama aliyeumizwa kwenye maandamano? wana sera gani juu ya familia ya mwananchi aliyepoteza maisha wakati akihangaikia kura za chama?
 
Jamani serikali ifute ruzuku kwa vyama VYOTE vya siasa ni kuharibu Kodi zetu kwa faida za wachache . Aibu !
 
hakiyanani!!!, heri ruzuku ielekezwe kwenye kusambaza maji vijijini.
 
Wakiruhusu mgombea binafsi hizo tambo za vicheche zitapungua.
Hawataki kabisa kusikia mgombea binafsi.
Utilili wa vyama vimetengeza wanaojiona ni bora kuliko wananchi wa kawaida.
Ikimpendeza Mama Samia ruhusu wagombea binafsi.
 
Kama tunataka DEMOKRASIA ya KWELI tusiogope sijui Chama siju nini kama tunataka Nchi ambayo ni RUSHWA FREE tusimuogope mla RUSHWA yeyote.

Ogopeni kupasuka kwa NCHI na sio kupasuka kwa Chama.

Twendeni na LISSU na HECHE.
 
Back
Top Bottom