Pre GE2025 UCHAGUZI CHADEMA: WanaCHADEMA unganeni kumtetea Mwenyekiti wenu Mbowe asidhalilishwe, Lissu anavuka Mipaka

Pre GE2025 UCHAGUZI CHADEMA: WanaCHADEMA unganeni kumtetea Mwenyekiti wenu Mbowe asidhalilishwe, Lissu anavuka Mipaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Liwalo na liwe this is too Much!Nikiri mimi ni Shabiki wa Lissu lakini anapoelekea hapana,kama anahama CHADEMA ahame tu namtakia Safari njema asituharibie Taasisi,sisi tutabaki Mashabiki wa CHADEMA hadi mwisho.

Hakuna asiyefahamu Mchango wa Mbowe kwenye Siasa za Upinzani Tanzania kama yupo atueleze kama kuna Mwanasiasa wa Upinzani kafanya Mikutano mingi ya kuamsha Watanzania kuliko Mbowe, ajitokeze mtu atuambie kama kuna Kiongozi yoyote wa Upinzani katengeneza Viongozi wa kisiasa wa Upinzani kuliko Mbowe,vilevile ajitokeze mtu aseme kama kuna Mtu mwingine kajenga Taasisi ya Upinzani imara kuliko Mbowe katika nchi hii.

Hakuna asiyefahamu madhara aliyopata Mbowe katika kupambania mabadiliko hapa Tanzania,Mzee wa watu kadhalilishwa mara nyingi,kafungwa mara nyingi,kaharibiwa Mali zake na mengine mengi katika kujenga Upinzani.

Wote tunafahamu Mbowe kaitikisa Dola kwelikweli na kahujumiwa kwa kiasi kikubwa na Dola watu wake wameumizwa, wameteswa wamefilisiwa, wamefungwa, wamenunuliwa,wameuwawa, Wagombea wameenguliwa, Uchaguzi umeharibiwa nk, yote hayo ni hofu ya Upinzani alioujenga Mbowe otherwise CHADEMA ingekuwa mbali sana.

Nikikumbuka Mzee wa watu anaandamana peke yake na Familia yake anakamatwa na Polisi pale Magomeni hawa wapiga kelele wote hawapo najiuliza Maswali mengi sana juu ya neno Siasa.

Lissu anapata wapi ujasiri wa kumkosea heshima kiasi hiki,kumdhalilisha, kumkashifu na vitu visivyo na ushahidi kwa kigezo tu cha Demokrasia ya kutaka Uenyekiti halafu wanaCHADEMA mnaangalia tu as if hamtambui heshima na Mchango wa Mbowe katika Taasisi yenu?

Amkeni mteteeni Mwenyekiti wenu na mumuonyeshe kwa Vitendo Lissu kuwa Mbowe hata kama anaondolewa kwenye Uenyekiti siyo mtu wa kudhalilishwa ifanyike Kampeni safi aondoke sawa ila heshima yake ilindwe kafanya kazi kubwa sana kwenye Taasisi yenu.

Ni mtazamo tu Masela msijenge Chuki,Povu Ruksa
 
We nawe unachofanya ni too much...nani asome huu upupu mrefu hivi? Ni yeye TAML
 
Back
Top Bottom