Safari Ni Mtaalam na asiekubali kuyumbishwa. Akina hamad rashid na wengine hawakumfanyia Uadilifu Prof Safari. Moja ya Sababu ya Prof. Safari kutolewa Chuo cha Diplomasia ni kuwa alikwenda kumhoji prof. Lipumba akiwa Jela. Wakuu wa nchi wakajua jamaa ni CUF, wakamtoa DIPLOMASIA.
Suala la kuandika kitabu ni fani yake, acha aweke wazi Uozo uliopo CUF may be wanaweza kubadilika, msimamo wake wa kimsingi kuwa tofauti yake na akina Seif na Lipumba ni juu ya kusisitiza kuwepo kwa katiba Huru na hilo ndio msimamo wa wadau wengi ambao wanapenda kuona nchi inabadilika. Uelewa wa wajumbe nalo ni Muhimu sana.
Moja ya tatizo la Upinzani ni kukosa wasomi wengi, na wasomi wetu wengi wamekuwa waoga na wengi wao wanaona bora kubakia CCM kulinda maslahi yao. Kuliko Ku-risk maisha yao.
Nimjuavyo hawezi ingia CCM...!!!
Profesa Safari kutunga kitabu cha uozo CUF baada ya kupata kura sita
Na Elias Msuya
Siku chache baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kufanya uchaguzi mkuu na kuwarudisha madarakani viongozi waliokuwepo awali, mmoja wa wagombea walioshindwa, Profesa Abdallah Safari amesema anatunga kitabu kueleza hatma ya uanachama wake kwa chama hicho.
Katika uchaguzi huo, Profesa Safari aligombea nafasi ya mwenyekiti na kuambulia kura sita, akiwa nyuma ya mgombea mwingine Koplo John Masanja aliyepata kura 10, huku Profesa Ibrahim Lipumba akirejea madarakani kwa kupata kura 646.
Sikufurahishwa na uchaguzi ule kwa ujumla. Wamenidhalilisha sana kwa kuniuliza maswali ya kipuuzi na kusahau mchango wangu katika chama.
Mimi nilijitolea kama wakili kukitetea chama mpaka nikafukuzwa kazi katika chuo cha Diplomasia. Sikujali nikaendelea kukitetea chama changu. Ilifika mahali nikampoteza baba yangu mzazi nikiwa nakihangaikia chama, Halafu leo nakuja kuulizwa maswali ya kipuuzi vile? alihoji na kuongeza:
Siku ile nilikuwa na familia yangu, mke na watoto wangu, nao walihuzunika kuliko hata mimi.
Kwa hiyo sasa natunga kitabu changu ambacho kitaitwa Haja ya kuwa na Tume huru ya Uchaguzi. Humo nitaeleza kila kitu ikiwamo hatima ya uanachama wangu ndani ya CUF, alisema Profesa Safari.
Akielezea kwanini alishindwa kujibu swali lililomtaka amtaje jina la katibu wake wa tawi wakati wa kuomba kura, Profesa Safari alisema hilo nalo lilikuwa swali la kipuuzi kwakuwa yeye anachojua katibu wa tawi lake ni Mwanamke, hiyo inatosha.
Mimi ni mwanasheria, naelewa ninachokifanya, niliwaeleza kuwa katibu wangu ni Mwanamke hiyo inatosha. Sasa ya nini nimtaje jina? Hayo yalikuwa ni maswali ya kipuuuzi tu, alisema na kuendelea kutamba
Mimi nimetunga vitabu vingi vinavyotumiwa vyuo vikuu na sekondari, Muulize Lipumba ametunga kitabu gani,
Profesa Safari alisema kwamba kulikuwa na njama za muda mrefu ndani ya CUF za kummaliza kisiasa na ndiyo maana hata kauli za viongozi zilikuwa zikiashiria hivyo.
Viongozi walishasema kuwa hawawezi kumwachia nguruwe shamba la mihogo, hivyo ndiyo maana walifanya kila mbinu kuhakikisha kuwa sipati kura katika uchaguzi ule. Siyo kwamba sikuwa na Timu ya kampeni, nilikuwa na timu yangu na meneja wa kampeni alikuwepo lakini hujuma, alisema.
Akieleza tofauti iliyopo kati yake na viongozi wa juu wa chama cha CUF, Profesa Safari alisema kuwa ipo haja ya kuwa na tume huru ya uchaguzi ndani ya CUF.
Akieleza hatima ya uanachama wake wa CUF na kama yuko tayari kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) endapo atajitoa CUF, Profesa Safari alisema alisema kamwe hawezi kufanya hivyo.
Alidai kuwa mwaka 1995 nilipotoka Uingereza, CCM walimtaka ajiunge nao na wakamuahidi nafasi kubwa kama vile ukatibu mkuu katika Wizara ya Katiba na Sheria, jaji lakini alikataa.
Pamoja na kuonyesha wazi kuitupia virago CUF, alisema yuko njia panda kwa sababu hajaona chama chochote chenye mwelekeo mzuri kisiasa.
Alisema kuwa Tanzania bado hakuna vyama thabiti vinavyoendesha siasa za ukweli.
Ninatafakari mwelekeo wangu. Ni mapema mno kusema nitafanya nini baada ya hapo.....give me time (Nipe muda) nitaeleza nitakapozindua kitabu changu, alisema.
Kwa sasa naishi kwa kutegemea vitabu vyangu. Ndiyo mimi ni wakili lakini hasa nategemea vitabu vyangu alisema Profesa Safari.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Wilfred Lwakatare alikanusha madai ya Profesa Safari kudhalilishwa kwenye uchaguzi huo.
Chama chetu kinafuata taratibu na kanuni, na kwakweli, aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi ule alizingatia hilo. Maswali yote yaliyoulizwa yalikuwa sahihi kabisa na hakukuwa na swali la kumdhalilisha mtu, alisema Lwakatare.
Alifafanua: Tusema kwamfano mtu anaulizwa, Unamfahamu katibu wako wa tawi nay eye akashindwa kujibu, hilo ni swali la kumdhalilisha? alihoji Lwakatare
Alisema kuwa kama Profesa Safari anaona amedhalilishwa, ni vema angefuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye vikao halali
Alikanusha madai kwamba kitendo cha kuwarudisha viongozi wale wale waliokuwepo ni kinyume cha demokrasia.
Source: Gazeti la Mwananchi