Uchaguzi huu October 2015, Ni Mahakama ya Kadhi V/S CCM. (Tutaona nani Mshindi).

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,373
Naangalia TBC sasa hivi, Namuona Rais wa Nchi yetu akiongolea suala la kura kwa katiba Pendekezwa. Inaonekana Rais amelishwa maneno mengi ya Uongo kuhusu ukusunywaji wa Maoni ya Katiba hiyo.

Waislamu wote na Taasisi zake walitoa Maoni kuhusu Mahakama ya Kadhi, lakini Sio Jaji Joseph Warioba wala Kundi la Kina Endrew Chenge waliothamini maoni ya Waislamu hao.

Leo Rais ametuthibitishia kua Serekali haita anzisha Mahakama ya Kadhi wala haita igaramia. Jukumu hilo ni la Waislamu wenyewe.

Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe.

Huo ndio uliokua msimamo wa Serekali ya CCM tangu zamani, ila wanapo ona wamebanwa hukimbilia kwa Waislamu na Misikitini kama ilivyokua Uchaguzi wa 2010. Waislamu waliokua wanaswali Msikiti Kichangani ni Mashuhuda ya hili ninalo lisema. Pale Yule Sheikh Kijana Mweupe alipokua akisimama na ijumaa takribani tatu za Mwisho kabla ya Uchaguzi na kuwabadilsha Waislamu muelekeo. Kua tumchague mwenzetu. Je Sheikh Umemuona mwenzetu huyo na kundi lake?

Sheikh Jongo hili tulikwambia. Sasa umeyaona. Sasa tunasubiri yale uliyoyasema pale Msikiti wa Gadafi Dodoma.

Sasa Jukumu la Mahakama ya Kadhi lipo Mikononi mwa Waislamu wenyewe. Haya sasa Waislamu ni Mpambano kati ya Dunia na Akhera.

Kila nafsi itauonja Umauti.

Je tutaendelea kudanganywa na kutumika kama punda kubeba mizigo tusio jua thamani yake.

This October, tutumie kura zetu kwa Maslahi yetu lengo liwe kuwaadabisha walio tusaliti.

Kwa hiyo Mahakama ya Kadhi ni Chama siku hizi? Itapambana vipi na CCM?Sijaelewa heading yako mleta mada
 
Uwelewa wako huakuruhusu kuchangia hapa! Walengwa wa Mada hii wameshaelewa!
Hilo jina lako na unachoandika havina tofauti, huwezi kumkejeli Rais kiac hicho kwani sio mjomba yako yule, uwe na hekima na busara na uungwana.
 
Hongera Rais Kikwete kwa kuweka mambo bayana. Long live my President
 
Mbona mchokozi hivi MZIMU! Wewe kweli ni Mzimu, Maneno gani tena haya?

"Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe"

Acha ujinga wako. HAKIKA HUU NI UPOTOSHAJI NA NI UCHONGANISHI AMBAO MSINGI WAKE HAUNA NIA NJEMA KWA WATANZANIA NA NCHI YAO.

Jamani kama ni wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wazuri Rais Kikwete jana alizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema amesikitishwa na tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, linalowahamasisha waumini wao kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana.

Akifafanua suala la Mahakama ya Kadhi, Rais Kikwete alisema Serikali ina msimamo wa mambo mawili katika mahakama hiyo.

Kwanza, alisema Serikali haina mpango wa kuianzisha na kuiweka katika Katiba na pili, haihusiki kuiendesha na badala yake, Waislamu wenyewe ndio watakaoiendesha kama wataihitaji.

Kwa msingi huo wa sehemu ya haotuba ya Mhe. Rais jana ndiyo maana katika Katiba Inaypoendekezwa kuhusu masuala ya dini inasema “Uhuru wa imani ya dini Ibara ya 41. (2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi. Na (3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali”.

Asante Mhe. Rais kwa ufafanuzi huo maana humu JF watu wachache wanawahadaa wenzao kwa kuwa wanaweza kusema na kushawishi, WASOMAJI WA JF WATU WANAOTOA MAELEZO YA KUWAPOTOSHA WENGINE HAWANA NIA NJEMA NA NCHI YAO. TUJENGE NCHI YETU KWA MANUFAA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO USIJIFURAHISHE KWA KUANDIKA TU TAMBUA UNAWEZA KUANGAMIZA NA KUWAPOTOSHA AMBAO WANAAMINI BILA KUFANYA UTAFITI.
 
Hilo jina lako na unachoandika havina tofauti, huwezi kumkejeli Rais kiac hicho kwani sio mjomba yako yule, uwe na hekima na busara na uungwana.

Acha kujificha kwenye kivuli chako Juha wewe. Soma uwelewe nini kimeandikwa.
 
We dada. Sio watu wote ni wajinga kama wewe!
 
Wakati Nyaraka zinasambazwa Makanisani katika uchaguzi wa 2010, CCM walikimbilia Misikitini na kujinusuru. Na kweli hiyo karata imekua ikiwasaidia tangu zamani. Not any More. You will see. Mark My words. BAKWATA, haiwakilishi Waisalamu kabisa zaidi ya wale Masheikh bora liende nipate tonge Mdomoni.
 
We dada. Sio watu wote ni wajinga kama wewe!

Umezidi bwana! Ebo! Acha kutuchanganya na mambo yako yasiyo na msingi. Ujinga wako peleka huko hapa ni majadiliano yenye hoja natija kwa nchi yetu. Acha tabia zako tena kalale kama umechoka. Tena mjinga kabisa. Kweeeeeeendaaaaaa!
 
Mhhh! Hapo ndio Mwisho wako! Haya wapishe wenye kujua waje wajadili.
 
Mhhh! Hapo ndio Mwisho wako! Haya wapishe wenye kujua waje wajadili.

Inawezekana macho yako hayaoni tena vua miwani, mi humu nipo kuelimisha watanzania na wenye mapenzi mema na nchi yao na hatima ya Tanzania hasa kuhusu mambo ya kijamii.
 
Tunaitaka iyo mahakama lkn hamna atakayeenda bal watakula ela kwa hal ya sasa n mwanamke gan atakaye kubal kua chin ya mwanaume wanahitaj n mrad wa kupga ela uo
 
Tunaitaka iyo mahakama lkn hamna atakayeenda bal watakula ela kwa hal ya sasa n mwanamke gan atakaye kubal kua chin ya mwanaume wanahitaj n mrad wa kupga ela uo

Mhh! Haya na wewe hoja yako ni ipi?
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.
 
Kweli kabisa wala haeleweki nahc anaweza kuleta chuki baina ya watu.
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.

Mzimu anajitahidi kupotosha kweli. Labda anataka kuonekana mwema lakini ni sawa na kung'ata na kupuliza ambayo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Hongera KgHM kwa kuliona hilo.
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.

Acha unafiki waislamu wanaitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…