Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu tusimame vizuri

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Sitabiri ila ndio ukweli wabunge na madiwani mliopo katika majiji na wilaya zilizo changamka changamka jiandaeni kupokea na kukubali msichokipenda.

Jua liwake au mvua inyeshe kila Mtanzania atasimulia kwa mambo makuu yatakayojitokeza.

Uchaguzi 2020 utakuwa una mchuano mkali zaidi ya 2015.

Nimeona sehemu na najua kuna watu hawataamini mawazo yao na mipango yao ila ukweli ndio huo.

Wenye nchi wameamua kuja kuonyesha mfano namna bora ya kufanya kazi ili watu wajifunze kutokuishi kwa mazoea. Siasa ya mwaka huu ina nguvu sana maana kuna kundi la waliokaa pabaya dhidi ya waliosimama sehemu sio nzuri.

Karibu sana 2020.
 
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa na mchuano mkali ndani ya CCM na sio ndani ya vyama vingi.

MwanaCCM yoyote anajua katika Uchaguzi Mkuu ujao akipenya kwenye kura za maoni ndani ya chama anakuwa ni kama amemla ngombe na kubakiza mkia!
 
Bosi hii ngoma ya mchuano ni kwa vyama vyote mzee utaniambia na cream ikipatikana sasa huko ndani huku nje ndio kilio na kusaga meno.

Mr. Kijani anataka kuweka miti mizuri ipandwe Dodoma na kuenea nchi nzima aachane na mikopo ya miti 10 anayoitegemea sasa kumpa kivuli na kupunga upepo kwa kiasi si unaona joto la nchi kali.

Huku nje Mr. Kioo yeye anamchora tu kiaina namjua atafungulia ile stock ya hard workers iliomsaidia kujenga msingi wa kujimwamba Mr. & Mrs. Vioo wasio paper chasers ubaya Mr. Kijani kaharibu mtaani kila mzazi mwenye mti mchanga hamsemi vizuri kwa maana miti hiyo imeshindwa kutoa kivuli na matunda kwa wakati kwa kukosa maji bahari kuu, mito na maziwa.
 
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa na mchuano mkali ndani ya CCM na sio ndani ya vyama vingi.

MwanaCCM yoyote anajua katika Uchaguzi Mkuu ujao akipenya kwenye kura za maoni ndani ya chama anakuwa ni kama amemla ngombe na kubakiza mkia!

Ni kweli kabisa usemayo, na hili sio kwasababu ccm inakubalika sana, bali mwenyekiti wa ccm ndiye rais wa nchi. Na kwakuwa yeye ni rais, anaweza kutumia madaraka yake na udhaifu wa katiba na wake binafsi kuzuia ushindani wowote dhidi yake binafsi na chama chake.

Hivyo atatumia vibaya madaraka yake kuharibu uchaguzi kama ambavyo amekuwa akifanya toka alivyokuwa mbunge, kwani huko poa hakuwa na sifa ya kushinda kwa njia ya kura zaidi ya kushinda kwa mizengwe. Kwahiyo huo udhaifu wake binafsi wa kutokuweza ushindani, ndio kahamishia kwenye uchaguzi wa nzima kwa kuwa katiba inampa mwanya wa kufanya atakalo bila kuwa na hofu ya kushitakiwa.
 
Huyu jamaa alipona kweli? Au walimuua, CCM siipendi kumambegesa. Inchi ikipinduliwa hii Kuna watu watachomwa Moto mbele ya familia zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiandikishe kwanza upate sifa Boss baada ya hapo pata sasa nguvu za kuandika utakacho.

Ukiweza kutokujiandikisha wewe kuwa mpenzi msikilizaji tu na upende kunywa maji mengi sana, uache kusikiliza ya watu ujijali wewe kwanza.

Haahaa, hakuna asiyependa mawazo yake ila basi tu.
 
Hata kama hapigiwi kura wewe jua haya hakuna aliye juu ya sheria.

Hata muasisi alilijua hilo, hakupinga pale sheria ilipomsemesha mbona aliitikiwa wito kwa wakati.
 
Hata kama hapigiwi kura wewe jua haya hakuna aliye juu ya sheria.

Hata muasisi alilijua hilo, hakupinga pale sheria ilipomsemesha mbona aliitikiwa wito kwa wakati.

Kwa taarifa yako hilo neno kuwa hakuna aliye juu ya sheria ni danganya toto tu. Ukweli ni kuwa rais na genge lake wako juu ya sheria kwa uwazi au kwa kificho. Kama rais hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote akiwa madarakani au akiwa ametoka, hapo unaposema hakuna aliye juu ya sheria unamaanisha nini? Na kibaya zaidi kinga hiyo aliyo nayo rais na madaraka aliyo nayo, anaweza kutumia hiyo nafasi yake kumlinda mtu yoyote amtakaye na mkono wa sheria. Hilo liko wazi na mifano ya dhahiri ipo.
 
Katiba ipo wazi Boss amini nikuambiacho hakuna aliye juu ya sheria.
 
Katiba ipo wazi Boss amini nikuambiacho hakuna aliye juu ya sheria.

Nilichokuambia sijakuambia kwa bahati mbaya, katiba ya nchi yetu inatekelezwa kwa utashi wa rais aliye madarakani,na sababu hasa ya rais kuwa juu ya katiba na hizo sheria ni udhaifu wa kumfamya rais asiweze kushitakiwa akiwa madarakani au akiwa ametoka. Kitendo cha rais kuchagua kila Mkuu wa taasisi ya kimamlaka kunamfanya rais kuwa na nguvu kuliko hiyo katiba. Ndio maana rais anaweza kufanya lolote bila kujali katiba na sheria zinamruhusu na hawezi kufanywa lolote, maana yoyote atakayehoji anaweza kumtoa kwenye nafasi yake, au kuagiza atupwe jela.
 
Haahaa KATIBA ni dude kubwa hutaweza kuamini likigeuka kwa upande wa pili. Wewe una macho ya kuona upande mmoja kwa kuitazama KATIBA kama wengi waonavyo lakini siku watu wakiona upande wa pili, ndipo unatimia ule msemo wetu wa kiswahili kuwa "sheria ni msumeno wenye kukata kuwili"
 

Si mpaka iwe msumeno wa kukata pawili?
 
Si mpaka iwe msumeno wa kukata pawili?
Brother ukitaka kuamini kuwa KATIBA ni dude kubwa wewe waulize Mr. & Mrs. Kijani wanahabari gani 2020.

Kule KISIWANI moto waka moto kolea, huku BARA maji kuingia maji kujaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…