Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Wakati siasa zikiendelea hasa kuelekea uchaguzi wa October 28, kuna wagombea kutoka vyama fulani ninawafanisha ni Chifu Mangungo. Lakini nitaomba mnisamehe kwa kutumia jina hili ambalo ninaamini pamoja na mambo mengine linaiweka Tanzania kwenye ramani ya Dunia.
Labda niwakumbushe kidogo historia fupi ya Chifu Mangungo. Chifu Mangungo wa Usagara huko Msowero na Chifu Mbwela wa Wazigua walisaini mikataba ya ulaghai(bogus treaties) na Karl Peters kati ya mwaka 1884 ambayo ilimsaidia Peters kupata kibali maalum (Schutzbrief) cha kutambulisha kama milki ya wajerumani.
Ni ukweli ulio wazi kwamba Chifu Mangungo, na kwa kiongozi yeyote wa Kiafrika wasingekubali kuiachia ardhi yake na mamlaka yake kwa mgeni laghai kama Karl Peters. Lakini hawakujua kusoma wala kuandika na wakalimani walitumika kupindisha maana na kutoa tafsiri isiyosawa kwa manufaa ya wakoloni.
Kwa utambulisho mfupi wa Chifu Mangungo basi Historia inaonyesha wazi kuwa tangu zamani wakati wazee wetu Kama akina Mkwawa, Isike, Mirambo, Kinjekitile n.k wakiwa wanapambana kuondoa mfumo wa unyonyaji wa kibepari wapo Watanzania wengine walishiriki kuhujumu jitihada hizo kwa kujua au kuto kujua. Walifanya hivyo kwa kuhujumu jitihada za Watanzania WAZALENDO wakiamini Wazungu ni mwarobaini wa matatizo yao.
Safari hii kampeni zikiwa zimepamba moto wapo wagombea ambao akili na mawazo yao wanategemea kuwa wazungu ndio utakuwa mwarobaini Kwao kupata ushindi. Wao kila jambo linalotokea nchini basi ripoti Yao ya kwanza ni kwa Wazungu. Hawa ndio wakati mwingine unadhaniwa kuwa wameshaingia mikataba na hawa watu kuwa wakishinda na kushika dola basi kuna vitu wazungu hawa wataachiwa. Ni dhahiri kuwa wanachofanya hakitofautiani na alichokifanya Mangungo, tofauti ndogo iliyopo ni kuwa Mangungo alidanganyika kwa kuwa hakujua kusoma lakini hawa wa sasa wanajua wanachokifanya ila kwa kuwa wanahamu na madaraka Kwao ni bora wapate madaraka na wazungu waingie upya kutunyonya.
Ukisoma kitabu cha Mwalimu cha Azimio la Arusha aliandika kuwa Taifa haliwezi kujivuna kuwa lipo huru kama bado linategemea misaada kutoka nje. Na huu ndo ukweli.
Rais Magufuli tangu aingie madarakani anajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha walau tunafikia hatua ya kujitegemea. Ni ukweli kuwa yapo mambo makubwa ameyafanya kwa kutumia fedha za ndani bila kuomba nje, na mfano mzuri ni uchaguzi huu ambao unatumia zaidi ya bilioni mia tatu ni fedha zetu za ndani.
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawahi kufanya uchaguzi kwa fedha za ndani, ni mara ya kwanza. Hili tu haliwezi kuwafurahisha wale ambao walitegemea tutaenda kuwakopa au kuwaomba ili watupe mashariti magumu ya kuzilipa na watuamulie namna ya kufanya uchaguzi.
Baada ya kuona milango imefungwa wanajipenyeza kwa baadhi ya wanasiasa ili kuhakikisha wanapenyeza nguvu zao kwenye uchaguzi huu. Wanasiasa ambao hawataki kufikiria kesho ya Afrika na kesho ya Tanzania wanadhani wanapendwa kumbe mabepari haya Hana longest sight. Watanzania wanaofanya haya hawatofautiani na Chifu Mangungo. Ninamfananisha JPM na miamba ya Afrika hasa akina Mkwawa, Isike, Kinjekitile n.k kwa Tanzania, lakini ninawafanisha Wanasiasa wanaoshirikiana na Mabeberu kupandikiza chuki nchini ili wapate wanachokitafuta na Chifu Mangungo aliyeamua kuuza Aridhi kwa Carl Peters ili hali akijua kuna watu wanategemea Hii aridhi.
Uchaguzi huu ni vita kati ya watu wanaotaka kuturudisha enzi za utumwa dhidi ya wanaotaka kuendelea kulisimamia taifa na hatimaye kuwa taifa linalojitegemea kwa asilimia kubwa mbeleni kwani rasilimali kutufanya kujitegemea zipo. Kura kwa JPM.