Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Huu uchaguzi wa serikali za mitaa ni wa mauzauza sana jamani. Siku kadhaa zilizopita nilikuwa saluni akapita mjumbe wa mtaa wa Matawi, maeneo ya Skanska, akatusalimia pale na kuanza kuongelea mambo ya uchaguzi na kusema akidai kwamba chama kinawalinda watu wake na hakiwezi kukubali mtu wa nje.
Katika mchakato wa kuchukua fomu za wagombea, ni dhahiri kuwa watu wa nje ni wagombea wa chama pinzani, CHADEMA, na vyama vingine watawanyimwa fursa hiyo.
Awali, katika mtaa huohuo niliwahi kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wajumbe wanapita kutoa fedha kwa ajili ya kujiandikisha, huku wakidai hela zinatolewa kwa wanaojuana na wengine hawapewi.
Sasa najiuliza, ni kwa nini kuna wananchi wachache wanapewa fedha ili waende kujiandikisha, Uchaguzi huu utakuwa wa haki kweli au ndo tutapikwa kama kawaida?