Mkuu
Mag3 nimekusoma vizuri. Tasinia ya habari kwa kweli tuna matatizo makubwa sana. Shida ni kuwa taaluma hii imevamiwa na makanjanja wengi na ndio maana wajanja ndani ya taasisi za habari wanapinga sana ile Sheria ya Habari 2016 hasa kipengele cha kutambua wanahabari wawe na kiwango gani cha elimu.
Wakijaa wenye elimu ya Diploma na degree walaji ndani ya MCT, TAMWA, UTPC wanaotafuna fedha za wa Sweden, Denmark nk watazilaje? Wao wanawakusanya mfano vikundi vikundi Mara press clubs nk kisha kuwapatia ukoko wale wenyewe wakipiga mpunga wa kutosha kwa masharti ya kutoandika mambo yasiyo iumiza serikali na chama tawala.
Lakini umuhimu wa waandishi hauishii kwenye habari za uchaguzi pekee, hivyo tasnia hii ni muhimu tuijenge vyema ili hata Lissu naye akipata madaraka na kwenda kinyume aongozwe njia sahihi ya kufuata