Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu Waandishi hatujatimiza wajibu ipasavyo

Kwenye hili nawatetea waandishi wa habari.. niambieni nchi hii kwa sasa nani anainua mdomo wake au kalamu yake kuandika tofauti na watawala wanataka? si maprof wala wanaojiita wananzuoni sijui... amebaki mtu mmoja tu antipas basi. wengine wote ...kimyaa
 
Tuseme ukweli unaomumiza.
👇
Kwa kipindi hiki hakuna mwanahabari anayeitendea haki taaluma ya habari, kila mtu ana hofu na maisha yake, hakuna mhariri anayekubali mkate wake utiwe sfongo kisa kutoa habari yenye kuonya serikali hakuna.

Wakati huu meza ya mhariri inapokea habari za kijamii kama ni za serikali basi siyo za kuumiza is just like soft story as "Mh. hgfzib azindua transfoma kijijini kwao".

Mtwara hakuna mwanahabari yeyote anaweza kwenda kuja na habari ya huko hata huyu anayejiita Pascal Mayalla hawezi kwenda kufanya investigation story akaja kuandika hapa, hata yeye anaogopa mkono wa serikali na maisha yake, kwa nini anatoa hiyo habari.

Makubi hatoi habari ngumu hata kidogo bali anaanglia angle ipi atoke nayo si kwamba hajui anajua vizuri kupata mkate wake wa siku na hakuna mwandishi anayependa kuharibu maisha yake kisa 'eti atoe habari ngumu ya kuinanga serikali mh!'.

Kwa sasa kila mwanahabari ana mawazo yake juu ya 28.10.2020 amchague nani ili aje kuwa huru kuhoji au kuandika habari yoyote pasipo hofu ya kuzushiwa wizi, kulipa kodi, kutaifisha pesa, kufungwa au kuokotwa kwenye kiroba nk.


NB. Mwishoo wa siku tusiwalaumu tu waandishi tasnia nyingi zipo dhohofu kwa hofu.
 
Ni kweli waandishi na vyombo vya habari mwaka huu vimeboa sana! Hata hivyo mimi binafsi siwezi kuwalaumu sana kwa vile sababu zipo wazi!
CCM ndio chanzo cha hayo yote! Kwanza serikali yake imepambana sana vyombo vya habari vilivyoonekana kuandika habari za upinzani au habari zisizoifurahisha serikali au CCM!
Sheria mbovu na kandamizi zinazotungwa kuhusu vyombo vya habari, zinaonekana kuvihusu zaidi vyombo vya habari vya upinzani ila sio CCM!
Kuna vimagazeti vinaweza kuandika chochote na kwa namna yoyote lakini hakuna hatua zinazochukliwa!
Tumeshuhudia mtu yoyote mwenye wadhifa katika wizara ya habari anaweza kukifungia au kufuta leseni ya chombo cha habari, kisa ni cha upinzani wakati sheria zinaelekeza chombo cha habari kikikosea kipelekwe mahakamani ili sheria ndio ikaamue kosa!
Lakini ukichunguza kwa umakini, ukalinganisha na kinachoendelea sasa , utagundua kuwa kulikuwa na mkakati kuhakikisha vyombo hivyo vya habari vya upinzani havifiki mwaka wa uchaguzi mkuu!
Kwa hiyo mazingira waliyo nayo wanahabari na vyombo vya habari hivi sasa yamejengwa na serikali ya CCM, Hivyo uhuru kamili wa habari na vyombo vya habari utapatikana tu pale tukiiondoa CCM madarakani!
Wana habari mna nguvu na uwezo mkubwa wa kulifanikisha hili kwa kuelimisha wote ambao hawaioni dosari hii!
 
Watanzania ufundi wetu ni wa kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Si waandishi, si viongozi wa dini, si viongozi wengi wa vyama vya siasa, si maprofessor. Huko taasisi za umma ndio husemi, private sector ndio nao wame athirika. Huko nyuma tulikuwa na tabia hizi lakini hii awamu ya tano imevunja rekodi. Hatuwezi kuhoji, tunaogopa. Mitano Tena sioni matumaini ya mabadiliko kwani katiba sio kipaumbele chao. Mitano kwanza-ameongelea kuhusu Uhuru, HAKI, maendeleo na amani na kusisitiza kuleta mfumo mpya wa utawala wa sheria na serikali.
Kila mmoja wetu aamue kuendelea kufunika kombe au kulifunua tupate Tanzania mpya. Binafsi kura yangu itaenda kwa Jasiri Lissu, CDM na ACT.
 
Yaani Lissu akishaingia Ikulu tu yule mwandishi apewe wizara ya habari au kurugenzi ya TBC!
Huko Mbali, aanzie hukohuko Mwanza awe kiongozi wa wenzake na kumtoa tapeli mmoja ambaye kiasili sio mwandishi maana hana historia ya uandishi bali ni opportunistic ndani ya tasinia ya habari.
Yeye kila kwenye fursa lazima ajiingize kwa uongo uongo ili apige mpunga, anaitwa Edwin Shako.
Ila siku wanahabari wa Mwanza wakishtuka ndio watakapojiona kumbe wamefanywa ignorants kwa muda mrefu sana.
After general election nitakuwa Mwanza nadhani nitapata dosier ya huyo bwana na nitatiririka hapa ili turudishe heshima ya wanahabari kutokea mikononi mwa matapeli wanaofanya inaonekana ya hovyo.
 
Sorry nimesahihishwa hapa News room kuwa anaitwa EDWIN SOKO. na ni mwenyekiti wa Press club na taasisi moja amejiundia eti ya kupambana na madawa ya kulevya.
Utakatishaji mtupu!
 
Je, wana habari hali hii ya kushindwa kutoa huduma yetu wakati muhimu kama huu wa uchaguzi twaionaje?
Kwani wewe ulitaka wanahabari mfanye jambo gani labda kiasi kwamba ungeona mmefanya kazi ya kutukuka?
Wewe binafsi umefanya lipi la maana ambalo unaweza kujisifu kuwa ni shujaa?
 
Kama kuna 'Jambo' huwa si tu 'linaniumiza' bali pia 'linanikera' Kulisikia ni pale 'Watanzania' wanapodhani Tanzania ya sasa ina 'Journalists' mahiri.
Huu ndiyo ukweli wenyewe hatuna journalists wala vyombo vya habari tuna magenge ya wahuni tu.
 

Uhuru wa waandishi wa habari utarudi magufuli akiondoka madarakani. Sasa hivi ni Aidha usifie, au ujifanye unafanya kazi ufunguwe, ama ukaishi na Azory Gwanda.
 
Tanzania sahv hakuna waandishi mahiri wa habari
Ndomana wote wamehamia kwenye habari za umbeaaa....

Ova
 
Na hao makanjanja ndiyo wame take over

Ova
 
Kwani wewe ulitaka wanahabari mfanye jambo gani labda kiasi kwamba ungeona mmefanya kazi ya kutukuka?
Wewe binafsi umefanya lipi la maana ambalo unaweza kujisifu kuwa ni shujaa?
Mwandishi ana kanuni zake za kazi anapaswa kuzifata bila woga. Balancing story.
Kwa nini waandishi wakongwe kama Ulimwengu na wengine wanatukuka? Ni kwa kusema kweli bila woga, lakini nirudi palepale kuwa uongozi wa vyama vya waandishi waweza kuwa chachu ya kutepeta na kujenga woga kwa waandishi kwa vile sio imara ila wengi wapo kupiga fedha zitolewazo na SIDA, NORAD nk basi bila kujenga uwezo wa watu wao zaidi ya visemina mbuzi
 
Waandishi wamekuwa vibaraka wa magufuli mwaka huu.
 
Huwezi kuwalaumu waandishi wa habari maana hii awamu imewaminya mno.
 
Hakika miaka hi mitano imetufundisha mengi sana hatutaisahau kamwe,waandishi wote mfukoni mwa mtu mmoja kimya walibaki kuabudu na kutoa makaripio kwa CDM tu baada ya kuwafukuza wale jamaa wa tbc naogopa kuandika kwa herufi kubwa maana nitakuwa nimewapa sifa isiyowasitahili.
 
Hivi yule mwandishi wa ITV anayeongozana na Lissu anaitwa nani?
Mabele Makubi namuelewa sana halafu naona ITV wamekivua Koti la mapambio sijui wamebadili Mkurugenzi? kabla ya Kampeni niliweka akili yangu Azam Sababu ya Tido lkn wameniangusha sana yaani wako tayari waoneshe kampeni ya dovutwa kuliko Lisu wapuuzi sana
 
Mzee sio habari ya ukanjanja Mtu kama
AYUBU RIOBA ana ukanjanja gani ...unaona alivyoigeuza Tbc kuwa kijiwe cha ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…