MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 816
Naanza kwa kuomba radhi kama nitafanya some technical mistakes katika posting yangu kwa vile ndio naanza kujiunga na forum hii, japo nimekuwa msomaji wake kwa muda. Nimejiunga na kuandika haya kwa uchungu ninaoupata na kisha sina pa kuyapeleka niliyoyapata hapa Igunga kisha nikabaki salama.
Mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya ubunge hapa Igunga Mwl Kashindye alikuwa mtumishi wa serikali akianzia ngazi ya chini kabisa ya Mwalimu wa UPE vijijini, alijiendeleza kielimu hadi kuhitimu chuo kikuu na kufikia kuwa Mkaguzi wa Elimu, vijiji vyote vya Igunga na watu wake na matatizo Yao anayajua vizuri sana, shida za waalimu anazijua vilivyo.
CCM ilikuwa imeshaandaa waalimu kuwa wasimamizi wa vituo, ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda kwa Hali yoyote ile iwayo, lakini sasa kwa kuwa mgombea wa CDM ni Mwalimu mwenzao, wakati mgombea wa CCM, Dr Kafumu ni Commissioner wa madini katika wizara ya nishati na madini, wizara inayoongoza kwa utata hapa nchini, na yeye mwenyewe akiwa ndie mtaalam wa kutoa mikataba ya madini nchini, imeonekana uwezekano wa yeye Dr Kafumu kushinda kihalali itakuwa ni vigumu, inabidi "Mbinu Mbadala" zitumike.
Awali CCM ilitaka kuwabadilisha waalimu hao wa Igunga wasikae vituoni ili waletwe wengine kutoka Singida, lakini ikaonekana hawa wa hapa wanaweza kufanya hasira na wakampigia mwenzao kampeni ya kufa mtu.
Wakiachwa waendelee uchakachuaji vituoni utakuwa mgumu. Kamati ya siasa ya wilaya ya Igunga, ikishirikisha viongozi wa kimkoa na Taifa, akiwemo Mhazini Mkuu Taifa Ndg Mwigulu, iliketi na kuamua kwa kauli moja kumuita Mkurugenzi (DED) Ndg Magayane kuwa awasiliane na wahusika wa Wizara ya elimu ili profile nzima ya Mwl Kashindye ipatikane ili ichunguzwe itafutiwe kasoro, na kama hazipo basi lazima ziwe fabricated ili zitumike kumuengua.
Izingatiwe kuwa DED Magayane ana tuhuma nzito ya ufisadi katika ujenzi wa barabara fupi ya lami iendayo kwenye Halmashauri ya wilaya, ilikuwa afukuzwe kazi kabla ya uchaguzi huu, lakini amerejeshwa kazini kwa masharti kuwa lazima CCM ishinde, jimbo likipotea na yeye apotee.
Vipengele vya kumuengua vimeshapatikana inasubiriwa siku ifike DED Magayane afanye vitu vyake, ni siri kubwa, lakini kwa kuwa miongoni mwao kuna wanaochukia dhuluma, basi vimeshavujishwa na tutavipeleka kunako husika ili kuvidiffuse.
Aidha, Mkuu wa polisi wilaya ya Igunga ambaye alikataa kuzuia operation Sangara ya CHADEMA ilipoanza wilayani Igunga, licha ya kupelekewa barua kutoka CCM ya kumtaka afanye hivyo, keshatimuliwa na ameletwa OCD mpya spesheli kuikabili CHADEMA.
Hata aliekuwa Manager wa NMB Igunga keshahamishwa kisa eti ni Mchagga na anashabikia CHADEMA kwa hiyo imehofiwa kuwa atafanya kampeni kwa vile ana influence kubwa kwa wateja wake ambao ni wengi sana hapa Igunga.
Ni kweli kuwa Mwigulu anamwaga fedha kifashisti kwa kila taasisi na makundi ya jamii, waziwazi, lakini mitego ikitegwa na TAKUKURU wakiarifiwa waje wamshike live, TAKUKURU haohao wanamjulisha kwa simu kuwa wanakuja, anawaambia wasubiri kwanza amalize kugawa, akishamaliza na kuondoka, ndio anawapigia waende wakavamie hewa.
Ndugu zangu wanaJF, ni mengi mno yatakayoikwamisha CHADEMA hapa Igunga, hata sijui niwasilishe lipi na niache lipi, maskini CHADEMA, pamoja na kupendwa na wengi sijui itashinda vipi dhidi ya dhulma hizi, au labda tupige sana kelele za mwiziii kwa pamoja mpaka ardhi itikisike!
Naishi kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamashimba, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga. Niulizeni swali lolote kuhusiana na hali ilivyo nitajibu nitakayoweza bila ya woga.
Naomba Kuwasilisha!