Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Mfumo wa utawala wa serikali ya Uingereza tofauti kabisa na Tanzania. Wao wana utawala wa Kifalme na anayeunda serikali ni Waziri Mkuu na hawana rais kama Tanzania. Ndio maana Prince Charles alipotembelea Canada hivi karibuni alikumbana na waandamanaji waliona na mabango kwamba utawala wa UK si wa kidemokrasia kwa ushikilia mfumo wa kuridhi wa kifalme.

Tumechukulia mfumo wa serikali ya Marekani ambayo mfumo wa utawala unafana kabisa na wetu, na hivyo mengi tunaweza kujifunza toka kwao kutokana na uzoefu wao wa kidemokrasia tangu mwaka 1776 hivi kama sikosei walipopiga vita kujiondoa toka ukoloni wa Mwingereza na kuachana na mfumo kandamizi wa kifalme wa UK.
 
watu waliofika katika mkutano wa CCM ni mara tatu ya CDM na picha walizotuletea katika magazeti ya bongo za chadema walichakachua, Waliweka picha za Arusha badala ya Igunga. igunga hakuna magorofa lakini picha za cdm zilikuwa na magorofa.
<br />
<br />
be great thinker man! Waliweka picha za Arusha akihutubia mgombea wa chadema Joseph Kashindye?
 
ushaona kuwa chadema ndo chama cha kujipatia umaarufu. Tatizo lako unatumia masaburi kufikiri. Mwambie mwinjilisti nape akuombea upone.
 
Du! kweli wanaigunga mkae macho,huo wali maharage usije wamaliza maana ccm wamewaon mnanjaa!
 
Kipindupindu jaribu kufupisha nukuru yako kwa kuweka link maana hakuna mtu anayeweza kuvutiwa na mlolongo mrefu na kumalisa nafasi bila sababu. Kama hujui namna ya kuweka link hapa JF si haba watakufunza namna ya kufanya.
 
Mmmmh ndio Doctor huyo bhana, madokta wote wa CCM si ndio walivyo? yaani kabisa nimchague? nimchagueje? mmh mji.... kweli huyu, halafu ujue kama kawaida wakashangilia.....!!! huwa hawa watu hawafikirii hata kidogo ukishawavisha fulana na kanga kwisha habari yao!

Bila kuficha ndugu zangu mimi nina taabu sana na wasomi wa TZ! Sasa Dr. mzima anashindwaje kujieleza mbele ya halaiki? Yaani sijui tunashindwaje kujieleza jamani?

Sasa wanaume wa Igunga mnalo! Akishinda ubunge ninyi na wake zenu wote mtakuwa wake zake Dr. Kafumu. Yaani kwa maana nyingine jimbo zima litakuwa ni wake wa Dr. Kafumu, na siku akija nyumbani kwenu mmwachie wake zenu, dada zenu na mabinti zenu! Zaidi na zaidi na ninyi wenyewe!

Dr. Hawezi kujieleza wazee tumsamehe kwa bure! Lakini kama ataenda bungeni Igunga itakuwa imekula kwenu!
 
kila unapotokea uchaguzi mdogo najikuta namkumbuka Halima Mdee

yeye peke yake alizungumza kitu cha maana kuhusu hizi chaguzi ndogo...

alisema chaguzi ndogo zinapoteza muda na pesa nyingi

ni bora ukawekwa utaratibu wa chama kinachoshikilia jimbo hilo
kuchagua ni nani arithi jimbo......

hakuna anaesikiliza haya,but huu ndo ukweli mtupu....

hizi chaguzi ndogo its a waste of time and money.....

zipigwe marufuku......

Halima James Mdee ni Iron Lady
 
tunataka ma great thinkers cdm sio masaburi kama wewe....wewe ni president elect wa familia yako inayokula mizizi kule handeni sio hapa jf


Mimi, kama 'President Elect', niko tayari kuvaa gwanda endapo CHADEMA kitafanikiwa kushinda uchaguzi mdogo, jimbo la Igunga.

Hii ni changamoto kwa CHADEMA na wapambe wao hapa JF, ambao macho na masikio yao yanafuatilia uchaguzi wa Igunga.

Jimbo la Igunga ni karata dume, ambayo CCM wanayo mikononi mwao. Kazi kwenu CHADEMA kuwapokonya, na kama mtafanikiwa, basi na mimi nitavaa gwanda, kama ilivyo kwa mh. Freeman Mbowe au mh. Zitto Kabwe. Nasema tena, kazi kwenu CHADEMA!
 
Nikukumbushe kuwa wananchi (pamoja na masikini sana) wanalipa kodi kwa serikali. Sehemu ya kodi hiyo hugawiwa kwa vyama vya siasa kama ruzuku kwa uwiano na idadi ya wabunge wake.

Ccm kwa kujua hilo wanagawa kofia na khanga bure na kuwasafirisha bure ikiwa ni matumizi ya ruzuku waliyopewa na serikali.

Kwa nini hautaki kukubali ukweli ulio wazi kwamba Chadema wana matumizi mabaya ya pesa za wananchi, kwa nini msipinge ufisadi kwa vitendo mnang'ang'ania maneno tu huku mkijua "watz wa leo si wa zamani"?

Unaweza kutuambia pesa ya ruzuku pamoja na biashara ya kuuza kofia kama unavyosema pengine na kombati, changanya na kodi mnayokwepa kulipa, pesa yote hiyo mnafanyia mambo gani mshindwe hata kuwanunulia kofia ziwasitiri na jua wananchi masikini wanaounga mkono jitihada zenu za "kuikomboa nchi", kwa nini mnalifanya suala la "ukombozi" kuwa adhabu kwa wananchi pekee na sio nyie? Kwa nini mnakosa huruma na wananchi hata kushindwa kuwagawia japo kofia bure?

Mnachofikiria ni kuwanyonya tu, kweli mwenye kidogo hunyang'anywa hata alichonacho.

Kuna picha ya jukwaa lilotumika kufanyia uzinduzi wa kampeni Igunga, ongeza na jengo la makao makuu ya Chadema vyote haviko proportional na ruzuku wanayoipata hata kidogo na kusema kweli kinachokosekana ni ushahidi wa nyaraka tu kuthibitisha kuwa kuna ubadhilifu na haitokuwa hivyo siku zote. Kama haitoshi, wanatengeneza kofia kwa bei ndogo na kuwauzia wananchi masikini kwa bei kubwa huku wakijua ugumu wa maisha yao na mfumuko wa bei.

Kwa kuyajua hayo, ni dhahiri kuwa Chadema ndicho chama chenye matumizi mabaya zaidi ya pesa za wananchi kuliko chama chochote kingine, achilia mbali Ccm.
Yuh should know better, sir...
Yaani CCM kugawa kofia na kuuza kwa bei ndogo ni kusaidia ugumu wa maisha? duh! tuna safari ndefu.
 
Kipindupindu jaribu kufupisha nukuru yako kwa kuweka link maana hakuna mtu anayeweza kuvutiwa na mlolongo mrefu na kumalisa nafasi bila sababu. Kama hujui namna ya kuweka link hapa JF si haba watakufunza namna ya kufanya.
tatizo mkiwekewa link hamsomi!!cha msingi hapo sio urefu wa article,hebu tujikite katika suala letu la msingi huko nje mliposema ndivyo wanavyofanya na sisi tumeiga huko!
 
CCM inawafanya watanzania kama vile watoto wadogo..,yaani vyakula.,pombe..,chumvi ndo mtaji wa CCM..,heb cheki hapo mbele ni watoto wadogo tuu waliojazana kuangalia hao Makomedi weo..!
Hakuna kitu..!
 
Wanajamvi mwenye macho haambiwa tazama lakni ukifuatilia habari ya gazeti letu la ukweli, Mwananchi CCM hawana chao Igunga. Angalia watu wa Igunga walivyowaelewa wa mambo mazito kama kodi na jinsi gani serikali haizitumii ipasavyo kodi hizi. Soma mwenyewe

Wengine waondoka mkutanoni
Wakati Mkapa akiendelea kuhutubia, baadhi ya watu wakiwa kwenye makundi walianza kuondoka kwenye mkutano huo.

Wengi waliohojiwa na Mwananchi Jumapili walisema hakuna jipya katika hotuba ya Mkapa na kuongeza kuwa, waliyokuwa wakiambiwa na wapinzani yalithibitishwa na Mkapa mwenyewe.
Walitoa mfano kuwa Mkapa alipoingia madarakani, makusanyo ya Serikali kwa mwezi yalikuwa ni Sh28 bilioni, lakini hadi anaondoka, makusanyo hayo yalikuwa ni Sh400 bilioni na kuongeza kuwa ni wazi Serikali ina fedha, lakini hazitumiki kwa shughuli za maendeleo.
 
sio pumba....hata huko marekani hawarudii rudii chaguzi kwa staili yetu....

ni bora chama kinachoshika jimbo kifanye chaguzi ya ndani....au tuje na sysytem nyingine itakayokubalika.....

kuna system nyingi tu.....
Kuna nchi ambazo system zake watu wanachagua chama na si mgombea as such, mf. Italy. kwa mtindo huo ni sawa kabisa kama nafasi imekuwa wazi ikarithiwa na mtu mwingine wa chama hicho. Lakini system yetu ni kwamba wananchi wanachagua mtu aliye mwanachama wa chama fulani. Kwa jinsi hiyo itakuwa ni makosa, kama nafasi imekuwa wazi, kurithisha mtu wa chama kilichokuwa kinashikilia uwakilishi bungeni. Hii ni kwa sababu watu hawakuchagua chama bali mtu, ambaye ni wazi ameshikamana na chama fulani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom