Uchaguzi Kenya:Mahakama yashindwa kusikiliza kesi ya kuahirishwa kwa uchaguzi

Uchaguzi Kenya:Mahakama yashindwa kusikiliza kesi ya kuahirishwa kwa uchaguzi

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
65,136
Reaction score
91,917
Mahakama ya Juu Kenya yashindwa kusikiliza kesi ya kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na ukosefu wa majaji wa kutosha mahakamani.

Jaji Mkuu David Maraga amesema baadhi ya majaji wamo nje ya nchi na wengine hawangeweza kufika mahakamani kwa sababu mbalimbali.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na wapiga kura watatu wakisema Tume ya Uchaguzi haiko tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki kesho.

Jaji Mkuu amekuwa mahakamani na Jaji Isaac Lenaola pekee.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakuweza kufika kortini baada ya kupigwa risasi kwa dereva wake jana jioni.

Jaji Ibrahim, ambaye amekuwa akiugua, yuko nje ya nchi.

Majaji Smokin Wanjala na jacktone Ojwang hawakuweza kufika kortini pia.

Jaji Njoki Ndung'u alikuwa amesafiri nje ya jiji la Nairobi na hakuweza kupata usafiri wa kumuwezesha kufika mahakamani kwa wakati.

"Sisi wawili hatuwezi kufikisha idadi inayohitajika ya majaji mahakamani kwa mujibu wa kifungu 162 (2) cha Katiba. Kesi imeahirishwa hadi wakati mwingine," ametangaza Jaji Maraga.

Wakili watatu hao Harun Ndubi ameshutumu hatua ya majaji kukosa kufika kortini akisema ni jambo la kushangaza.

"Wakitoweka wakati tunawahitaji kutekeleza jukumu hili muhimu, unashangaa iwapo wanafuata kiapo walichokula," amesema.

Seneta wa Siaya ambaye aliwakilisha Raila Odinga mahakamani amesema kilichotokea leo ni "mapinduzi ya katiba".

"Haya yamekuwa yakifanyika, hata katika tume ya uchaguzi. Stakadhabi zilizowasilishwa na tume kujibu kesi zimewasilishwa na naibu mwenyekiti na wala si mwenyekiti. Ni wazi kwamba tume ya uchaguzi inafanya kazi bila mchango wa mwenyekiti. Wafula Chebukati amekuwa abiria," amesema.

"Taasisi ambayo imelemazwa na Jubilee kwanza ni IEBC. Na tume iliyosalia haina uwezo wa kuandaa uchaguzi."

Bw Orengo amesema anaamini ukosefu wa majaji wa kutosha mahakamani haufai kushangaza wengi na kudokeza kwamba uamuzi wa kutangaza leo kuwa Siku ya Mapumziko ulilenga kuvuruga shughuli za mahakama.

"Kuna jaribio la kuhujumu taasisi za serikali zikiwemo taasisi huru kama vile tume ya uchaguzi na Mahakama ya Juu," amesema.
 
Majaji akaunti zitakuwa zimenona. Sijui itakuaje huko Kisumu, Homabay,Siaya kauntiz.
 
Hajawateka kila mtu katoa udhuru wake,
watakuwa wamegundua njama ya odinga na jaji mkuu kuahirisha uchaguzi ili ifike tarehe 31 oktoba ambayo ndo kikatiba ni mwisho wa rais uhuru kuwa rais na hivyo jaji mkuu ndo angekamata madaraka kusubiri uchaguzi mwingine baada ya miezi 3,

sasa nadhani timu uhuru nao wamehakikisha column ya majaji haitimii kwa vyovyote vile ili kesi iliyofunguliwa jana kutaka kuzuia uchaguzi wa kesho ife,

ndivyo ilivyotokea jaji amesema kesi haiwezi kuendelea kwahiyo uchaguzi kesho upo.

Sasa odinga kabaki na karata ya kuzuia uchaguzi kwa kufanya fujo hiyo kesho.

Huyu jaluo hafai kabisa
 
Hicho alichofanya Uhuru unaona kinafaa?hizi double standards za kudai katiba mpya nyumbani na kushangilia wanaozuia Katiba kufanya kazi nchi nyingine!!
 
Wabongo banah nyie mko na shida mingi huko kwenu mnazusha mambo za uwongo kwa Uhuru, fight for your Tz kwanza wachana na mambo za kwetu Buda
 
Kenya kwa kweli ni Nchini kubwa ya kutajika Ukanda huu wa Africa ndio maana hatuwakosi Majirani kuanzisha nyuzi za kukemea na pongezi.
 
WaTz n nini nzuri yenye Kenyata amefanya kwa izo miaka amekua rais? leave us alone we know who fits us....nyie nyongorokeni na maguli yenu nughu nyinyi
 
Wabongo banah nyie mko na shida mingi huko kwenu mnazusha mambo za uwongo kwa Uhuru, fight for your Tz kwanza wachana na mambo za kwetu Buda

wewe bana acha upumbavu... ongea hoja longo longo ya nini?
wewe unafikiri Kenya kuwa katika sintofahamu ya uchaguzi muda wote huu ni sawa??
 
WaTz n nini nzuri yenye Kenyata amefanya kwa izo miaka amekua rais? leave us alone we know who fits us....nyie nyongorokeni na maguli yenu nughu nyinyi
Hilo tusi mwenyewe. Unaongea kama umetoka kulala saa hii !
 
majaji wapo sita...kiherehere nyingi na hkuna unalolijua kuhusu Kenya
 
WaTz n nini nzuri yenye Kenyata amefanya kwa izo miaka amekua rais? leave us alone we know who fits us....nyie nyongorokeni na maguli yenu nughu nyinyi
leave this nugus alone...wanapenda sana udaku....kufatilia za nchi zingine...wakenya hata huwezi waskia wakifuatilia siasa za nchi ingine kana kwamba ni wakimbizi...
 
Africa ya vihoja sana
Hao ni jamaa zake Mbow na nyeupe, hahahaha, yaani upepo wa wapinzani wa Tz unawaelemea vibaya sana, maana wangekuwa kwa Mh. Odinga basi CCM tusingekunywa maji, ila sasa huo udikiteta anaoufanya uhuru wanaona poa, hahaha
 
Back
Top Bottom