Kenya sasa hivi hakuna wa kumnyooshea mwengine kuhusu ukabila, tatizo unafiki ndio zetu. Nyie hapo kwenye upinzani juzi mumemtawaza kiongozi na msemaji wa kabila bwana Mudavadi, ambaye kuna uwezekano akawa ndiye atakayelipeperusha bendera lenu, leo hii mnanyoosha kidole na kutaja ukabila.
Ukabila Kenya ulianza hata kabla ya kunyakua uhuru, mkoloni aliwagawa mababu zetu kwa misingi ya kikabila, wakati anakuja kuachia nchi, tayari kulikua na mgawanyiko. Waasisi wa Kenya nao wakaendeleza na siye vizazi vya leo tukapokea na tupo mbioni kuwapokeza watoto wetu.
Rais wa nchi ni kioo cha tulivyo, viongozi wetu wapo jinsi tulivyo. Hakuna anayeweza kushinda urais Kenya bila kucheza michezo ya ukabila. Hata huyu Uhuru na Ruto walicheza hayo ya ukabila hadi wakafika hapo. Upinzani umekua ukijaribu kucheza ukabila ule wao wa 40 against 2, yaani ukabila ni kansa iliyo dani ya damu yetu na itabidi tuishi vivyo hivyo. Hata Wakenya kama nyie mlio huko ughaibuni ndio wakabila mwanzo mwisho, mumejigawa na kuishi kwa misingi ya ukabila.
Aidha tukubali huu ugonjwa utumalize sote au turekebishe.