Uchaguzi klabu ya Yanga kufanyika Mei 05 badala ya tarehe iliyotangazwa awali ya Aprili 28

Uchaguzi klabu ya Yanga kufanyika Mei 05 badala ya tarehe iliyotangazwa awali ya Aprili 28

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ally Mchungahela ametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kwamba utafanyika Mei 5 mwaka huu.

Uchaguzi huo umetangazwa kufanyika siku hiyo kutokana na agizo la Serikali kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT), kuitaka TFF isimamie klabu hiyo ifanye uchaguzi wake ndani ya siku 30.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo Karume Ilala jana, Mchungahela alisema wametoa taarifa ya kufanyika uchaguzi huo kwa lengo la kuwajulisha wapenzi na wanachama wa Yanga maendeleo ya mchakato wa uchaguzi yalipofikia na kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa leo makao makuu ya Yanga.

Alisema kwa wale waliochukua fomu awali kwa ajili ya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi hawatachukua tena na badala yake watasubiri kupigiwa kura siku ya uchaguzi huo mkuu kwa vile walishafanyiwa usaili na kufanya kampeni. “Hakuna asiyefahamu uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika hapo awali lakini baadae ulishindwa kufanyika kwa sababu za kisheria na sasa uchaguzi utafanyika kwa tarehe tuliyopanga na si vinginevyo kwa ushirikiano wa wanayanga wenyewe chini ya uangalizi wa Shirikisho la soka nchini kwa sababu ni chombo kinachosimamia mpira,” alisema Mchungahela.

Mchungahela alisema wao wana mamlaka ya mwisho kutangaza tarehe ya uchaguzi. Tarehe hiyo ni tofauti na ile iliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Baraza la wadhamini la Yanga chini ya George Mkuchika kwamba Aprili 28 ndio uchaguzi ungefanyika.

Mchungahela alisema tarehe hiyo iliyopangwa na baraza la wadhamini kutakuwa na fainali za Afcon kwa vijana zinazotarajiwa kuanza Aprili 14 nchini hivyo wengi watakuwa wakifuatilia fainali. Wajumbe Yanga waliohudhuria kwenye mkutano huo ni Omary Kaaya, Zayumba Hamis, Karume Benjani, Mwamedi Mtengulwa ambaye ni mbunge kutoka Rufiji na wakili Sam Mapande. Mchungahela alisema hadi sasa wameshapata daftari la leja linaloonesha orodha ya wanachama hai wa timu hiyo na kwamba hiyo ni ishara njema kwa wanachama.
 
Mapopoma wapo bize na Simba huku hata uongozi tu unawashinda kuchagua.
 
Uchaguzi wa heri nawatakia chama langu tuko pamoja
Daima mbele nyuma mwiko
 
Back
Top Bottom