Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #181
HALI ILIVYO NDANI YA DEMOCRATMag3
Baada ya uchaguzi wa Indiana na W.Viriginia hali nyingine inajitokeza kwa Demo. Sanders aliwahilalamika kuhusu SD na kwamba wanapaswa kuunga mkono mgombea na sehemu alizoshinda
Wakati Sanders ameshinda Caucus 7 mfululizo ambazo kimatiki si ngome ya Democrat , kauli mbiu ilikuwa 'ushindi wa majimbo 7' na aungwe mkono na SD
Baada ya uchaguzi wa NY, Clinton alishinda majimbo 5 makubwa ikiwemo Pen, Conn, Maryland, Delaware. Kwa maneno mengi alishinda majimbo 6 kati ya 7.
Hakukuwa na kauli za 'ushindi' huo mfululizo licha ya ukubwa na umuhimu wake
Sanders amebadili kauli, anatumia kura za maoni kujenga hoja.
Anasema kura za maoni zinaonyesha akimshinda Trump kwa Point 20 huku Clinton akimshinda kwa ukaribu sana
Habari za wiki hii, vyombo vingi vya habari vimeondoka katika hoja ya SD na hesabu zinazomkabili Sanders,vinazungumzia kura za maoni kati ya Dem Vs Trump
Hili linafanyika makusudi kwa maana mbili.
Kwanza, 'kuwatisha' SD kuwa Clinton ni risk kwasababu Trump anamkaribia.
Sanders anataka kushawishi SD,huko nyuma alipinga influence yao katika primaries
Pili, kuendelea kuwashawishi wapiga kura kuwa Clinton hachaguliki
Kitu ambacho ni intriguing ni namna vyombo vya habari vinavyoungana na Sanders katika kura za maoni dhidi ya Trump. Hili limechukua sehemu kubwa ya maongezi.
Tafiti zinazofanyika sasa hivi nyingi ni kuhusu Clinton/Sanders Vs Trump
Kwanini tafiti hizo zinatoka mfululizo kila siku, na kwa mpangilio fulani.
Inakuwaje watafiti walianza siku moja na kumaliza katika muda sawia?
Je, kuna mahusiano yoyote ya Sanders na wamiliki vya vyombo vya habari ambavyo kwa Marekani umiliki wake umehusishwa sana na makundi fulani ya jamii?
Je, kuna uhusiano wa watafiti na vyombo vya habari?
Tunauliza hivyo, kwasababu mwendo wa vyombo vya habari katika mazingira yaliyopo vingemuonyesha Sanders ugumu na pengine kuweka shinikizo ajitoe.
Vingeonyesha madhara yanayoendelea upande wa Democrat
Kinyume chake kumekuwa na kumtia moyo kwa kujenga hoja ambazo kila siku zinabadilika. Nini kinaendelea nyuma ya pazia na katika Democrat kwa ujumla?
Tusemezane
VYOMBO VYA HABARI NA USAIDIZI KWA SANDERS
MWELEKEO WA 'CONVENTION' UNAZIDI KUPATA KASI
Katika bandiko tulilonukuu tulieleza vyombo vya habari na ushiriki katika mchakato wa Democrat. Tulihoji 'mahusiano' ya vyombo hivyo na Seneta Bernie Sanders
Kwanza, kila ilipotokea Sanders kashinda mfululizo hiyo ndiyo ilikuwa habari.
Kwa mfano, kabla ya uchaguzi wa NY, Sanders alishinda majimbo 7 yakiwa na caucus zaidi. Habari katika vyombo ilikuwa ushindi mfululizo
Clinton alishinda NY, Penn, Conn, Delaware, Maryland mfululizo. Haikuwa habari
Hesabu zikaonyesha ugumu kwa Sanders, kauli ikabadilika uchaguzi lazima uende Philadelphia. Hoja ikawa kuwa wajumbe wa SD wasihesabiwe hadi kura katika mkutano mkuu. Hoja hiyo ilijibiwa kuwa ni utaratibu wa Dem kama ulivyotumika kwa Clinton 2008
Sanders akaja na hoja kuwa kwa kuangalia kura za maoni, yeye anamshinda Trump kwa mbali ukilinganisha na Bi Clinton. Kauli kairudia mara nyingi.
Tulihoji kwanini kuwe na ulinganifu kati ya Sanders na Trump na si Sanders na Clinton?
Vyombo vya habari vikaiuchukua habari hiyo na kuifanya habari ya kila siku.
Tulihoji kuhusu taasisi mbali mbali kuendesha kura ya maoni kati ya Sanders na Clinton Vs Trump. Democrat hawajamaliza mchakato na hali ilivyo Clinton anaongoza.
Iweje kuwe na kura ya maoni kumhusisha Sanders na Trump ili hali nafasi yake ni finyu?
Taasisi zikatoa kura za maoni za kitaifa zikionyesha kukaribiana kwa Clinton na Trump kila siku. Ndani ya wiki moja ambayo Trump alikuwa mapunzikoni katika hali ya kujiuliza , kura hizo zinaonyesha akiwa sawa na Clinton 'dead heat' na zingine akimshinda Clinton
Hili linafanyika kisayansi na kwa umakini wa hali ya juu sana.
Kwamba, Sanders ana nafasi kuliko Clinton na hivyo kujenga mazingira yafuatayo
1. Kuwakatisha tamaa wafuasi wa Clinton dakika za mwisho ili Sanders ashinde majimbo yaliyobaki kwa kiasi kikubwa na kujenga hoja ya kwenda convention
2. Kujenga mazingira ya kuwatisha Super Delegates (SD) kuwa Clinton hamwezi Sanders na hivyo wabadili mweleko na kumuunga mkono Sanders
Katika kushadidia hilo vyombo vya habari vinaonyesha kura za maoni vikisisitiza kipengele cha 'disliked candidates' katika historia ya Marekani kuwa Trump na Clinton.
Kwa maneno mengine tayari vinamjenga Sanders kuwa ni 'liked'
Katika wakati huu, Trump anaunganisha Republican licha ya upinzani mkubwa alio nao. Ni mapema mno kubaini republican wame rally behind him.
Clinton ana vita mbili, kwanza, na Sanders na pili Trump.
Hivyo kwa Democrat ni ngumu kupata idadi ya wapiga kura jambo linaloonyesha kura za maoni zinafanywa kwa makusudi na si kwa kuzingatia hali ilivyo.
Hakuna anayeeleza kuhusu mashambulizi ya Sanders na Trump dhidi ya Clinton na kwamba hilo si tu linabadilisha kura za maoni, bali linamumiza sana Clinton
Kwa mtazamo huo, uwezekano wa uchaguzi kwenda convention unaongezeka, si kutokana na namba bali usaidizi mkubwa wa vyombo vya habari kwa Sanders.
Kuna uhusiano gani kati ya Sanders na vyombo vya habari na kwanini na nani walioko nyuma ya mango huo?
Na hili linaeleza nini kuhusu hatma ya Bi Clinton kuanzia June 7 kuelekea Philadephia?
Tutajadili