Uchaguzi Marekani

Uchaguzi Marekani

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Wanajamvi, uzi huu utakuwa endelevu ukizijadili siasa za Marekani kuelekea uchaguzi

Tumefanya hivyo chaguzi zilizopita na tunaendelea ingawa tumechelewa kidogo

Siasa za ndani ya nchi zimechukua sehemu kubwa ya mijadala kutokana na umuhimu

Mchakato wa kupata wagombea kwa Republican(GOP) na Democrat(Dem) unaendelea.

Mlolongo wa wagombea umepungua na kufikia 4 kwa republican na 2 kwa Dem

Katika chama cha Dem, wagombea waliojitokeza walikuwa watatu ambao ni secretary Hillary Clinton, Seneta Bernie Sander na aliyejiondoka O'Malley

Kwasasa wamebaki wawili baada ya O'Malley kuhitimisha kampeni mapema

Kwa upande wa GOP wagombea waliobaki ni 4, Tajiri Donald Trump, Seneta Marco Rubio, Seneta Ted Cruz na Gavana Kasich wa Ohio

Mchakato unaendelea Trump akiongoza upande wa GOP, na Clinton upande wa Dem

Kuna wasi wasi mkubwa upande wa GOP kutokana na kampeni za rafu zilizochezwa

Wasi wasi kutoka vigogo wa GOP juu ya Trump kubeba bendera ya GOP uchaguzi mkuu

Trump hakupewa nafasi ndani ya GOP alipoanza kampeni.

Kasi yake na kauli zake zinaonekana kusikika miongoni mwa wahifidhina.

GOP 'establishment' wameshikwa na butwaa endapo Trump ata kuwa mgombea

Nini kinaendelea katika kampeni? Kwanini kuna wasi wasi ndani ya GOP?

Kwanini wanataka 'kumkata' Trump kiaina?

Nini kinaendelea upande Dem kati ya Clinton na Sander?

Tutaendelea kumega kila wakati tukiangalia wagombea na nini wamarekani wanafikiri

Ni uzi endelevu utakaokuwa unajadiliwa kila Jumatatu. Jumatano na Jumamosi

Tuwe pamoja
 
MTAZAMO 'MDOGO' WA NAMNA WAGOMBEA WANAVYOPATIKANA

Katika uzi wa uchaguzi wa 2010-Marekani, tulieleza kwa kadri mchakato wa kupata wagombea ndani ya vyama unavyofanyika na 'unavyochanganya'

Kwa minajili ya mnakasha, tutapitia kwa ufupi kujenga uelewa tukisonga mbele

Lipo neno linatumika mara nyingi 'the establishment' ambalo wengi huwatatiza

Neno hili kwa maana rahisi ya kiswahili 'Magwiji' yenye ushawishi katika vyama, taasisi za umma, taasisi binafsi na hata vyama vya michezo na kijamii

Mifano, klabu za Simba na Yanga zina watu wenye ushawishi wanaoziongoza hata kama si viongozi. Kwamba, wao ndio wanaamua nani afanye nini. Hawa ni ''the establishment''

Vyama vya siasa vina watu wenye ushawishi wanaoamua nani awe nani.

Mathalan, CCM ina kundi la watu wanaoamua kiongozi gani awe katika nafasi gani.
Hawa ndio walioleta kile kinachojulikana kama 'kukatwa' au kuchinjwa

Vyama vya upinzani vina establishment,watu wanaoamua aina ya uongozi utakaokuwepo. Mara nyingi,magwiji wamesigishana na wanaotaka mwelekeo tofauti na kuzua tafrani

Ndivyo ilivyo duniani kote, kule India familia ya Gandhi ikiwa ni 'the establishment'

Kenya kuna 'the establishment' kutoka Wakikuyu wanaoongoza siasa za nchi hiyo

Vijana-ANC walipoanzisha Umkhonto Wesizwe, lengo lilikuwa kukabiliana Magwiji.
Vijana hao walitaka mwendo tofauti wa kukabiliana na ubaguzi kwa silaha

Kwa wale wanaomsoma Mohamed Said, anamtaja Abdul Wahid na wenzake kuvamia ofisi za TAA na kubadili uongozi kwa nguvu. Hawa walipambana dhidi ya 'the establishment'

Kuibuka kwa G55 ya CCM kulionekana kuchagizwa na Zanzibar kujiunga na IOC.

Lakini,mwenendo wa G55, ulikuwa kukabiliana na 'Magwiji' 'the establishment'

CCM-Zanzibar wanaojulikana kama wahafidhina, hawa ni ''the establishment'

Hata ndani ya CUF wapo viongozi wenye ushawishi ambao ni 'Magwiji' pia

Sifa mojawapo ya magwiji ni kutotaka mabadiliko tofauti na mazoea

Hapa ndipo tunafikia katika wagombea wa Marekani

Senata Rubio, Senata Cruz na Gavana Kasich ni 'The establishment wa GOP'
Wamekuwepo Washington kama sehemu ya uongozi wa Republican

Kwa upande wa Dem, Hillary Clinton kama seneta na secretary of state ni 'gwiji'
Pia mumewe alikuwa kiongozi wa Dem hivyo kumfanya Hillary awe 'gwiji' mkamilifu

Senata Bernie Sanders ni independent, hata hivyo amefanya kazi katika seneti ya Marekani, anajua siasa za vyama na ana ushawishi. Naye pia ni 'the establishment'

Mtu pekee ambaye si 'gwiji' ni Donald Trump. Huyu hajawahi kuwa sehemu ya Washington. DC.( DC inatofautisha na jimbo linaloitwa Washington)

Hapa tusisitize ingawa ni maarufu (celebrity) na tajiri,hajawahi kuwa kiongozi wa GOP

Ni mtu anayetoka nje ya kundi la GOP linalojulikana Washington, DC

Hata hivyo, rekodi hiyo inamletea tatizo miongoni mwa Mwagwiji na ndilo linaloonekana kutaka kupelekea 'kukatwa' au kuchinjiwa baharini.

Ni kwanini? Tutaendelea kufafanua
 
UCHAGUZI NDANI YA VYAMA, GOP & DEM

Kinachoendelea sasa hivi ni uchaguzi ndani ya vyama kupata mgombea
Marekani, mgombea hupatikana kwa kura za wananchi na si viongozi

Hili limelenga kupata wapiga kura wa chama husika kwa kuwashirikisha kuanzia mwanzo

Kwa maana nyingine, wanachukua 'uhodhi' wa madaraka ya viongozi kupata viongozi

Chaguzi ndani ya vyama zinalenga kupata wajumbe watakaokwenda mkutano mkuu
Mkutano mkuu iwe Republican(RNC) au Dem(DNC) ndiyo unapitisha jina la mgombea

Hivyo, uchaguzi unaoendelea ni kupata wajumbe wa mkutano mkuu
Hapa ieleweke, wajumbe hupatikana katika njia tofauti miongoni mwa vyama

Inapotokea hakuna mjumbe aliyepata idadi ya wajumbe wa kutosha, mkutano mkuu huingia katika kuchagua kiongozi (Brokered convention) au contested convention

Ndilo linaloweza kutokea kama hali ya GOP kuhusiana na 'the establishment' itaendelea
Tutafafanua mbele ya safari

Kwasasa uchaguzi ni primaries, kwamba watu wa majimbo wa vyama husika kuchagua wajumbe wa mkutano mkuu. Mfano, Michigan wanachagua wananchi wote wa kila chama

Yapo majimbo uchaguzi hufanywa na wajumbe wa chama wa jimbo husika(Caucus).

Tueleze wa mifano rahisi. Kwa mfano, CCM inatafuta wajumbe na kila mkoa utapiga kura za kupata idadi ya wajumbe kwenda mkutano mkuu(primairies)

Lakini pia kuna uwezekano mikoa mingine, wajumbe wa CCM wa vitongoji , miji, manispaa au majiji wakakutana na kuchagua wajumbe(Caucus)

Hata pale Dodoma, wabunge wa CCM walipokutana kupitisha jina la Spika, ile inaitwa caucus. Kwamba, ni wajumbe fulani tu wanaopiga kura

Taratibu huu upo kwa vyama vyote. Tofauti ni jinsi vyama vinavyogawana wajumbe

Kwa baadhi ya mjimbo, GOP -atakayeshinda kwa kura anachukua wajumbe wote.

Mfano, Florida, ina wajumbe 50, mshindi atachukua wote bila kujali nani alishinda kitongoji au mji gani

Kwa upande wa Dem, wajumbe wanagawanya kwa uwiano kutokana na ushindi
Mfano, Jimbo la Iowa Hillary na Bernie walipata asilimia 49.. wakipishana point tu.

Hii ina maana kama kuna wajumbe 30, wote watawagawana sawa

Hata hivyo, wapo wajumbe wanaokwenda mkutano mkuu kwa hadhi zao ndani ya vyama
Ndio maana utasikia non committed delegates , super delegate n.k

Ikitokea hakuna mjumbe aliyefikisha idadi inayotakiwa, ngoma inakwenda mkutan mkuu ambako kura zitapigwa kwa wagombea waliobaki(Brokered convention)

Utaratibu ni mpana sana unaohakikisha demokrasi inafanya kazi.
Tunajaribu kueleza katika lugha nyepesi na kuchukua muhimu ili tuwe pamoja

Kwa majimbo yaliyofanya uchaguzi,Trump anaongoza kwa GOP, na Clinton kwa Dem

Kwa upande wa Dem, uwiano wa wajumbe hufanya mchakato kuwa mrefu

Kwa GOP, mshindi anachukua wote, inaleta tatizo sana hasa kwa wasiomtaka Trump

Hivyo, jitihada zinazoendelea ni kuhakikisha Trump hafikishi idadi ya wajumbe wanaotakiwa mchezo uhamie mkutano mkuu ambako ndiko 'machinjio' yanapowezekana

Si rahisi kwa kuangalia hali ya uchaguzi mkuu!!Wajumbe wa Trump wanatokana na wananchi. Je, ni vema kumchinja akiwa na wafuasi?

GOP wanaogopa mkutano mkuu,historia inaonyesha huvunja umoja wa chama'makovu'

Republican wamefikaje hapo walipo? Nini kinamzuia Hillary Clinton hadi sasa?

Tutajadili
 
GOP NA DEM WAMEFIKAJE HAPA WALIPO?

Demomcrat
Baada ya kushindwa na Obama 2008, Mrs Clinton alikubali nafasi ya secretary of states

Nafasi ilimpa wasaa wa kushughulika na mambo ya kimataifa na kupata uzoefu

Tayari alikuwa na uzoefu wa kampeni za mambo ya ndani. Kuondoka katika nafasi ilikuwa kujiandaa kutengeneza timu Moya timu ya ushindi

Kutokana na uzoefu wa kampeni kali ya 2008 pamoja na mizizi ya mumewe, wengi waliona ni kupoteza muda kuingia ushindani naye, wakikataa licha ya kuombwa.

Bernie Sanders na O'Malley wakajitosa. O'Malley hakuwa maarufu.aliachia ngazi mapema

Bernie Sanders ni seneta kutoka Vermont aliingia akiwa chini ya point 30 nyum ya Clinton

Sanders ameonyesha kuziba pengo na kuzuia Hillary kuwa mgombea mapema

Kwa mfano, kura za maoni Hillary kuwa mbele New Hampshire, akapoteza kwa Sanders

Ndivyo ilivyotokea Michigan ambako Hillary aliongoza kura za maoni kwa Zaidi ya point 12, matokeo ya mwisho akashindwa na Sanders kwa takribani point 2.

Hii ilikuwa ni moja ya political upset katika primaries za Marekani

Ingawa Hillary ameshinda maeneo mengi ya kusini, Sanders anampa ushindani mzito.

Kwa idadi ya wajumbe Hillary anao wengi ukilinganisha na Bernie hadi sasa

Kuna hali isiyoelezeka kati ya wawili hawa. Mrs Clinton anakubalika na weusi(black), na watu wa umri wa miaka ya 50+. Sanders anakubalika na vijana wa vyuo licha ya uzee

Kitendawili ni pale ambapo wanawake hasa wa umri wa kati wanapompigia kura Sanders

Ilitegemewa Clinton angeungwa mkono na kundi la wanawake, inavyoonekana ni tofauti

Kampeni ya Sanders inaonekana kuwa na nguvu isiyoweza kuelezeka kwa wepesi

Kushindana na Clinton Family si jambo dogo. Kuziba 'gap' si jambo rahisi

Mrs Clinton anaonekana kufanya vizuri miongoni mwa watu wa rangi.
Sanders akifanya vema miongoni mwa weupe na kada ya kati

Swali, iwapo Sanders atashinda, ataweza kukabiliana na changamoto za watu wa rangi?

Katika moja ya mikutano, Sanders aliulizwa kwanini anaficha dini yake, ndipo alipojitambulisha kuwa yeye ni Myahudi (Jews).

Haifahamiki kwanini aliamua kuficha na hilo linaeleza nini kuhusu kampeni yake ikijulikani ushawishi wa jamii hiyo katika siasa za Marekani hasa kwa ufadhili na media

GOP inafuata
 
REPUBLICAN

Kulikuwa na wagombea Zaidi ya 10 na taratibu wakaanza kupungua.

Wingi wa wagombea ulizaa tatizo linaloonekana kusumbua GOP, Donald Trump

Ilionekana wagombea waliojitokeza wangetoa ushindani kuliko ilivyodhaniwa kwa Trump

Trump alikuwa mtoa maoni katika TV akizungumzia maeneo ya uchumi na siasa

Alionekana mtu makini kwa kuzingatia umaarufu wake katika biashara

Wengi walidhani wakati utakapofika Trump ataonyesha njia katika mambo ya uchumi

The establishment waliamini hana mvuto, kati ya wagombea 10 atapatikana mmoja

Kampeni zilipoanza Trump akaanza kuonyesha ubabe wa kauli.

Wengi wakimfananisha kama Reagan Kutokana na chuki hasa za rangi, Trump akapata kundi linaloamwamini. Kwamba Marekani inahitaji mbabe katika siasa zake na za dunia

Kundi la Trump ni la watu watiifu(loyal) kwamba atakachosema wanakikubali bila mantiki

Ukiangalia midahalo, Trump hana sera Zaidi ya kauli za kibabe za kila mara na kila siku

Tatizo likaanza, kuwa Trump ana loyal voters ambao kwa namna yoyote wapo naye

Ni asilimia isiyokubwa , ingawa ni kubwa kwa ushindi, yupo kati ya asilimia 35 na 40

Hii maana yake, asilimia 60 au 65 zinagawanwa na wagombea (Cruz, Rubio, Kasich)

Katika hali hiyo Trump anaibuka kwa ushindi kwavile ana wapiga kura wake watiifu, wakati wenzake wakigawana majimbo ya ushindi na kumwacha akitamba.

The establishment wa GOP walipouzinduka, tayari Trump ana wajumbe wengi

Ndipo jitihada zimeanza kumzuia kushinda ili suala liende mkutano mkuu (RNC)

Ndani ya mkutano mkuu, uwezekano wa kumchinjilia mbali kwa kura upo.

Kwamba wajumbe watagawanyika na huenda mmoja au wawili wakaombwa kujitoa ili kumwacha Trump na mtu atakyetoa ushindani kwa asilimia nyingi

Kwenda mkutano mkuu kuna athari zake. Atakayechaguliwa dhidi ya Trump wapiga kura wa Trump hawatamuunga mkono, hilo ni tatizo katika uchaguzi mkuu na Democrat

Kumwacha Trump kuna tatizo. Lugha yake ya kashfa dhidi ya watu weusi, walatino, wanawake, waislam na kuhusishwa kwake na kundi la wazungu 'white supremacist' la KKK linaiweka GOP katika wakati mgumu sana katika uchaguzi mkuu na democrat

Makundi tajwa yatakpokwenda upande wa Democrat ni wazi Dem watarudi Ikulu

Mazingira haya yanaichanganya Republican na the establishment wanaoona hali mbaya

Hakuna njia ya mkato kumzuia Trump bila madhara au njia ya kumwacha bila madhara

Waswahili wanasema jinni limeshatoka ndani ya chupa!

Hivyo,uchaguzi wa kesho tarehe 15 unaoitwa super Tuesday 3 utatoa mwelekeo mpya kabisa

1. Trump anaweza kushinda na kumzuia isiwezekane
2. Trump anaweza kushindwa na kuchelewesha mgombea kupatikana
3. Hillary Clinton akishinda, Sanders atakuwa na wakati mgumu
4. Sanders akishinda uchaguzi wa Dem utaendelea kwa muda mrefu Zaidi

Tutawaletea nini kinatarajiwa leo hii, baada ya masaa machache

Pia tutawaeletea matokeo ya majimbo ya uchaguzi leo hii kuanzia saa 10 usiku kuamkia Jumatano kwa wakati 'live' kadri yatakavyotolewa

Inaendelea....
 
MPAMBANO WA LEO

Majimbo yanayopiga kura leo ni Florida, Ohio, North Carolina, Missouri
Vita kubwa ipo katika majimbo mawili, Florida na Ohio

Majimbo hayo yana idadi kubwa ya wajumbe ambao wanaweza kubadili sura nzima

Democrat
Hillary Clinton anategemewa kushinda Florida kufuatana na kura za maoni
Anatarajia kushinda North Carolina pia

Ohio ni uwanja wa vita. Kimazingira Ohio inakaribiana na Michigan katika masuala ya uchumi (manufacturing). Kama Michigan, Ohio ni eneo ambalo free trade imeathiri sana

Ohio itakuwa na ushindani mkubwa kati ya Bi Clinton na Bwana Sanders.

Ingawa Clinton inasemwa anaongoza kura za maoni, kasi ya Sanders kuziba pengo ni kubwa na lolote linaweza kutokea

Hali hiyo ipo katika jimbo la Illinoi ambako Sanders anaonekana kuungwa mkono na vijana wadogo. Kesi ya vijana wa miaka 17 kupiga kura ilifanikiwa, na hivyo kuleta ushindani mkubwa. Hapa napo Sanders anaweza kumshangaza Bi Clinton

Kwa upande Missouri, Bi Clinton anayo nafasi. Hata hivyo idadi ya wajumbe haileti msisimko. Umuhimu wa jimbo hili ni kufidia tu kura za wajumbe kwa atakayepoteza sehemu nyingine na mwelekeo upo kwa Bi Clinton

Republican
Florida ni nyumbani kwa Marco Rubio ambaye amefanya vibaya katika chaguzi zilizopita

Tatizo la uwepo wake linagawa kura kati yake na Ted Cruz na gavana Kasich hivyo kumwacha Trump akiwa na wapiga kura wake 'watiifu' wasiogawika

Ikiwa Trump atashinda Florida, itakuwa pigo kwa Rubio kwani ni nyumbani kwake
Ted Cruz hana mategemeo ya ushindi katika jimbo hili au Ohio

Ohio: Ni eneo jingine la 'vita' .Ni nyumbani kwa gavana Kasich na inatagemewa atashinda

Hata hivyo, kura za maoni zinaonyesha Trump kuleta ushindani mkubwa
Ikiwa aTrump atashinda, itakuwa pigo kwa Kasich na kufungua milango zaidi kwa Trump

Kwingineko hakuna athari kubwa sana inayoweza kumzuia Trump

Hivyo, kwa Dem, ikiwa Clinton atashinda majimbo matatu, hesabu za wajumbe zitampa nafasi kubwa sana kushinda nafasi hiyo.

Ikiwa Sanders atashinda Ohio na Illinoi, bado atakuwa na hoja juu ya uwezo wa Bi Clinton kushinda majimbo ambayo ni ngome za Dem

Kwa upande wa GOP, ushindi wa Trump Floirda na Ohio utahitimisha uchaguzi

Atakuwa na wajumbe wa kutosha na hoja ya kumzuia mchakato uende mkutano mkuu itakuwa na kikwazo kukbwa

Ukiangalia uchaguzi wa leo, kwa upande wa Republican kinachoendelea si kushinda, bali jitihada za kumzuia Trump asitangaze ushindi. Hilo litawezekana?

Tutaendelea kuwaletea yanayojiri hadi matokeo ya mwisho katika muda 'real time'

Itaendelea....
 
NI KIPI KINACHOWATISHA REPUBLICAN DHIDI YA TRUMP?

Tajiri Trump anatumia pesa katika kampeni ingawa imebainika ipo michango anayokusanya
Matumizi yake yamekuwa kidogo hasa katika matangazo kwa vile anasaidiwa na media

Trump ni mtu mwenye kauli za utata sana. Kila anapozitoa vyombo vya habari huzichukua na kuzifanyia kazi. Kinyume chake, Trump anapata 'promo' kwa udadisi kuhusu yeye.

Kauli alizotoa zinazovuma katika media ni kama zile za

1. Kujenga ukuta kuzuia Walatino wasiingie Marekani, na kurudisha takribani milioni 11
2. Kauli ya kejeli aliyoitoa dhidi ya mwanadada wa Fox akidhalilisha wanawake kwa ujumla
3. Marufuku ya Waislam kuingia nchini Marekani
4. Kauli kuhusu watu weusi iliyowagusa weusi wa Marekani pia

Kama ni hivyo, kwanini anaendelea kushinda?
Jibu tumelieleza,wenye duku duku na mitazamo wanayoona inajibiwa na kauli za Trump

Mfano: Namba 1 juu. Ni kweli uwepo wa Walatino umeongeza idadi ya wafanyakazi na kupunguza kipato. Waathirika hapa ni watu weusi kwa kuangalia elimu

Marufuku ya kuingia waislam: Kutokana na hali ya usalama wa dunia na yale ya Sept/11, wapo wanaoamini kuzuia waislam kutaiweka Marekani salama!

Kuhusu watu weusi: Kauli hiyo inaungwa mkono na kundi la 'white supremacists' wabaguzi. Donald Trump ametajwa na KKK na kuhusishwa nalo.

Majibu yake si kukana dhana ya ubaguzi bali kukana kushirikiana nao

Makundi hayo ndiyo yanatengeneza ile asilimia anayoshinda nayo.
Ni makundi matiifu(loyal) ambayo hayawezi kubadili msimamo iwe iwavyo

Trump alisema kama yupo mwanadamaji anyempinga, atandikwe sumbwi yeye atalipa gharama za kisheria.Siku chache baadaye mwandamaji mmoja akachapwa sumbwi

Ikifika hapo, The establishment na GOP wanahofia sana chaguo la Trump.
Wanatambua, uchaguzi na Democrat watakuwa wamepoteza sehemu kubwa ya kura

Kwa mfano, hawatakuwa na kura za minority ikiwemo za dini, unasaba na jinsia

Wana hofu mdomo wa Trump unaweza kuwaweka pabaya katika uchaguzi wa wabunge (Congress) na maseneta(Senate) hivyo kuweza kupoteza mabunge yote mawili

Hizi ndizo sababu zinazoifanya Republican iangalie siku ya leo kwa jicho kali

Tutaendelea
 
MATOKEO YANAVYOTUJIA

Hillary Clinton kashinda Florida, Ohio na North Carolina
Illinoi na missour bado wanahesabu, Clinton yupo mbele

Republican
Trumo kashinda Florida
Kasich kashinda Ohio

Majimbo mengine yanaendelea kuhesabu

Tunaendelea...
 
4. Kauli kuhusu watu weusi iliyowagusa weusi wa Marekani pia

Mzee, natumai na wewe haupo kwenye kundi linaloamini habari za kizushi zinazotungwa kwenye mitandao.

Lakini kabla sijaendelea, ngoja niulize ili nijue kwa uhakika unazungumzia kauli ipi.

Ni kauli ipi hiyo ya Trump kuhusu watu weusi unayoizungumzia hapo?

Unaweza kuniwekea hapa hiyo kauli na chanzo labda cha ulipoitoa, tafadhali?
 
UPDATE
Donald Trump kashinda jimbo la Illinoi

Marco Rubio amehitimisha kampeni baada ya kushindwa na Trump nyumbani kwake Florida

Tutakuwa tubaleta update katika bandiko hili

Update
Donald Trump kashinda North Carolina

Update (saa 1.21 asubuhi)
Hillary Clinton kashinda Illinoi

Update 1.40
Missouri

Bado kuna kufungana kwa kiwango kikubwa

Republican: Asilimia 99 ya kura imeshahesabiwa, Trump anamzidi Cruz kwa kura 300

Democrat: Asilimia 98 ya kura imeshahesabiwa, Sanders anamzidi Clinton kwa kura 200

Miji iliyobaki ina wakazi wengi wanaoweza kubadilisha matokeo ya Rep au Dem

Update 1.43 (asubuhi)
Democrat Missouri, Hillary Clinton anaongoza kwa kura 1000 dhidi ya Sanders
 
BAADA YA JUMANNE

Washindi wakkubwa wa siku hii ni Hillary Clinton wa Dem na Donal Trump

Bi Clinton alihitaji ushindi hasa sehemu mbili muhimu sana, Ohio na Illinoi

Ni baada ya kupoteza jimbo la Michigan licha ya kudhaniwa kuwa mbele kwa point nyingi

Ilianza kuonekana ushindi wa Bi Clinton ulikuwa maeneo ya kusini, na kwamba alipata tabu na maeneo ya juu na kati magharibi. Kushinda Ohio ilikuwa ni lazima kwasababu hizi

1. Kupunguza mwendokasi wa Sanders (Momentum)
2. Kuzuia wajumbe (super delegates) wasihame kutoka kwake
3. Kuleta imani kwa wafadhili kuendelea kutoa pesa kwa kampeni
4. Anakubalika maeneo yote na ana uwezo wa kushinda kote

Hapa tufafanue kuhusu super delegates na wajumbe wanaochaguliwa

Wajumbe wanaotokana na ushindi wa mgombea wanaitwa 'won delegates'

Lipo kundi linaloingia mkutano mkuu kutokana na sifa zao(super delegate)
- Marais wastaafu na makamu wao
-Magavana
-Wabunge wa Congress na seneti
-Wajumbe wa kuchaguliwa kuingia mkutano mkuu n.k.

Wote pamoja na wale wa 'kushindaniwa' ndio wanaotengeneza mkutano mkuu (DNC)

Super delegates wanaweza kuahidi kumuunga mkono mgombe, lakini hawafungwi kwa hilo. Wakati wowote wanaweza kubadili kura zao kwa mgombea wanayemtaka

Kwa hesabu Bi Clinton ana wajumbe wengi wa kushinda na super delegates
Hili ndilo alilotaka Ohio, kuwashawishi super delegates kwamba anakubalika.

Ilifahamika atashinda Florida, North Carolina. Mtinange ulikuwa Illinoi na Ohio sehemu muhimu ya uchaguzi mkuu. Jana, Bi Clinton kashinda maeneo hayo

Ushindi wake unaendelea kutoa imani anakubalika maeneo yote na ndicho alichotaka

Maana yake, ameshinda wajumbe wengi kulinganisha na Sanders na anawapa imani super delegates kuwa anakubalika

Ushindi wa Florida ulikuwa mkubwa akimshinda mpinzani wake kwa asilimia nyingi

Hili linampa wajumbe wengi wakati wa kugawana kwa uwiano

Ilinoi na Missouri walikaribiana na hivyo kugawana wajumbe kwa ukaribu sana

Sanders alitaka kushinda Ohio na Illinoi kuwashawishi super delegates kuwa anakubalika ili wahame na kumuunga mkono. Hilo halikutokea kwa upande wake

Hii ina maana gani kwa hesabu? Ni kuwa ili Sanders apate wajumbe wa kutosha ni lazima amshinde Bi Clinton kwa maeneo mengine kwa asilimia takribani 60.

Chini ya hapo watagawana wajumbe huku Bi Clinton akiwa anaongoza tayari kwa idadi

Kushinda majimbo 5 imeongeza morali kwa timu Bi Clinton, ikivunja moyo timu Sanders.

Hesabu hazionekani kumpendelea Sanders, ana wakati mgumu kumfikia Bi. Clinton

Kwa upande wa GOP

Inaendelea
 
JUMANNE (GOP)
Kiwewe kilikuwa kumzuia Trump kwa wagombea kushinda Florida na Ohio

Majimbo ya mshindi anachukua wote na yenye wajumbe wengi

Florida, nyumbani kwa Marco Rubio ilitegemewa angefanya vema
Rubio ameshindwa vibaya na Trump akiwa senata wa eneo hilo

Kabla ya uchaguzi, kulikuwa na mjadala miongoni mwa washauri wa Rubio wakimtaka abwage anyanga kabla ya 'kuadhibiwa' kama seneta nyumbani kwake

Kuadhibiwa kutamshusia hadhi ya kukataliwa nyumbani, hoja itakayomuumiza Rubio
Alikataa ushuri akiamini atashinda, kashindwa na kufunga kampeni

Trump ameshinda maeneo yote isipokuwa Ohio kwa Gavana Kasich.
Gavana amechukua wajumbe wote 66 na kuweka 'kizuizi' cha muda kwa Trump.

Kwa jana, ilikuwa win-win situation. Kwamba Trump ameendeleza wimbi la ushindi kwa majimbo 4, the establishment wa GOP wakimzuia wakati wanatafakari nini cha kufanya

Mchakato unaelekea majimbo ya magharibi kama Arizona. Suala la wahamiaji haramu ni maarufu huko na ''sera'' za Trump zinakubalika. Hivyo, kumshinda itahitaji nguvu za ziada

Tatizo linalojitokeza kwa 'the establishment' ni kuwa Ted Cruz anamkaribia Trump nafasi ya pili kwa wajumbe na kuonekana kama ndiye 'chaguo'

Gavana Kasich amemshinda Trump Ohio. Je, ni kwavile ni nyumbani au ndio kuimarika?

Hapa pana tatizo, ukiangalia takwimu Kasich anashika nafasi ya tatu.
Kwa idadi ya wajumbe yupo nyuma sana ya Trump

Je, nguvu za ''the establishment'' zielekezwe kwa Kasich au kwa Cruz ambaye jana hakushinda popote ingawa ana nafasi ya pili ya idadi ya wajumbe?

''The establishment'' wanakabiliwa na changamoto nyingine, je, waendelee kumzuia Trump hadi mkutano mkuu ili 'wamchinjilie mbali''

Je,mkutano mkuu nani anafaa, Cruz aliye na wajumbe wengi au Kasich na momentum?

Nini hatma ya kumchinjilia mbali Trump, wafuasi wake wanaoonekana kuongezeka watachukua hatua gani?

Akiamua kugombe binafsi nini nafasi ya republican mbele ya Dem?

Hesabu zinaonyesha Trump atakuwa mgombea, the establishment wanakataa ukweli huo

Kila njia watakayojaribu kumzuia ina miba mikali!
 
YA REPUBLICAN NA CCM

''YANAFANANA'' KWA VIWANGO TOFAUTI

Kwavile Trump anashinda chaguzi ndani ya chama, ikubalike kuwa ana wafuasi

Hata kama ni kundi dogo ndani ya chama, au anafaidika na wingi wa wagombea hilo haliwezi kuondoa ukweli kuwa anashinda chaguzi na anakubalika

Anakubalika kwa maana zifuatazo, kwanza, kundi linalompigia kura ni la watiifu wake na hivyo litakwenda naye hadi mwisho. Hii ni 'plus' kwa kuwa na wafuasi committed

Pili, wale walioacha kupiga kura wengine wanarudi kwasababu yake. Hiyo ni 'plus' nyingine

Tatu, hoja zake zinarindima masikioni mwa watu, ambao ni wachaguzi

Nne, katika wale wasio na vyama (independent/ undecided) wapo watakaomuunga mkono

Hivyo ni haki kusema anakubalika ndani ya GOP kama ambavyo Lowassa alivyokuwa anakubalika ndani ya wanachama wa CCM kwa wafuasi n.k.

Trump ana makondo kando ya kauli zake yanayotishia hali ya baadaye wakati wa uchaguzi
Tumeeleza lugha inayokirihi kwa wapiga kura wa makundi ya kijinsia, kidini na hata kijamii

Lowassa alikuwa na makando kando yaliyoitishia CCM kuelekea uchaguzi

Trump ameachwa na 'the establishment' akajipanga vizuri ikitumainiwa mbele ya safari 'kifo' chake cha uchaguzi kitatokea naturally kwa kuzingatia makando kando

CCM walimwacha Lowassa akajipanga wakitegemea mbele ya safari naye atajimaliza

Trump anaonekana kubeba bendera kama ilivyoonekana kwa Lowassa wa CCM

Anapigwa vita na the establishment wa GOP kama Lowassa ilivyokuwa kwa the establishment ya CCM

Tofauti zilizopo kati ya hali hizi mbili zinazofanana.

Inaendelea
 
TOFAUTI ZAILIZOPO

Republican hawamzuii mtu kugombea , wanachama ndio wanaoamua

CCM hawamzui mtu kugombea, wanaoamua hatma ni 'the establishment'

Mchakato wa Republican upo wazi na kila hatua ipo wazi kwa washindi na washindwa

Mchakato wa CCM umegubikwa na 'chaguo la the establishment' na si wanachama

Republican wanatafuta njia za kidemokrasia kumzuia Trump
CCM wanatumia hoja za 'kitengo' na the establishment

The establishment ya Republican inaongozwa na ushawishi na nguvu za hoja
The establishment ya CCM inaongozwa na utashi wa kikundi cha watu wachache

Mchakato wa Republican upo wazi ukifuata taratibu
Mchakato wa CCM uliongozwa na kukiukwa taratibu na kubadili sheria za mchezo katikati

Kamati ya maadili ya CCM haipo kikatiba, ilipata wapi nguvu za kukata watu majina?
Kilichotokea ilikuwa kukiuka taratibu za vikao na 'the establishment' kumpanga mtu wao

Lowassa aliondoka na kundi kubwa la wafuasi lililoitikisa CCM uchaguzi mkuu.
Hatujui kama Republican watasubiri mkutano mkuu au watukubaliana na hali ilivyo

Nao pia wanakabiliwa na tatizo la kuondokewa na wapiga kura kama Trump atasimama kama mgombea binafsi. Wakiwa na Dem , GOP wanaweza kuterereka

Hii ni katika kuonyesha viwango tofauti katika kile kinachoitwa demokrasia na mfano wa demokrasia. Ukomavu na udumavu!

Tusemazane
 
Pamoja na kukubaliana na wewe katika huu mtiririko wa Uchaguzi wa Marekani, lakini naona kama unaharibu hoja yako nzuri na zenye mtiririko wa kuvutia, kwa kuchanganya siasa za CCM (Tz/Africa) na siasa za wamarekeni ambao wanafahamu nini maana ya demokrasia..

Ukiangalia siasa za CCM hazina tofauti na siasa za vyama vya upinzani ukichukulia mchakato mzima wa kuwapata wagombea urais..Rejea kwa Dr.Slaa hajulikani lini wapi na nani waliomchagua agombee urais au kituko ni hili la Lowassa nilitegemea viongozi wetu wawe na mishipa ya aibu walau wamshindanishe na wagombea wengine lkn hicho hakikutokea..

Sitaki kuharibu mtiririko wako ila nitafarijika zaidi kama utajikita zaidi US hizi siasa zetu ni kituko.. kma utapenda lakini..Samahani kama nimekukwaza....
 
Alinda wala hatujaondoka katika hoja za marekani na wala hazitaingia siasa za Tanzania .Ilikuwa by the way kuonyesha wenzetu walivyokomaa katika mambo haya.

Hoja yako imezingatiwa sana na ahsante kwa maoni
 
IDADI YA WAJUMBE INAYOTAKIWA 'KUBEBA BENDERA'

Ipo idadi ya wajumbe mgombea anahitaji ili kuteuliwa (nomination)
Idadi hiyo inapatikana kama tulivyoeleza mabandiko yaliyopita

Democrat: Idadi inayotakiwa ni 2,383
Hadi jana hali ipo kama ifuatavyo

Hillary Clinton ana wajumbe 1,132
Bernie Sanders ana wajumbe 818

Idadi hiyo ni pamoja na super delegates tuliowaeleza hapo juu.
Super delegates wanaweza kubadili mwelekeo wakati wowote

Tuttoa idadi ya wajumbe wa kushinda baadaye kidogo

Republican: Idadi inayotakiwa kupata nomination ni wajumbe 1237
Donald Trump ana wajumbe 661
Ted Cruz 405
Rubio 169 (kajitoa)
John Kasich 142

Ikumbukwe kuna majimbo mengi hayajafanya uchaguzi. Kati ya hao, California na New York zina wajumbe wengi.

Lakini pia yapo majimbo yenye ushawishi wa aina fulani
Kwa mfano, Arizona ni jimbo lenye tatatizo la wahamiaji haramu

Katika jimbo hili, mtinange mkubwa upo katika republican.

Je, kwa 'sera' za Trump dhidi ya wahamiaji kuna anayeweza kumshinda kati ya Cruz na Kasich? Na je, wafuasi wa Rubio wataelekea upande gani miongoni mwa hao wawili

Tutaendelea
 
KWANINI BERNIE SANDERS ANAENDELEA NA KAMPENI?

Matokeo ya jana yalikatisha tamaa upande wa Mr Sanders Aliwekeza sana Ohio na Illinoi

Kusini, Sanders alitambua ushindi Florida na North Carolina ni mgumu.

Kwa kiasi fulani uamuzi wa kuchagua maeneo ulikuwa ni 'risk'
Aliamini anaweza kushinda Ohio na Illinoi, hata kama si kwa wingi wa wajumbe

kwamba hoja ya kushinda maeneo muhimu ingemsaidia sana

Risk aliyochukua imemgharimu, Florida, Ohio, Illinoi na Missouri amepoteza
Florida na NC zimemuumiza sana

Bi.Clinton alishinda asilimia nyingi.Kwa utaratibu 'proportion' Mr Sander alipoteza wajumbe

Hoja iliyopo, kwanini aendelee na kampeni ikiwa hesabu haziendi vema?

Hesabu zasema lazima ashinde chaguzi zilizobaki kwa asilimia kubwa
Jambo hilo linaloonkena kutokuwa rahisi kwa kuangalia ramani

Anachokifanya ni kuhakikisha anashinda hata kwa asilimia kidogo
Atajenga hoja ameshinda maeneo mengi ramani ikiangaliwa kwa upana wake

Na ukweli ni kuwa sehemu ya majimbo yaliyobaki inatumia utaratibu wa Caucus, Sanders ana nafasi. Ushindi anaoutaka si asilimia kubwa, bali kushinda hata kwa point moja

Dem watakapoangalia ramani itaonekana ameshinda eneo kubwa ingawa hana wajumbe wa kutosha.Ndipo Super delegates wanapoweza kubadili mwelekeo

Kumbuka wanaruhusiwa kumuunga yoyote kwa wakati wowote

Kwa Bi Clinton ukweli huo unampa wasi wasi na anatmbua safari bado ipo!

Kampeni kwa Dem zaweza endelea kwa muda mrefu ikiwa Sanders atapenda

Tusemezane
 
Back
Top Bottom