Elections 2010 Uchaguzi mdogo Igunga (UPDATES): Upigaji Kura

Status
Not open for further replies.

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,418
Reaction score
9,209
Upigaji kura unaendelea huko Igunga. Watu wengi wamejitokeza na kura zinaendelea katika hali ya amani na utulivu.

Waliojitokeza kwa wingi ni wazee na kina mama.

-------------------
CLOSED: KUPATA MATOKEO FUATILIA THREAD HII - MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO IGUNGA

05:24 PM - Mbowe on Channel 10: Tumeripoti vitendo vingi vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu lakini vyombo vya dola havichukui hatua

05: 10 PM
Mwigulu Nchemba on Channel 10: Ktk kata ya Nhongo (Igunga) kuna mwanamke kapewa karatasi ya kura huku ikiwa imetikiwa sehemu ya mgombea wa CHADEMA


05:04 PM


05:00PM - KURA SASA ZINAHESABIWA KATIKA VITUO



Esta Bulaya live MTV.

Anasifia polisi.

Anasema kinamama, wazee wamejitokeza kwa wingi.

anaulizwa kuhusu mwamko wa vijana.

Anajibu, ati kwamba amekuwa sapraizdi kwamba vijana hawajajitokeza kwa wingi.
TBC imeripoti zoezi la kupiga kura Igunga na kumwonyesha mwanamke anayejipambanua kuwa ni wa CHADEMA ambaye amesema balozi mmoja wa nyumba kumi kareport kuwa yeye kafariki dunia ili asipige kura kwa kuwa alikataa kuiunga mkono CCM.
 
naam asubuhi kumekucha, wananchi waigunga wakijazana vituoni kwa wingi, hali ya hewa ni nzuri na shuwari. vituo vimefunguliwa mambo yote yako mazuri hadi sasa nimo nikipita hapa na pale
 
Kwenye baadhi ya vituo watu hawaoni majina yao.

Mawakala wavutana kwani walikuwa hawatambuani lakini limetatuliwa.
 
OK! Pamoja na hayo wana-JF hawa watu ni wezi sana Waangalie hata namna masanduku yatavyo kuwa yana safirishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine humo kwenye magari pawe na raia wetu CDM,kumbukeni vitendo alivyofanya Mahanga Makongoro pale segerea wakati anabadilisha masanduku yake mwenyewe kama hayo yaliyopo Nzega kwa DC.
 
tatizo la kuhamisha majina ya watu kutoka vituo walivyopiga kura 2010 na kuwapeleka vituo vingine limeanza kuonekana
 
vipi kuhusu vituo hewa?hivi cdm ina mawakala wa kutosha vituo vyote?
 
Uchaguzi mdogo wa Igunga unafanyika leo ambapo vyama ninane vinashiriki (tofauti na vyama viwili tu uchaguzi wa 2010) Nani kuvuna nini ni hapo jioni maana kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi matokeo yatatangazwa leo hii.

Kwa wale mnaopenda kufuatilia maendeleo ya yanayojiri Igunga ITV wana program maalum ya siku nzima ku cover uchaguzi huo
 
Wana JF Igunga tafadhali tupasheni yanojiri Igunga.

Updates kutoka kwa Wa Jikoni:

  • Hali ni tulivu.
  • Watu wamejitokeza kupiga kura asubuhi hii, wengi wakiwa ni kina mama.
  • Watu wanahakiki majina yao.
  • Hakuna malalamiko, so far
 
vipi kuhusu vituo hewa?hivi cdm ina mawakala wa kutosha vituo vyote?

inao wa kutosha kwa mjibu chanzo kilichoko huko igunga kwa vita hii ukisikia chadema hawana wakala kituo fulani itakuwa ni upumbavu kwasababu makama kutoka mikoa mbalimbali wako tayari kwenda kusimamia na nec imeruhusu mawakala kutoka mikoa mbalimbali..
 

Nani hao? CHADEMA?
 
Ngoja tukawaombee CHADEMA kwanza....tutarudi baadaye...!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…