Asubuhi nimefika hapa mjini Igunga nikitokea mji mdogo wa ZIBA, huko hali shwari vijana wamefurika kwenye vituo vya kupigia kura karibu vyote hapa mjini ila kwenye miji midogo ya MWISI, NGONGORO, SAKAMALIWA, IGURUBI, CHOMACHANKORO, juzi na jana hali nilishuhudia ilikuwa safi. Nimefika Igunga wiki hii na nimefanya utafiti katika sehemu tajwa hapo juu. Nimewahoji wananchi 53 kila mji. CHADEMA imeteka Igunga kama kweli uchaguzi utafanyika kwa amani na "usawa" leo. Ila walimu walioanza kazi mwaka jana wa Igunga wamezuiwa kupiga kura. Wenyewe wanalalamika kunyimwa fursa ya kumchagua mwalimu mwenzao. Nitaupdate wakati wa kukusanya idadi ya kura matokeo. nimeacha namba zangu za simu ktk miji yote ya igunga.