Asalamu alaykum.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni umefanyika kwa usalama na amani na hakuna udanganyifu uliofanyika katika upigaji kura kwa ile jana tatizo kubwa lilikuwa wakati wa uandikishaji kuna watu wengi sana walikataliwa kuandikishwa kutokana na kutokuwa na vipande vya ukaazi ambavyo waratibu wa vipande hivyo ni viongozi wa serikali za mitaa (masheha) wanatuhumiwa kutoa vipande hivyo kwa ubaguzi mara nyingi hukataa kuwapa watu wenye asili ya pemba.
Tatizo jengine sio kama watu wamechoka na upinzani lakini kutokana na hali za maisha zilivyo ngumu wananchi wanachoka kukipa chama ambacho kila kinapotokea uchaguzi kinakoseshwa ushindi hivyo wananchi wengi wamekata tamaa lakini kubwa zaidi kuliko yote wananchi wengi hawana elimu ya uraia na hivyo wamekuwa wakitilia chama ambacho wanaamini hata kama hukukipa kitashinda tu kwani mara kadhaa viongozi wake wamesikika waksiema hawatoi nchi kwa kura kwa kuwa wamepindua.
lakini pia wananchi wengi hawajajitokeza kupiga kura kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuvunjika moyo, kuogopa kwa kuwa kila uchaguzi unaofanyika zanziabr huwa hauna salama lakini zaidi kazi ya kuihamasisha jamii haikuwa kubwa hivyo wananchi wengi wameona huu ni uchaguzi ambao hausaidii kitu katika kubadilisha utawala.
kila la kheri huo ni mtazamo wangu