Pre GE2025 Uchaguzi mkuu 2025 tutegemee wagombea wenye sifa kutoka CCM wakienguliwa na wasio na sifa wakipitishwa na kusimamiwa waende bunge bila kupigiwa kura;

Pre GE2025 Uchaguzi mkuu 2025 tutegemee wagombea wenye sifa kutoka CCM wakienguliwa na wasio na sifa wakipitishwa na kusimamiwa waende bunge bila kupigiwa kura;

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Chama cha siasa katika siasa za vyama vingi ujipima kukubalika kwake kwa kuruhusu wananchi kupiga kura

Kwa hali ilivyo sana nchni ni wazi hakuna tena utaratibu wa kupata viongozi kupitia uchaguzi bali viongozi wa kisiasa wanateuliwa na tume ya uchaguzi au wasimamizi wa uchaguzi

Ni vigumu kusema huu ni msimamo wa chama cha mapinduzi au la, kwani hata wanachama wa chama hicho nao wanaandamana kukatwa majina kwenye chaguzi za ndani.

Wana CCM kwa siku za hivi karibuni wameogopa kabisa hata kuvaa nguo za chama wala kupeperusha bendera za chama maeneo mbalimbali. Wana CCM wamekuwa wanyonge kuchangia mada kwenye majukwaa mbalimbali kwa sababu kila wakisimama wanaonekana watu wasio na akili na maarifa bali wanategemea kusaidia kila jambo.

Kwa kifupi Tanzania wakati majirani zetu wakiimarisha mifumo ya uchaguzi na kujenga trust Duniani sisi tunabomoa mifumo ya uchaguzi na kuiga mbinu na mikakati ya mataifa yanayoongoza kwa mkono wa chuma.

Tumeona mfumo wa uchaguzi Kenya, S. Africa, Botswana, Ghana nk hakuna taarifa za wagombea wa kisiasa kukatwa majina. Mfumo wa ukataji majina upo kwenye nchi ambazo usiku na mchana kuna uvunjifu wa amani.

Najiuliza, kama wana CCM wanatamani na wao wawe huru kwenye nchi yao kufanya siasa lakini mfumo unakataa! Nani yupo nyuma ya uchafuzi huu.?
 
Back
Top Bottom