Uchaguzi mkuu TFF,Shaffih Dauda adakwa na takukuru kwa rushwa!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986


---------------------------------------------------
Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamekamatwa jijini Mwanza.

Baadhi ya waliokamatwa ni pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Shaffih Dauda, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo.

Imeelezwa walikamatwa jana saa tatu usiku jijini humo wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma na Kelvin Shevi.

Msemaji wa Takukuru jijini hapa, Ernest Makale amethibitishwa kukamatwa kwao na kusema wamehojiwa.

“Tumewahoji na kuwaachia kwa dhamana, sasa uchunguzi unaendelea,” alisema.

Imeelezwa watuhumiwa walisema kwamba walifika jijini Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup jijini humo.
 
Shaffih Dauda anajiharibia sana na sijui ni kwanini hataki ' kutosheka ' na alichonacho. Hii si dalili njema Kwake hata kidogo na tayari ' Credibility ' yako itaanza kushuka. Mimi ninavyojua ni kwamba Mtu yoyote aliye ' smart ' hasa ' upstairs ' hawezi kutaka kujihusisha na masuala ya ' Soka ' hasa hili la Tanzania ' lililolaaniwa ' Kitambo na Mzee wetu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi.
 
Sasa nimeamini kuwa Mtemi Ramadhani atakuwa Mwenyekiti kadiri ya matwaka ya system
 
Shafii mtu wa kuchongachonga sana anatakiwa apigwe chin I fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…