Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Sijui ni lini uchaguzi Mkuu wa Chadema utafanyika japo nakumbuka ulikuwa ufanyike katikati ya mwaka huu. Kwa vile muda uliobakia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ni kama mwaka mmoja na nusu tu, je:
- CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa
- Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?
- Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?
- Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini? Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?
- Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?
- Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?
- Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?
- Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?